MKEHA
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 714
- 1,137
Kwa urembo na uzuri wa mama, wanaume wengi walipenda kuwa nae ili awe mke wao. Lakini kati ya wanaume hao wengi ni baba tu aliyebahatika kumuoa mama. Baba alijitahidi sana kuchakarika ili familia yake iwe njema kwa kufanya kazi zake kwa juhudi kubwa sana na maarifa.
Na ni kweli toka nizaliwe sijawahi lala njaa kwani baba anajitahidi sana kuleta sembe, mchele, maharage,mafuta, sukari na vyakula vingine kede wa kede.
Pamoja na kuwa mama aliolewa na baba lakini kumbe bado wale wanaume wengine walikuwa na nia nae waliendelea kumfuatilia mama wakitamani baba atoweke siku moja ili wapate nafasi ya kumchumbia tena mama.
Kuna siku baba aliacha kwenda kwenye kijiwe cha kahawa ambapo alikuwa akikutana na wenzake kupiga stori baada ya muda wa kazi, zilipita kama siku tano hizi bila kufika kijiweni wala kuoneka kwenye mishe mishe zake. Lakini pamoja na hayo yote sisi tuliendelea kula kama kawaida na huduma zingine ziliendelea kama kawaida.
Sisi kama familia tulijua kila kitu kuwa baba yupo ila ameamua kuishi tofauti na watu walivyo zoea kwamba muda baada ya kazi lazima aende kijiweni kwa mzee Ntiruhungwa anywe kahawa huku mazungumzo mengine ya siasa na michezo yakiendelea. Baada ya kubadili mfumo wa maisha yake acha vurugu zianze sana nyumbani kwetu.
Wale wanaume waliowahi kumchumbia mama wakaanza visa, mara warushe mawe juu ya paa la nyumba yetu, mara mawe kwenye madirisha yetu. Ilikuwa ni kama vita.
Wengine wakitoka vilabuni wanaputa karibu na nyumbani kwetu wakiimba nyimbo za kashfa juu ya baba yetu. Lakini familia yetu kimyaaaaaaa.
Wanaume wengine walifikia hatua ya kwenda kwa viongozi wa dini wakitaka eti ndoa ya baba na mama ivunjike kwani baba hatimizi tena wajibu wake kwa mama kana kwamba wanalala chumbani kwa wazazi wetu. Walishinikiza watoto tuseme baba alipo, tulipewa pipi, biskuti na zawadi nyingine ili tusema wapi baba alipo.
Kuna wengine walikuja na barua za posa wakutaka mama aolewe tena kwani mmewe ambaye ni baba yetu hawamwoni tena kijiweni na ile tabia ya kutupigia hadithi usiku wapita njia hawaisikii tena.
Tulifuatwa kila sehemu tuseme wapi baba alipo. Baada ya siku kupita mara huyo, Stori itaendelea wiki ijayo. USIKOSE KUFUATILIA KISA HIKI SIKU NYINGINE