Mama aibiwa mtoto kliniki Mkoani Morogoro

Mama aibiwa mtoto kliniki Mkoani Morogoro

Huyu mama sijui ni ujinga au ni umri mdogo aliokua nao, sasa unamwachaje mtu anambeba mwanao kwenye bodaboda tofauti na uliyopanda wewe, na mtu huyo wala humjui.
 
Kweli tunatakiwa tuwe makini hasa pale unapokutana na mtu usiyemjua.
 
Duh! Tusiosoma tuna tabu

Mna tabu ndiyo. Kutwa nzima mume akiondoka tu remote mkononi, unapindukia kulia unapindukia kushoto, ni movie na wewe ...wewe na mikanda. Hujui hata kinachoendelea duniani. Tahadhari chungu nzima zinatolewa za matapeli wewe umeshupalia part 2 na 3... Kha!
 
Kazi kweli kweli.

Kwa majuu huyo mwizi angepatikana siku hiyohiyo kupitia kwa huyo bodaboda.

Hivi unajisikiaje kumtunzia mtu siri kama hii? Kwamba ana mtoto wa kuiba.

Hivi kuna masharti magumu mno kuasili (adopt) mtoto kwenye vituo vya kuleana.

Anyway,kwa kuwa hajaibiwa kizazi au kiungo cha uzazi,basi akape tena kajamaa kafanye yake.

NB.Wavute walau miezi kadhaa maana akipatikana huku wameshatwishana nyingine inakuwa soo.
 
hapa hakuna cha umaskini wala ccm maana mmekalili kila kitu ccm
Huyu ni mjinga mwenyewe kaenda kununuliwa sweta anapenda burebure angekitoa hiko kifaa akatoka nae nje kimya kmya
Unadhani waliotengeneza hicho kifaa ni wajinga kwamba mtu yeyote yule anaweza kukichomoa kirahisi, ingekua hivo kingekua na kazi gani sasa..... Alafu notice sijalaumu CCM, sina neno CCM kwenye sentensi yangu, mi shida yangu ipo na tanzania nzima, sio CCM sio Kuku sio bata doesn't matter, tumeshindwa kuhandle every sector
 
hivi kweli mtu unaweza kuiba mtoto? Hivi unamwambia mme wako kuwa umejifungua? Hiv mimi niishi na mke nisijue kama mjamzito au la? Huu ni ushirikina tu!
 
Hapo walipochukua bodaboda ndo pa kuanzia,aliyembeba yule mama mwizi atasema wapi alimshusha.

Kweli afanye uchunguzi kuanzia aipochukua bodaboda, afatilie ataweza kumpata, ingawa amefanya uzembe sana lakini dah! Amuombe na Mungu akute hai maana wengine wanawatoa kafara au kuwapeleka mbali sana
 
Huyu mama sijui ni ujinga au ni umri mdogo aliokua nao, sasa unamwachaje mtu anambeba mwanao kwenye bodaboda tofauti na uliyopanda wewe, na mtu huyo wala humjui.

Wakati mwingine huwa wanakuja na dawa za kukupumbaza unafata kila anachokuwa anakuambia so tusimlaumu sana
 
Uchaguzi wa mwaka huu kuna kazi! By the way, hawa CCM hawajaridhika na viungo vya albino hadi wanaparamia na vitoto vichanga!
 
ANAYEDAIWA MWIZI WA MTOTO ANASWA!




Dustan Shekidele, Moro
SIKU chache baada ya gazeti hili kuripoti kuibiwa kwa mtoto lrene Daniel mwenye umri wa siku 34, mkazi wa Kilakala, mkoani hapa, habari njema ni kwamba mwizi wa mtoto huyo amenaswa laivu,Ijumaa Wikienda lina full stori.

Mama aliyeibiwa mtoto wake Mei 8 mwaka huu mkoani Morogoro.Mtoto huyo aliibiwa kimafia Mei 8, mwaka huu wakati mama yake Martha Masawe akiwa kwenye foleni katika Kliniki ya Nunge mkoani hapa.
Baada ya habari hiyo kuchapishwa Mei 10, mwaka huu, wananchi wa Kitongoji cha Mikumi Wilaya ya Kilosa mkoani hapa walimtilia shaka mkazi mwenzao Jesca Patrick (23) ambaye ghafla alionekana akiwa na mtoto mchanga mara baada ya kutoka Morogoro mjini wakati hawakuwahi kumuona akiwa na ujauzito.

Mama anaedaiwa kuiba mtoto ambaye alifahamika kwa jina la Jesca.“Waliposoma habari ya kuibiwa mtoto gazetini halafu ghafla wakaona Jesca ana mtoto mchanga, wakamtilia shaka na kutoa taarifa polisi katika Kituo cha Polisi cha Mikumi, akakamatwa,” kisema chanzo chetu.
Mama aliyeibiwa mtoto akiwa na aliyedaiwa kuwa mwizi wa mtoto wake.
Mwanahabari wetu alifika kituoni hapo na kumshuhudia Jesca akiwa chini ya ulinzi wa polisi ambapo alipoulizwa kama ni kweli alimuiba mtoto huyo, alikiri kutenda kosa hilo na kuomba asamehewe.
”Siwezi kubisha ni kweli nilifanya jaribio la kumuiba mtoto huyo kwani nilifanya juhudi za kuzaa lakini bahati mbaya mpaka leo sijabahatika kupata mtoto hivyo naomba mnisamehe,” alisema Jesca ambaye ni mkazi wa Mikumi.
Kwa upande wake Martha, alikuwa na haya ya kusema:
“Kwa kweli nalishukuru sana gazeti hili, yaani nilitamani nife kwa kumkosa mwanangu. Pia nalishukuru jeshi la polisi kwa kufanikisha kumpata mtoto wangu akiwa hai na afya njema na kumtia mbaroni mtu aliyemuiba,nimefurahi sana,” alisema Martha.


 
Back
Top Bottom