Mama aibiwa mtoto kliniki Mkoani Morogoro

Mama aibiwa mtoto kliniki Mkoani Morogoro

Lugano5

R I P
Joined
Jul 15, 2010
Posts
4,520
Reaction score
759
View attachment 250877
Martha Masawe akilia kwa uchungu baada ya kuibiwa mwanae.

Inauma sana! Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Martha Masawe (20), mkazi wa Kilakala mkoani hapa, ameibiwa mtoto mchanga mwenye umri wa siku 34 akiwa katika Hospitali ya Nunge, Ijumaa Wikienda lina ‘full' stori.

Tukio lililofanywa kimafia lilijiri Ijumaa iliyopita saa 7:00 mchana wakati Martha akiwa kwenye foleni.

Akihojiwa na Ijumaa Wikienda huku akiangua kilio hospitalini hapo Martha alisema:

"Usiku wa kuamkia leo (Ijumaa) mwanagu alikohoa sana, asubuhi baba yake aliniambia nimlete hospitali kucheki kifua.

"Nikiwa kwenye foleni alikuja mama mmoja, akaomba amshike mwanangu huku akisema ni mzuri.

"Baadaye aliniuliza ana tatizo gani? Nikamwambia anaumwa kifua, akanishauri twende dukani tukamnunulie sweta.

"Tulikwenda maduka ya Kikundi tukanunua sweta na nguo nyingine kisha kila mtu akapanda bodaboda yake tukaanza safari ya kurudi hospitali.

"Chaajabu nafika hapa hospitali nimekaa zaidi ya nusu saa yule mama hajatokea. Nikawasimulia manesi wakadai tayari nimeibiwa mtoto."

Baadaye mama huyo alipata msaada wa askari wa doria, afande Mwajabu aliyeongozana naye kwenda kituo cha polisi kufungua mashtaka na namna ya kumuelewesha mumewe.


Chanzo: GPL
 
hajaibiwa bali ametapeliwa. inasikitisha sana.
ila nshindwa kuelewa ilikuwaje awe tayari kwenda dukani kununuliwa sweta na mtu asiyemjua?
Wamama muwe makini na wa mama wenzenu mnaowachia watoto wachanga
 
pu.MBA.vu huyo anamwachaje MTU mwingine aondoke kwenye bodaboda na mwanaye???angekuwa mke wangu bora asirudi nyumbani,apotee huko huko.wakinamama be careful na watoto wenu
 
Inauma sana aise, mama wa mtoto kafanya kosa kubwa mno:
1. mtu humjui anakutaka muongozane kununua sweta unaenda tu...we hukuona umuhim huo mapema?
2. umenunua sweta sawa, iwaje unadiriki kupanda pikipiki tofauti na mwanao ili hali huyo msamaria uchwara humfaham?
damu yako kweli unaachia kizembe hivi....matapeli wengi huja ma roho ya usamaria ili wakutapeli kirahisi.
Kinamama: Kuweni makini sana wapendwa, si dhani kama kutosoma ni tatizo kwa sababu akili ya maisha ni mtu mwenyewe haitegemei moja kwa moja kusoma...kwani wasomi hawatapeliwi??
Yote kwa yote pole sana kwa familia husika.
 
pu.MBA.vu huyo anamwachaje MTU mwingine aondoke kwenye bodaboda na mwanaye???angekuwa mke wangu bora asirudi nyumbani,apotee huko huko.wakinamama be careful na watoto wenu

Kafanya uzembe sana huyo mama...
 
Wanawake wasiosoma nao wakati mwingine kuwaoa ni ishu! sidhani kama baba wa mtoto hajamnasa makofi.

Akili ya maisha haitegemei kusoma tu, huyo mama ni mzembe kupitiliza natumai mumewe atakuwa kamlipua makofi japo haisaidii kumpata mtoto lakin itamfanya mkewe kuwa makin wakati mwingine na kutorudia ujinga aliofanya.
 
hahahahahah kwa hili nimecheka sana huyu mzazi gani mbona akili zake kazi restisha in peace
 
vitu vingine bana. huyo mama kuona mtoto anaenda kununuliwa sweta akajua ni malaika alieshuka akalegea adi kuachia mtoto kipumbavu.
 
daah kweli ni mzembe lakini inauma sana hakutegemea
kama mwanamke namuonea huruma sana.....hapo tumbo la uzazi lina maumivu na uchungu kama anazaa tena
 
Duuh sasa sjui huyo mtoto anapelekwa wapi!! Inasikitisha sana
 
Hapo walipochukua bodaboda ndo pa kuanzia,aliyembeba yule mama mwizi atasema wapi alimshusha.
 
Lakini umri wake pia wa miaka 20 umechangia. Sasa kama huyo mwizi aliweza kupanda bodaboda na mtoto yeye alishindwaje? halafu kuna wakati huwa naona umuhimu wa kusoma magazeti ya shigongo maana hizi kesi za kuibiwa watoto huwa zinaandikwa sana kwenye hayo magazeti na wateja wakubwa wa hayo magazeti ni wanawake sasa sijui huwa wanasoma hadithi tu hawasomi matukio yanayoandikwa humo?

Mimi ni mwanaume ila nimeumia sana kwa kitendo cha kuibiwa mtoto bila kujali ni uzembe au la. Lakini kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano ni rahisi kumpata huyo mama kwani majirani watajua huyu hakuwa na mtoto kampata wapi? vinginevyo awe alitengeneza mimba feki.
 
Back
Top Bottom