Malumbano ya Spika Sitta na Mzee Mrema


Sitta aliufunga mjadala wa richmond kulingana na hoja za kamati na wala hoja ya richmond haikuwa ya Sitta. Na mapendekezo 23 yalikiwa ni ya Bunge kwa kauli moja wala hayakuwa ya Spika. Yeye spika ni kama referee tu na sii mchezaji. Kama mafisadi wamefunga goli kwa usaidizi wa NEC ya ccm inabidi refa alikubali goli na wala kamwe hawezi kuliita corner kick. Wakulaumiwa ni wale wabunge wanakamati kwa usaliti wao kwa umma na wala sii spika. Sisi nasi sote tumeleweshwa bangi ya propaganda za mafisadi?
 
Mrema kama jina lake ni "Memavu" tu...
Mtandao unafanya kazi vizuuri, ila safari hii umepitia choo cha kike. Kweli wanamtumia mtu kama mrema kupambana na watu makini kama Sitta!?
 

AK usiwe moungo ni wapi Sitta ameongelea Richmond nje ya bunge nionyeshe kule Songea alichosema ni kuhusu kutaka kunyang'anywa kadi ya CCM kama unataka tuamini kunyang'anywa kadi kunahusiana na Richmond sema

hata hivyo mambo yaliyofungwa ndani ya bunge nani kakuambia hayawezi kuongelewa nje au kwa vile umemsikia Mrema kasema hivi utekelezaji wa mambo ya bunge hufanywa ndani au nje ya bunge mambo ambayo hayatakiwi kuongelewa ni yaliyo mahakamani tu
 
Hivi Mrema anaona bunge lile la Msekwa lililomwambia ubongo wake(Mrema) umejaa matope, ni bora kuliko hili la sasa?
Kweli pesa ina nguvu za ajabu!
 
Sitta takes swipe at Mrema on Richmond

By Dominic Nkolimwa
5th March 2010


Speaker of the National Assembly Samwel Sitta



Speaker of the National Assembly Samwel Sitta has accused Tanzania Labour Party (TLP) chairman Augustine Mrema of distortion that he (Sitta) has breached the law for harping on the Richmond issue while discussion on the matter has been closed.
Sitta said Mrema might have been bribed to indulge in delibarate distortion simply to defame him.
Mrema told reporters at a press conference yesterday that Sitta had breached the law by reopening discussion of the Richmond issue while parliament had put a lid on it.
However, Sitta refuted the claims, saying he had not opened debate on the matter.
"Mrema is talking about something he is not conversant with, which goes to show that he is politically bankrupt," he said.
He said he had always been speaking the truth, adding that is why he had many enemies.
"Probably Mrema is being used by those enemies, because there are no facts and no connection whatsoever with what he has said and the truth," he said.
Mrema, in his allegations, asked the Speaker to resign from his position, failure of which he should be removed because he was threatening the country's peace and harmony.
He said Sitta had shown his stance during the Richmond debate in parliament while, as speaker, he was supposed to be impartial.
Mrema said further that Sitta was one of the anti-corruption team which was waging a crusade against graft throughout the country.
However, Sitta refuted the claims, saying he had never travelled to any region with the said team as alleged by Mrema.




SOURCE: THE GUARDIAN
 

Je wambunge wa upinzani walilithika na maamuzi hayo? na je wambunge wote wa CCM walilithika? na kama yeye spika na mpiganaji, hakuwa na uwezo wa kupendekeza mapendekezo ya kufanya maelezo na maoni ya upinzani (which is manority to the parliment) kusikilizwa na kutafakariwa zaidi bungeni? I think kama Sitta ni mpambanaji wa kweli it was his responsibility to honour tanzanians and put his personal benefits aside.
 

Heshima kwako pia F-T, ninachosema hapa spika has done what it was supposed to be done by HIM, yeye hakuufunga mjadala umefungwa na kamati ya bunge ya CCM yeye kasoma tu maazimio ya kamati ambayo hata Anna Makinda angesoma tusitafute visingizio source ni Richmond wasingefanya madudu leo tusingeongea hili yeye tumsifu kwa kutufumbua macho vingenevyo lingekuwa limeshakwisha bila wewe na mimi kujua
 
maradhi yamempofusha, maradhi yanamnyong'onyesha.
Kweli naamini adui yako muombee njaa, leo Mrema anachukua nafasi ya Tambe Hiza, amekua Mwanapropanganda wa CCM, amakweli hawezi kusema wazi, ila leo anaujutia ule uamuzi wake wakujitoa kwenye chama hicho, mimi namsamehe, kwa maana namuona anaumwa, na ukichanganya na uzee, ndo kabisa, sasa uwezo wake wamaamuzi unaendana na mtoto Darasa la nne, POLE LYATONGA, POLE MREMA.
 

Sawa kabisa. Ni vyema wa-Tanzania wakaelewa ukweli kwamba nchi yetu ni ya udikteta wa chama kimoja. Sitta na wenzake hata kama hawakuridhika na uamuzi huo ambao ni wazi ni msimamo wa NEC ya CCM hawana ubavu wa kwenda kinyume labda watangaze uasi rasmi. Na hapo hatujui kitakachotokea kwao. Na sijui kama wakifanya hivyo wananchi watainuka kwa wingi na kusimama kidete pamoja nao dhidi ya dola iliyodhibitiwa kikamilifu na CCM.

Mimi binafsi namuelewa Sitta anapotumia majukwaa ya nje kuonyesha hisia zake za kutoridhika ingawa sijisikii comfortable na hali hiyo. It shouldn't be like that at all. Lakini ndiyo Tanzania yetu hiyo.

Na Mrema si mtu wa kumsema Sitta kwa hayo. Nategemea huyu mzee akiwa mpinzani mwenye cv kubwa (nakubali kusahihishwa) aelekeze nguvu zake zaidi kwenye kupigilia nyundo kwenye yale ambayo akina Sitta na wenzake wameshindwa kuyafanikisha ndani ya chama chao. Aongeze nguvu kwenye kupiga vita mfumo wa kifisadi uliogeuka kuwa taasisi ndani ya serikali na hususan taasisi nyeti za kiuongozi, kiuchumi na kisiasa.

Kumkosoa Sitta dhidi ya maamuzi ya chama chake (CCM) si jukumu la Mrema - awaachie CCM msiba wao. Kimkakati yeye anatakiwa kubakia kuwa kiongozi wa upinzani - aongelee yale ambayo yanajenga upinzani wa kweli badala ya kuimarisha uozo tunaouona hivi sasa. Vinginevyo abwage manyanga rasmi tusiendelee kumuona mpinzani mbabaishaji.
 

Ndugu yangu MP kuna watu wanataka kutuchanganya kama makande lakini hatuchanganyiki kirahisi, kwenye ishu hii kuna sehemu tatu
1. Source: Richmond=EL, RA, Hosea nk kama wezi
2. Bunge: Wapambanaji=Sitta nk kama mahakama
3. Mtekelezaji: Serikali=Rais nk
Sasa watu wamevuka na kuacha sehemu zingine kama vile hazihusiki wanakazania sehenu ya pili hasa Sitta ka vile alikuwa peke yake tujiulize wahusika source kina Hosea wamefanywa nini na mtekelezaji amefanya nini

Ningemuona Mrema wa maana kama angehoji Rais amefanya nini mbona yuko kimya Rais ameliacha bunge bila support lakini yeye Mrema na baadhi yetu tunalaumu watu ambao angalau wanajitahidi this is not fair enough je vipi kundi ambalo si la wapambanaji wao wako kwenye lawama au tunawapongeza kwa kukaa kimya
 

Kwani malumbano hayo ni kati ya nani na nani kama sio Sitta na Mrema? Sitta anamjibu Mrema binafsi, hapo sio Speaker na Mwenyekiti.
 

Fair enough, but my big question is that, Sitta kama Mpiganaji kwanini alikubali kusoma maazimio ya Kamati ya Bunge ya CCM ambayo anajua na alijua kwamba inalenga kutetea ufisadi na sio kuimalisha maisha ya mtanzania? What he did was wrong and I still do believe as a spika he had everything in his power to take this further… and what he read that day was more to do with protecting his own income na posho..

kwa hiyo he should be the last person kwenda kwenye makanisa/msikitini na kusema CCM ni mafisadi.. By the way what what is he still doing in CCM kama ni mafisadi? Why cant he join opposition or start his own political party ambacho kitakuwa na morals?
 

Sikumbuki, hivi Mrema alisema lolote pale Rostam Aziz alipoenda pale KKKT kujaribu kujisafisha dhidi ya tuhuma za ufisadi zinazomwandama? Mrema hapa anafanya kazi ya wapinzani wa Sitta walioshupalia avuliwe uanachama. Pia anataka ajiweke juu CC na NEC ya CCM ambao hawakubariki uhuni wa wanaotaka Spika anyang'anywe uanachama. TLP si ni tawi lingine la CCM?
 

Luteni, je rais ndie mwendesha bunge? ni kazi ya rais kusimamia hoja za kila siku bungeni? nimesahau civic yangu ya secondary school naomba unikumbushe..
 


Haswaaaaa! wakuu zangu tunachezewa akili zetu kama walio lala vile! Huko CCM na Bungeni kwenye sheria mh. Sitta katuvuruga sasa sielewi huko makanisani ndio kuna jipya gani, zaidi ya kutafuta kura za wananchi apate kurudi bungeni.
 

My big question is kwanini hao source wezi wa Richmond waliosababisha hili saga bado wanadunda mitaani tusiwasakame tumsakame mtu aliyesaidia kutuonyesha huyo mwizi hilo ndilo swali langu kuu
 
Spika sitta nae kafulia tuache kumpamba najiuliza ni kwanini alifunga mjadala wa Richadmonduli kiyamela badala ya kushinikiza serekali itekeleze maazimio yote ya bunge yeye kakimbilia kuzima mjadala.
If u can't fight them, Join them...
 
Luteni, je rais ndie mwendesha bunge? ni kazi ya rais kusimamia hoja za kila siku bungeni? nimesahau civic yangu ya secondary school naomba unikumbushe..

nafikiri tumeanza kuwa mbali kadri tunavyoendelea support ya rais si lazima aingilie shughuri za bunge wala mahakama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…