PostGE2025 Malumbano ya Hoja ITV- Maoni yangu ya nini kifanyike baada ya madhila ya MO29

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,866
Reaction score
4,252
Jana nimeangalia kipindi cha MAlumbano ya Hoja ITV, mwanzo hadi mwisho. Si kawaida yangu sana kutazama ila jana nimekimaliza. Niwapongeze wote waliohudhuria na kutoa maoni yao katika mjadala ule. Nami kama mwananchi na mdau nina maoni yangu kama ifuatavyo;

1. Mzee Nyerere aliacha maadui watatu ambao aliwaainisha vyema, yaani UJINGA, MARADHI, na UMASIKINI. Akasema ili tukabiliane nao ilibidi tuwe na mambo manne muhimu; WATU, ARDHI, SIASA SAFI na UONGOZI BORA. Bahati mbaya hadi leo hawa maadui bado tunao. Yale mambo manne tuliyopaswa kuwa nayo tumeshindwa vibaya sana kwenye mawili; siasa safi na uongozi bora. Sasa kwa rekodi hiyo na mtiririko wa matukio, hatima yake ndio ilifikia Oktoba 29. Bado hapajawa na nia thabiti ya kutaka kujifunza toka kwenye janga lile. Upande wa pili bado tukingali na wale maadui watatu. aliongezeka mwingine ambaye no HOFU.

Raisi aliyepo sasa (Samia) alipokuja na zile 4R (Resilience, Rebuild, Reform na Reconciliation). ni wazi kwamba kwa wakati ule hazikuwa na kazi ya kutosha ya kufanya na ndio maana hazikuzaa matunda, na badala yake hali ilizido kuwa tete kwa kufungia upinzani na wapinzani kuwekwa jela.

Tukizungumzia Resilience ni neno zito sana. Ustahimilivu. Kama huna ustahimilivu. Kama huna ngozi ngumu, bora usijihusishe na siasa. Siasa haitaki mihemko, chuki, pupa, wala hasira,. vinginevyo madhara yake ndio kama tuliyoyashuhudia. Zile 4R ndio wakati wake sasa. Reconciliation ni pamoja na kukiri kuwa kuna upotevu wa maisha wa kiasi kikubwa ulitokea. Ni pamoja na kuwajibika. Kama hatawajibika mtu/watu ni wazi kuwa hakutakuwa na tija.

2. Kuhusu katiba, imezungumzwa vya kutosha. Liko wazi na bayana

3. kuhusu vyombo vya habari. Hapa kuna shida kubwa sana. Jana nimeona waendesha mada wakitaka kumfokea mtoa hoja, ila ukweli unabaki pale kuwa vyombo vua habari vimetekwa. Haiwezekani yatokee yote yale halafu pasiwe na chombo hata kimoja cha ndani kiichoripoti matukio ya hiyo siku. Mauaji na vurugu na uharibifu wa mali. Kuja kuendesha mada ya nini kifanyike leo ni udhaifu mkubwa.

Vyombo vya habari vimedhibitiwa. Haiwezekani mkuu wa mkoa aseme kuwa kuhusu taarifa ya yanayoendelea ndani ya nchi wananchi na jumuiya ya kimataifa izingatie taarifa toka vyombo vya ndani na sio vinginevyo. Kwa lugha nyingine huwa yanatokea mambo mengi nchi hii na hatupewei taarifa. Hata tukio la Polepole lilipita hivihivi. Vyombo vya habari viwe na mamlaka kamili na vipate nguvu toka umoja wa vyombo vya abari vya kimataifa na kuacha kutegemea serikali kwa utashi na ufadhili. Shida huanzia kwa hawa wakuu wa vyombo kununuliwa. Balile wa leo sio yule tuliyemjua miaka 5 nyuma.

3. Matamko ya wanasiasa yana madhara sana. Kuna wanasiasa wamepewa vyeo mbalimbali chamani na serikali. Hujikuta wao sio raia bali malaika fulani hivi. wako juu ya sheria. Yuuko mmoja anapenda sana biskuti. Mkuu wa mkoa huko kanda za juu kusini. Matamshi yake ni ya kibabe, kikatili, na yenye kubeba dharau kwa wengine. Huyu alisema wazazi wajiandae kuzika watoto wao. Leo kweli wamezika sana, na yeye yupo tu. Liwahi tena kutoa kauli tata huko nyuma, na badala ya kukemewa, huwa wanapewa vyeo.

Yuko mwingine kanda ya ziwa ambaye haoni shida kutamka hadharani kuhusu kupoteza watu kwa namna yoyote ile. Wapo wengine wengi. Ifike mahali vijana na watu hawa wakemewe vyema na mamlaka zitakazoluwepo (sio ccm) kwa lengo la kuondoa taharuki na chuki dhidi yao na serikali na chama chao.

4. Kuhusu polisi. Hawa ni donda ndugu. Polisi wametengenezwa kuwa maka maroboti. Kama mbwa. Wanatumwa kuuma na kudhuru bila kufikiri. Wanajisahau kuwa nao ni raia. Nao wana damu ka waliowaua. Wana ndugu zao mitaani. Kinachowaumiza asjkari ni ORDER/AMRI. Hizi amri huwa hazitakiwi kupingwa. Sasa ili kuleta muafaka, hizi amri nazo zihojiwe. Zipingwe. Kama amri ilikuwa ni %95 ya sehemu ya utendaji, basi sasa iwe %50. 50 amri, na 50 mantiki. Polisi akitumwa kudhuru awe na uwezo wa kufanya maamuzi na hatimaye kutakaa amri dhalimu na sheria imlinde dhidi ya wakubwa wake wanaotoa amri hizo dhalimu.

Tunasikia kabla ya matukio, polisi (hasa FFU) hupewa nangi na pombe ili kuwavuruga akili zao waweze kuonyesha ukatili wa kutosha kwenye operesheni zao. Hili lipo wazi maana haya Hayati Magufuli aliwahi kulizungumzia hilo - kuwapa polisi "cha Arusha" kabla ya operesheni. Polisi wakifikia hatua ya kukataa kutumika, jamii itakuwa na amani.

Tuendelee kuwaombea wale wote waliipoteza uhai ili wapate pumziko la amani milele. Ni imani yetu kuwa pakiwepo na haja ya jamii kutaka kufanya maandamano siku zijao, vyombo vya dola vijitafakari sana katika kutoa amri kandamizi zitakazopelekea uvunjifu wa amani na upotevu wa mali na maisha
 
Screenshot_20251113-171829~2.png
 
Hoja yangu iambatane na kipima joto cha leo Ijumaa.

Watu wanafunguka sana kuhusu yaliyotokea na kuainisha maeneo ambayo yanaoaswa kufanyiwa kazi. Tatizo linarudi pale kwamba wanashindwa kumuunganisha Rais na haya yanayotokea. Kitendo cha matokeo ya urais kushindikana kuhojiwa mahakama.za ndani ni uminywaji mkubwa sana wa haki. Kitendo cha tume ya uchaguzi kutohojiwa maamuzi yake ni ukandamizaji mkubwa sana wa haki. Sasa hatuwezi kuzungumzia haki wakati haki yenyewe imebakwa na wabakaji ndio ndio wako mstari wa mbele kutaka kuizungumzia hiyo haki.

Ilipaswa kabisa kuwa watu hawa wawekwe kando ndipo mazungumzo haki yaanze. Vinginevyo tuendelee kushuhudia vuguvugu nyingi
 
haya yote muasisi ni Magufuri
Acha ujinga Wewe na samia wako, Samia alivyoshika madaraka alisema anafungua nchi wakina lissu na lema walirejeshwa nchini tena kwa kulipiwa nauli na posho,ili Magufuli haonekane hakufaa, mpaka kaja na 4r, Sasahivi hapo Magufuli anausikaje! wakati mambo yake yote mliyaondoa.Bebeni msalaba wenu wenyewe Magufuli hausiki na haya.
 
wAsiojulikana,kuminya vyombo vya habari,kuua demokrasia na kujifanya mungu mtu muasisi ni huyo mshamba kutoka shamba chato

Na huu ujinga wake kuisha ni mpaka ccm iondolewe madarakan bila hivyo kila atakae kuwa rais kupitia ccm lazima achukue notice kutoka awamu ya tano
 
Mkuu Kuna sehemu niliona unasema uongozi wa sasa sio mbaya. Hapa mbona unaonyesha uongozi wa sasa ni mbaya tena kama uliopita?
Mkuu unanichanganya
 
Huu uongozi ulikuwa mzuri sana ila kuna hizo dosari za kukopi ya magufuri ndo yaliyouchafua,si unajua huyu ni mwanamke kushikwa masikio ni rahis nae ameingia mkenge
 
uzuri wake umeisha kabisa,akitaka uwe mzuri inabid ajiuzuru tu
Kwa nchi hizi za dunia ya tatu kusema uongozi fulani ni mzuri ni kujiongopea tu. Kuona uzuri wa uongozi fulani labda yawe mapenzi binafsi yanayotokana na sababu binafsi.

Hizi nchi zetu hakuna kiongozi hata mmoja anaingia madarakani kusaidia wananchi, wote kazi yao ni moja kukomba kilichopo na kusaidia familia zao na watu wao wa karibu.
 
Jana nimeangalia kipindi cha MAlumbano ya Hoja ITV, mwanzo hadi mwisho. Si kawaida yangu sana kutazama ila jana nimekimaliza. Niwapongeze wote waliohudhuria na kutoa maoni yao katika mjadala ule. Nami kama mwananchi na mdau nina maoni yangu kama ifuatavyo;

1. Mzee Nyerere aliacha maadui watatu ambao aliwaainisha vyema, yaani UJINGA, MARADHI, na UMASIKINI. Akasema ili tukabiliane nao ilibidi tuwe na mambo manne muhimu; WATU, ARDHI, SIASA SAFI na UONGOZI BORA. Bahati mbaya hadi leo hawa maadui bado tunao. Yale mambo manne tuliyopaswa kuwa nayo tumeshindwa vibaya sana kwenye mawili; siasa safi na uongozi bora. Sasa kwa rekodi hiyo na mtiririko wa matukio, hatima yake ndio ilifikia Oktoba 29. Bado hapajawa na nia thabiti ya kutaka kujifunza toka kwenye janga lile. Upande wa pili bado tukingali na wale maadui watatu. aliongezeka mwingine ambaye no HOFU.

Raisi aliyepo sasa (Samia) alipokuja na zile 4R (Resilience, Rebuild, Reform na Reconciliation). ni wazi kwamba kwa wakati ule hazikuwa na kazi ya kutosha ya kufanya na ndio maana hazikuzaa matunda, na badala yake hali ilizido kuwa tete kwa kufungia upinzani na wapinzani kuwekwa jela.

Tukizungumzia Resilience ni neno zito sana. Ustahimilivu. Kama huna ustahimilivu. Kama huna ngozi ngumu, bora usijihusishe na siasa. Siasa haitaki mihemko, chuki, pupa, wala hasira,. vinginevyo madhara yake ndio kama tuliyoyashuhudia. Zile 4R ndio wakati wake sasa. Reconciliation ni pamoja na kukiri kuwa kuna upotevu wa maisha wa kiasi kikubwa ulitokea. Ni pamoja na kuwajibika. Kama hatawajibika mtu/watu ni wazi kuwa hakutakuwa na tija.

2. Kuhusu katiba, imezungumzwa vya kutosha. Liko wazi na bayana

3. kuhusu vyombo vya habari. Hapa kuna shida kubwa sana. Jana nimeona waendesha mada wakitaka kumfokea mtoa hoja, ila ukweli unabaki pale kuwa vyombo vua habari vimetekwa. Haiwezekani yatokee yote yale halafu pasiwe na chombo hata kimoja cha ndani kiichoripoti matukio ya hiyo siku. Mauaji na vurugu na uharibifu wa mali. Kuja kuendesha mada ya nini kifanyike leo ni udhaifu mkubwa.

Vyombo vya habari vimedhibitiwa. Haiwezekani mkuu wa mkoa aseme kuwa kuhusu taarifa ya yanayoendelea ndani ya nchi wananchi na jumuiya ya kimataifa izingatie taarifa toka vyombo vya ndani na sio vinginevyo. Kwa lugha nyingine huwa yanatokea mambo mengi nchi hii na hatupewei taarifa. Hata tukio la Polepole lilipita hivihivi. Vyombo vya habari viwe na mamlaka kamili na vipate nguvu toka umoja wa vyombo vya abari vya kimataifa na kuacha kutegemea serikali kwa utashi na ufadhili. Shida huanzia kwa hawa wakuu wa vyombo kununuliwa. Balile wa leo sio yule tuliyemjua miaka 5 nyuma.

3. Matamko ya wanasiasa yana madhara sana. Kuna wanasiasa wamepewa vyeo mbalimbali chamani na serikali. Hujikuta wao sio raia bali malaika fulani hivi. wako juu ya sheria. Yuuko mmoja anapenda sana biskuti. Mkuu wa mkoa huko kanda za juu kusini. Matamshi yake ni ya kibabe, kikatili, na yenye kubeba dharau kwa wengine. Huyu alisema wazazi wajiandae kuzika watoto wao. Leo kweli wamezika sana, na yeye yupo tu. Liwahi tena kutoa kauli tata huko nyuma, na badala ya kukemewa, huwa wanapewa vyeo.

Yuko mwingine kanda ya ziwa ambaye haoni shida kutamka hadharani kuhusu kupoteza watu kwa namna yoyote ile. Wapo wengine wengi. Ifike mahali vijana na watu hawa wakemewe vyema na mamlaka zitakazoluwepo (sio ccm) kwa lengo la kuondoa taharuki na chuki dhidi yao na serikali na chama chao.

4. Kuhusu polisi. Hawa ni donda ndugu. Polisi wametengenezwa kuwa maka maroboti. Kama mbwa. Wanatumwa kuuma na kudhuru bila kufikiri. Wanajisahau kuwa nao ni raia. Nao wana damu ka waliowaua. Wana ndugu zao mitaani. Kinachowaumiza asjkari ni ORDER/AMRI. Hizi amri huwa hazitakiwi kupingwa. Sasa ili kuleta muafaka, hizi amri nazo zihojiwe. Zipingwe. Kama amri ilikuwa ni %95 ya sehemu ya utendaji, basi sasa iwe %50. 50 amri, na 50 mantiki. Polisi akitumwa kudhuru awe na uwezo wa kufanya maamuzi na hatimaye kutakaa amri dhalimu na sheria imlinde dhidi ya wakubwa wake wanaotoa amri hizo dhalimu.

Tunasikia kabla ya matukio, polisi (hasa FFU) hupewa nangi na pombe ili kuwavuruga akili zao waweze kuonyesha ukatili wa kutosha kwenye operesheni zao. Hili lipo wazi maana haya Hayati Magufuli aliwahi kulizungumzia hilo - kuwapa polisi "cha Arusha" kabla ya operesheni. Polisi wakifikia hatua ya kukataa kutumika, jamii itakuwa na amani.

Tuendelee kuwaombea wale wote waliipoteza uhai ili wapate pumziko la amani milele. Ni imani yetu kuwa pakiwepo na haja ya jamii kutaka kufanya maandamano siku zijao, vyombo vya dola vijitafakari sana katika kutoa amri kandamizi zitakazopelekea uvunjifu wa amani na upotevu wa mali na maisha
Ungelisoma kesi za Nurenburg Ujerumani baada ya vita vikuu vya pili vya dunia ungeelewa kuwa kutenda jinai katika harakati za kutekeleza jukumu la kisheria hakumpatii kinga mvunja sheria kwa kisingizio cha kupokea amri kutoka juu.

Hao wote unasema walitumwa kuua na unadhani hawana hatia kwa sababu waliamrishwa, unakosea, wote hao wanafungwa kwa sheria hizi hizi zilizopo.

Wakiburuzwa mahakamani, hakuna atakayekwepa mkono wa sheria kwa utetezi wa kutumwa.

Hakuna amri halali inayovunja sheria ikatolewa kwa mdomo na baadaye mtekelezaji akaweza kuepuka adhabu!

Kiongozi hawezi kutoa amri ya mdomo inayokwenda kuvunja sheria bila ya kutoa maandishi na amri hiyo ikawa halali.

Hata kungelikuwa na maandishi, bado mtoa amri na mtekelezaji, sheria inawabana kutekeleza majukumu yao kwa kuvunja sheria

Ninachotaka kukwambia hapa ni kwamba, hata sasa, hao wote waliopanga na kutekeleza mauaji kinyume cha sheria, watakapofikishwa kortini, utaona namna watakavyoanza kukataana!

Utetezi wa 'nilitumwa' kutekeleza amri haramu huwa hauna mashiko, adhabu na hatia humpata aliyetekeleza.

Labda jambo hili lifumbiwe macho tu, lakini wakitaka kuwawajibisha wale wote waliotenda jinai hiyo ni rahisi sana 'kumalizana' nao.
 
Asante kwa tathmini yako njema. Kadhalika sikusema kuwa kwa kutekeleza amri.za wakubwa wao, wanapewa kinga kisheria, hapana. Kikubwa ni kwamba nao waone mantiki katika kutekeleza amri.wanazopewa. wasiwe kama roboti, maana watakumbana na sheria lakini pia watakumbana na hasira ya wananchi/raia
 
Acha ujinga Wewe na samia wako, Samia alivyoshika madaraka alisema anafungua nchi wakina lissu na lema walirejeshwa nchini tena kwa kulipiwa nauli na posho,ili Magufuli haonekane hakufaa, mpaka kaja na 4r, Sasahivi hapo Magufuli anausikaje! wakati mambo yake yote mliyaondoa.Bebeni msalaba wenu wenyewe Magufuli hausiki na haya.
Alikuja na 4R ili nani atekeleze?
 
Back
Top Bottom