Malumbano ya familia ya Shelukindo na Mh Januari Makamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malumbano ya familia ya Shelukindo na Mh Januari Makamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 23, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145


  [​IMG]

  TAARIFA YA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA FAMILIA YA WILLIAM SHELUKINDO KUHUSU UBUNGE JIMBO LA BUMBULI MKOANI TANGA

  Kumezuka taarifa za uhakika kwamba tangu Mhe. Januari Makamba ashinde Ubonge katika Jimbo la Bumbuli hajawahi kukutana hata siku mmoja na mbunge wa zamani wa jimbo hilo Mzee William Shelukindo.

  Katika hutuba yake alioitoa mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kura za maoni katika Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Januari Makamba ailisema ataendelea kumuheshimu kama Mzee Shelukindo kama kiongozi wa muda mrefu kwenye Serikali.

  Mheshimiwa Makamba aliendelea kusema Mzee Shelukindo ni hazina kubwa na uzoefu na busara zake bado zinahitajika katika jimbo la Bumbuli na kuahidi kuomba ushauri wake pindi atakapohitaji kufanya hivyo, wakati akiwatumikia wananchi wa Bumbuli kama mbunge wao.


  Lakini kutokutana kwa viongozi hawa kutokutana tangu mheshimiwa Makamba achukue kumesababisha minong'ono na kuleta wasi wasi mkubwa kwa baadhi ya wanasiasa na wananchi wa Bumbuli.


  Kumekuwa na upotoshwaji wa habari kwamba Mzee Shelukindo anawatayarisha watoto wake ili waweze kushindana na Mhe. Makamba katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.


  Sisi kama watoto Mzee Shelukindo na tunawashutumu vikali baadhi ya wanasiasa wa Bumbuli ambao wamekuwa wakichochea maneno ili kuleta ugomvi na malumbano yasiokuwa ya msingi kati ya familia hizo mbili za Shelukindo na Makamba.


  Watoto wa Mzee William Shelukindo, Bw. Samuel Shelukindo na Baraka Shelukindo wanawaasa wanasiasa wa Bumbuli kuacha uchochezi na kutotoa taarifa potufu na badala yake kumsaidia Mhe.Makamba ili kushughulikia changamoto zinazolikabili jimbo la Bumbuli.


  Tunasema bado tuna mahusiano mazuri sana na Mhe. Makamba na tunamheshimu kama Mbunge wetu na hawatakubali kuona uhusiano huo unavurugwa na watu wachache wenye maslahi yao binafsi.


  Sisi kama familia ya Shelukindo tunasema kwamba hakuna ndugu wala mtoto yoyote kutoka kwenye familia yetu mwenye nia ya kuingia kwenye siasa ili kupambana na Mhe. Makamba mwaka 2015.


  Kama familia tupo kwenye mikakati ya kuwakutanisha Mhe. Makamba na Mzee Shelukindo ili kufuta fitna zilienezwa na kumuezesha Mhe. Makamba kuendelea kufanya kazi yake ya ubunge bila wasi wasi wowote kwa manufaa ya watu wote wa Bumbuli.

  Asanteni
  Bw. Samuel Shelukindo na Bw. Baraka Shelukindo
  Cont:0784888765- Baraka Shelukindo


   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  haipunguzi wa haiongezi matatizo ya wana bumbuli......


  Badala watu kuishi kwa kuzusha maneno kuwa hawakutani n.k bora wangeshiriki kwenye maendeleo ya bumbuli

  afterall hawa wote si ni wanachama wa ccm? Ina maana hawakuwa wakikutana hata kwenye vikao vya chama? Au watu wanataka mpaka wapige picha wanapata lunch ndo waridhike?
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kumbe shelukindo ana mitoto?asante nimejua kupiti jf,
   
 4. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Nikilisikia hilo jina shelukindo napata hasira si yule aliyekuwa mwenyekiti wa body kiwanda cha matairi arusha KIWANDA KILIPO KUFA TU NAYE AKAKOSA UBUNGE
   
 5. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Mimi simtetei January lakini nawajua vizuri sana wakina Baraka. Hawana la maana wanataka heshima na vilevile wanataka January a kiss-up kwao. Familia yao haileta lolote Lushoto hatuna maji kule Lushoto, barabara imeishia mjini, watu wamekaa kaa tu bila kazi, shule na hospitali zote ni za kanisa tu na leo wanataka heshima. Mtu pekee atayetakiwa kupewa heshima ni kama Msuya alivyofanya Same!. Huyu mzee alikuwa anafanya vitu kwa manufaa yake tu. Mfano Mzuri Moshi kule marangu kuna lami hadi vijijini kabisa tena nzuri ni kwasababu wamebadilisha sehemu imekuwa ya kitalii!! sasa Lushoto pamoja na kuwa sehemu ya kitalii na watu wanaenda kupumzika na kupanda milima huyu mzee hakuweza kuwaelewesha serikali kwamba barabara itasaidia kwenye pato la taifa. Hakuna hata umeme!!. Baraka na Samweli nyamazeni hamna lipya
   
 6. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kamundu: Mzee Shelukindo alijitahidi kuwaletea wawekezaji. Sasa hivi wapo akina Mkapa & Co wamejenga mahekalu Lushoto na wanafika kila mara kumpumzika.

  Hivi nyinyi watu wa Lushoto hamuwezi kufikiri OUT OF THE BOX?! Yaani ubunge Lushoto lazima uwe UKOO wa Makamba au Shelukindo tu. Acheni Siasa hizo za Ufalme vinginevyo CDM watachukuwa JIMBO hilo 2015.
   
 7. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mngekaa kimya tu mngekufa hamna lolote mnataka ubunge nyie tunawajua sana watoto wa magamba wote mnapitia migongo ya baba zenu
   
 8. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2012
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  duh kwanza siamini kama hii barua imetoka kwa watoto wa Mzee shelukindo, its too simple, nahisi inatoka kwa Makamba mwenyewe, tunamjua jinsi anavyojijenga kupitia vyombo vya habari baadala ya kutumikia watu waliomchagua.
  ningetegemea Makamba ndio angefanya effort kukutana na mzee shelukindo kwasababu kadhaa, kwanza ni zaidi ya mzee wake kiumri, na wakati wa kampeni alimtukana na kumkashifu sana mzee shelukindo na alimvunjia sana heshima...na nimkiongozi anayemfuata kumnyang'anya kiti.
  ubunge wa January Makamba si wa harari kila mtu anajua, ni baba yake ndio aliyelazimisha na kunishinikiza kijana wake achaguliwe kwa nguvu, viongozi wote wa chama wilaya ya lushoto wanajua hili na wale wa jimboni, hata baada ya uchaguzi baadhi ya wagombea waliopeleka malalamiko kwenye kamati kuu walikuwa na hoja za nguvu, na hata kwenye kikao cha kamati kuu ilipofika kwenye suala la January, Mzee makamba alibanwa sana haswa na mzee Msekwa, kwakua alikuwa amefanya maamuzi bila kupitishwa na kamati, alipeleka kadi za chama zaidi ya 15,000 bila utaratibu wa chama kufuatwa jimboni, lakini baada ya kujua kwamba ni mwanachama pekee aliyeandikishwa ndiye atakayepiga kura, aliamua kubadilisha utaritibu na kusema yoyote mwenye kadi apige kura, na ndio hapo badala ya wapiga kura waliojiandika jimboni bumbuli 9,800, matokeo yalipotangazwa waliopiga kura walikuwa 18,000 na zaidi, maswali yote haya mzee makamba alishindwa kujibu na badala yake aliomba tu asamehe maana angeadhirika kama kijana wake akitupwa, lingine ni kwamba kabla uchaguzi karatasi za kura zilishaonekana na matangazo yalifanyika usiku kucha kuwaambia watu wachagua namba 4 ambayo ndio jina la januari, si hilo tu pia, aliyekuwepo katika wa ccm wilaya katika vikao vilivyopita alikuwa afukuzwe kazi ndani ya chama lakini badala yake mzee makamba alimpeleka wilaya ya lushoto na yeye ndiye aliyesimamia kuhakikisha ushindi wa January....
  lakini yote hayo si kitu....Chama kinajua kama January ni mtoto wa kufikia wa Mzee Makamba, japo hili linapingwa sana, lakini ni kweli kabisa....
  toka January amepata ubunge mpaka sasa hakuna aliliofanya jimboni na amefika jimboni si zaidi ya mara 4, hapokei simu za wananchi,viongozi wa chama na mara nyingi amekuwa akidanganya yuko nje ya nchi. Mpaka sasa Januari anafikia Hotelini akienda jimboni hana nyumba wala mji zaid ya kijijini kwa mzee wake ambako ni mbali na makao makuu ya jimbo, aliwaahidi wananchi baada ya miezi site atakuwa ametimiza ahadi zake lakini alikaa mwaka mzima bila kufika wala kukutana na wananchi wa jimbo lake.
  Amegombana na waliokuwa wapambe wake waliomsaidia kupata ubunge, wengi wanamdai kwakuwa aliwaomba wamsaidie akiahidi kama angekuwa waziri na wao angewasaidia kwenye biashara zao, wengi walimuamini na kujitoa,lakni baada ya kupata mpaka leo hana mawasiliano nao, Mzee makamba anajua hili na wengi wameenda kumuona mzee wake na wakati mwingine akiwaomba watu wamvumilie na pia hata kutoa yeye pesa zake kuwalipa, mara kadhaa wanabumbuli wamekuwa wakimfuata mbunge wao mjini na yeye kutowapokea wala kuwasaidia na hata kutopokea simu zao, mara kadhaa wananchi wamejikuta wakienda kwa Mzee makamba kushtaki, wakati mmoja mzee makamba alilazimika kumuita january usiku na kumdanganya ana wazee anataka kuonana nao, alipofika alikuta wanajimbo na ndipo alipowapa nauli warudi nyumbani na kuwa yeye ni mbunge wa wote si wao tu....
  Januari amekuwa mbali sana na wananchi na hata viongozi wa jimbo na hata baadhi ya viongozi wamekuwa wakimlalamikia kuwa anawadharau...
  kwa sasa hakuna wanajimbo wanaomuona kuwa anafaa na wengi wanajuta kumchagua, na mipango ya 2015 kumtoa imeanza mapema sana, hata ikiwezekana kumpa chama pinzani, 2010 alifanikiwa kuwanunua wagombea wote wa upinzani lakini safari ijayo itakuwa tofauti......

  tunachomshauri January, badala ya kufikiria hta uraisi wa nchi ajiulize kwanza amelifanyia nini jimbo na watu waliomchagua, ni dharau sana yeye kushinda UBUNGE na kumtuma mama yake na mke wake kwenda kuwashukuru wananchi kwakuwa eye yuko busy, wananchi hawakukuchagua kwa kuwa wanashida na vitenge na khanga kutoka kwa mama yako na mke wako....kuwa karibu na wanachi na uwatumikie kama ulivyowaahidi.
   
 9. Lenana

  Lenana JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 422
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Gutter politics as usual!
   
 10. Lenana

  Lenana JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 422
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Ni kwamba lugha ya kiswahili yawapiga chenga wana wa shulukindo au!? Am doubting the source of information and whether the content of the same are genuine and from the purpoted source!?
   
 11. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 2,897
  Trophy Points: 280
  Sasa taarifa itoke kwa watoto wa Shelukindo, lakini picha iwe ya mzee Makamba, mbona inachanganya? Halafu kama nia ni kukanusha uhusiano mbaya wa familia hizo, iwaje waweke hadharani hapa kwamba Januari hajawahi kwenda kumtembelea Shelukindo?
   
 12. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mbona sijaona watoto wa Lau Masha wakimlalamikia Wenje? Hawamjui sababu Wenje alikuwa anakaa Milimani kwa Washashi Mwanza; na watoto wa Lau wanasoma South Africa kwa Maraha

  Sasa Hao watoto wa Makamba wamesoma nje hao watoto wa Shelukindo wamesoma nje... neema kwao watulizane
   
 13. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  Mar 24, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,814
  Likes Received: 5,132
  Trophy Points: 280
  ..Yaani wanataka Mzee Shelukindo na January wakae wajadili "mgogoro" ktk familia zao??

  ..huku ni kumvunjia heshima Mzee William Shelukindo.
   
 15. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2012
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  sijaelewa mleta maada alikusudia tujadili nin hasa katika mada yake. Maudhui ya habari hayajakaa sawa kabisa
   
 16. c

  chuwaalbert JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 3,070
  Likes Received: 1,450
  Trophy Points: 280
  "Sisi kama familia ya Shelukindo tunasema kwamba hakuna ndugu wala mtoto yoyote kutoka kwenye familia yetu mwenye nia ya kuingia kwenye siasa ili kupambana na Mhe. Makamba mwaka 2015".

  Kuna ukweli gani hapa? Humu jamvini ulishawahi letwa uzi unaompigia chapuo Baraka kwa ajili ya Ubunge 2015! Sasa hapo penye red ni aje wakuu?
   
 17. Mkomamanga

  Mkomamanga JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 818
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Pelekeni kipindi cha 'family matters'
   
 18. Mkomamanga

  Mkomamanga JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 818
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Kwani Januari mwenyewe mbona ni 'mzanaki' katika familia ya Makamba? Kwani ni msambaa huyo? Si lazima kuwa msambaa ndiyo uwe mbunge wa usambaani lakini ni muhimu kuwa na mwakilishi wa watu!!!! Tokeni ndani ya box mtendee haki watu wa Lushoto (Bumbuli), Makamba Senior amekuwa kwenye siasa muda mrefu (Niwakumbushe tu kuwa mkuu wa mkoa ni sawa na kuwa waziri) sasa alifanya nini? Hata Januari atawaacha solemba. Wala msilalamike eti hawakutani na Shelukindo, mbona alisema kuwa yeye ataendesha jimbo kwa 'electronic gadget'? Maana alisisitiza kuwa atakuwa na website na mtandao wa kupata maoni yenu, sasa mwamtafuta wa nini. Kama hamtaki kuwakilishwa kwa njia ya kielektroniki basi fanyeni uamzi 2015 kumpata wa papo hapo.
   
 19. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #19
  Mar 27, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  hatunahaja ya kujua mahusiano yao ukishashindwa ubunge jipange upya au kagombee kuchukua nafasi aliyoanguka Baba
   
 20. SINA JINA1

  SINA JINA1 JF-Expert Member

  #20
  Mar 27, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli Jf nizaidi ya social netiweki...

  source;
  Mwakalinga
   
Loading...