Malumbano ndani ya basi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malumbano ndani ya basi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Tuko, Sep 13, 2010.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Sep 13, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Hivi majuzi nilikuwa katika safari ya kuelekea katika vijjiji fulani, kukatokea malumbano ambayo yalinisisimua sana. Basi lilikuwa limejaa sana, konda 'anapanga' abiria. Abiria hawakufurahi lakini hakukuwa na option kwani hakukuwa na basi jingine linaloenda huko na barabara ni mbovu. Ndani ya basi alikuwepo bibi ambaye naye alikuwa analalamika kuwa anabanwa sana na anaumia. Kijana mmoja akamwambia yule bibi 'bibi usilalamike, shida yote hii inaletwa na nyie wazee mnaomchagua Kikwete' Kwa kweli yule bibi alikuwa mkali ajabu, analalamika 'kwa nini nilaumiwe mim... mbona nyie vijana hampigi kura mkamchagua huyo Lipumba (Inaonekana bibi alikuwa namfaham tu Kikwete na Lipumba). Bibi aliendelea kulalamika kwa muda mrefu kuwa kwanza kule kwenye gari walikuwepo wazee wawili tu, na vijana wengi... 'sasa kama nyie mnaona sisi wazee tunamchagua Kikwete, kwa nini nyie ambao ni wengi hampigi kura mkamchagua Lipumba au hiyo CHADEMA' aliendelea kulalama bibi huyo huku akishangiliwa na abiria wengi...

  Msg niliyopata ni kuwa vijana hatupigi kura, na hata wazee wetu wanalijua hilo.

  Vijana tubadilike mwaka huu (ingawa najua kwa bahati mbaya wengi hatujajiandikisha)..
   
 2. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #2
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,127
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa Tuko vijana wengi hawajajiandikisha au hawataki kupiga kura lakini ndio wanaoongoza kulalamika.
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nadhani sababu ingine kuu ni kwamba CCM wanaiba sana kura.
   
 4. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Na pia wananunua sana shahada za kupigia kura,bila kusahau kuwa hata marehemu nao huwa wanaonekana wamewapigia kura
   
 5. b

  bobishimkali Member

  #5
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unadhani ushindi wa KIKWETE wa 2005 ulitokana na kura za wazee? Hapa sikubaliani na wewe kwa sababu vijana walio wengi ambao walishiriki katika uchaguzi walimpa kura KIKWETE hususan vijana wasomi wa vyuo vikuu .Nakumbuka siku moja JK alitembelea chuo kikuu cha mlimani kabla hajatangaza nia ya kugombea 2005,ambapo vijana wengi walimfuata na kumtaka awanie nafasi ya urais. Napenda nikueleze kwamba vijana wengi bado wana imani na kikwete na watampa kura zao katika uchaguzi 2010. Hivyo, ushindi wa kikwete katika uchaguzi ujao hautatokana na kura za wazee tu bali pia kura za vijana
   
 6. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #6
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Natumai hata mwaka huu wanafunzi wa vyuo vikuu watapiga kura kumchagua Kikwete wakiwa majumbani mwao huku wakiwa walijiandikisha katika vituo vya sehemu wanaposoma na wakati huo vyuo vitakuwa havijafungiliwa wakati wa uchaguzi
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Pumba!
   
 8. MAWANI

  MAWANI Member

  #8
  Sep 13, 2010
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Walikuwa wanamwamini na sasa wameona pumba zake. Subili Oct 31, 2010. Hata mimi ni k=ijana nilimpa lakini nimeona ni careless kiasi gani". By the way, hata wazee nao wameanza kujua kuwa JK hafai. wajukuu zao wanakufa sababu ya kukosa dawa n.k!!!!!!!
   
Loading...