Malumbano la hoja: Mchangiaji ashangaa jiji la Dar kuvunjwa kwa kisingizio cha kubana matumizi , ashangaa Chanika kuwa jiji magomeni kuwa nje ya jiji

Watanzania tu wagumu sana kuelewa...yani ni mwezi sasa unakwenda bado jambo hilo watu hawajaelewa....hahahah eti jiji limevunjwa! Kwani hilo jiji wanaosema limevunjwa lilikuwa linaanzia wapi na kuishia wapi? Hahahaha yani hili swala la jiji ndio linashihirisha uwezo wetu wakuelewa mambo!

Yani hadi huyo mchungaji anajua jiji limevunjwa hahahahaha! Yani watu hadi leo wameshindwa kujua kilichovunjwa!
Angalia hata taarifa za serikali
1. Jiji la ilala
2. Manispaa ya kinondoni
3. Manispaa ya temeke
4. Manispaa ya ubungo
5. Manispaa ya kigamboni
Kwahiyo jiji ni ilala tu.
Wewe umeelewaje labda?
 
Akizungumza kwa kujiamini mmoja wa wachangiaji amepinga kuvunjwa kwa jiji kulikoleta mkanganyiko wa hadhi ya maeneo , kwa kutolea mfano wa Chanika kuwa jijini huku Magomeni , Kinondoni , Masaki , Temeke , Mwenge na Mbezi Beach kuwa nje ya jiji .

Ametoa plan ambayo kama ingefanyiwa kazi basi mkanganyiko huo usingekuwepo na bado matumizi yangeendelea kubanwa , amedai kwamba kama lengo lilikuwa ni kubana matumizi ilikuwa rahisi tu kubadili muundo wa Jiji ambapo amependekeza vikao vya jiji vingekuwa vya mameya wa manispaa zake kwa lengo la kujadili palikofikiwa kwenye mipango ya manispaa hizo , bado jiji lingeendelea kuwepo bila kuipromote Buguruni kwa Mnyamani na kuitupa Oysterbay .

Mwisho mchangiaji huyo amekiri kufahamu mamlaka ya Rais na amesema hapingi mipango yake
Bado kidogo mtasikia wilaya mipya ya katoro.
 
Watanzania tu wagumu sana kuelewa...yani ni mwezi sasa unakwenda bado jambo hilo watu hawajaelewa....hahahah eti jiji limevunjwa! Kwani hilo jiji wanaosema limevunjwa lilikuwa linaanzia wapi na kuishia wapi? Hahahaha yani hili swala la jiji ndio linashihirisha uwezo wetu wakuelewa mambo!

Yani hadi huyo mchungaji anajua jiji limevunjwa hahahahaha! Yani watu hadi leo wameshindwa kujua kilichovunjwa!
Ukisema jiji la ilala tayari umeshaitoa Oysterbay, Masaki, mikocheni, mbezi beach, kijitonyama e.t.c
 
Kuondoa halmashauri ya jiji kwa sababu ina-overlap halmashauri za manispaa ni jambo la maana. Overlap hiyo ilitengeneza redundancy, hivyo cost ilikuwa kubwa wakati hakuna ulazima wa halmashauri hiyo iliyokuwa kama blanket.

Tatizo ni vile walivyoamua kipande kile pekee cha halmashauri ya ilala ndo kiwe chini ya halmashauri ya jiji. Wangefanya extension ya eneo la halmashauri ya Ilala, au ikiwezekana kugawa Dar Es Salaam upya ili ku-condolidate maeneo yote ya hadhi ya jiji itengenezeke yawe chini ya halmashauri ya jiji, na maeneo yaliyobaki yafanywe halmashauri ya hadhi za kimanispaa.
 
Back
Top Bottom