Malumbano juu ya shule nzuri

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205


Je, uliwahi kusikia watu (wazazi na hata mara nyingine wanafunzi) wakiwa na majadiliano na hata wakati mwingine mabishano makubwa kuhusu kuwa shule fulani ni nzuri kuliko shule fulani?

Au ukiwa mzazi (au mzazi mtarajiwa) umewahi kujikuta ukihitaji kuchagua shule nzuri ya kupeleka mtoto wako?

Binafsi nimeyasikia sana na hata mwenyewe nimejikuta nikihitaji kuchagua shule.

Maoni yangu ni kuwa suala hili lina zaidi ya jinsi watu wanavyolichukulia.

Mfano ukiwauliza watu wawili : Je, kati ya shule A na shule B ni ipi nzuri zaidi?

Mara nyingi hili huonekana kuwa swali jepesi na mara moja kila mmoja atakupa anayofikiri ni bora kuliko nyingine, je hii ni sawa?

Kama siyo kuna upungufu gani hapa?

Nawakaribisha wanajf tujadili hili kama mmenipata.
 
Shule nzuri ni kichwa chako plus other maujanja kama kilaza hata ukienda shule gani utabaki kuwa kilaza.
 
Shule nzuri ni kichwa chako plus other maujanja kama kilaza hata ukienda shule gani utabaki kuwa kilaza.

Nakubali mkuu kichwa chako kina nafasi muhimu sana katika mafanikio ya kielimu lakini bado nafikiri yapo tunayoweza jadili kuhusu hoja ya shule kuitwa nzuri.. tuwasikie wengine wana maoni gani
 
Back
Top Bottom