Malkia Elizabeth I (7 Septemba 1533 - 24 Machi 1603) wa Uingereza

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,274
6,592
Elizabeth I wa Uingereza
16640574_583697331815673_7254100268370385756_n.jpg


Malkia Elizabeth mnamo 1585
Elizabeth I wa Uingereza (7 Septemba 1533 - 24 Machi 1603) alikuwa malkia wa Uingereza kuanzia 1558 hadi 1603. Alikuwa mwanamke wa tatu aliyetawala Uingereza kama malkia

Wakati wake ulikuwa kipindi cha kustawi kwa utamaduni na uchumi katika Uingereza ambako William Shakespeare alitunga maigizo na tamthiliya zake, Francis Bacon aliandika falsafa yake na Francis Drake aliweka misingi ya upanuzi wa kikoloni wa Uingereza duniani. Elizabeth alihakikisha pia kipaumbele cha Kanisa Anglikana kama dini rasmi ya taifa.

Alliitwa mara nyingi "malkia bikira" kwa sababu hajaoa wala kuzaa watoto. Kutokana na neno la Kiingereza kwa bikira "virgin" koloni ya kwanza ya Uingereza ikaitwa "Virginia"

Alizaliwa katika nasaba ya Tudor kama mtoto wa mfalme Henry VIII wa Uingereza na mke wake wa pili Anne Boleyn. Hakumjua mamake aliyeuawa akiwa mdogo wa miaka mitatu. Alipata elimu nzuri alijua lugha sita za Kiingereza, Kifaransa, Kiitalia, Kihispania, Kigiriki na Kilatini.

Kwa miaka mingi hali ya cheo chake ilikuwa mashakani. Babake Henry VIII hakumtaka kama mrithi baada ya kumchukia mamake aliyemwua. Lakini mke wa mwisho wa Henry VIII alimshawishi mfalme kuwaingiza mabinti zake katika orodha la ufuatano wa warithi wa cheo chake lililothebitishwa na bunge.

Elizabeth alikuwa malkia baada ya kifo cha dada yake Maria Tudor. Mwenyewe alilelewa kama Mkristo wa Kiprotestanti akahakikisha ya kwamba ibada za kikatoliki zilikomeshwa zilizopewa nafasi kubwa na dadake aliyekuwa mkatoliki. Kwa kusudi hii alitangaza sheria kuwa ibada zote zilipaswa kufuata liturgia ya Common Book of Prayer na kumfanya mfalme au malkia kuwa gavana mkuu wa kanisa la Uingereza. Hatua hii hatimaye ilitenganisha kanisa Anglikana na usimamizi wa Papa wa Roma.

Alimaliza vita dhidi ya Ufaransa iliyowahi kudhoofisha nguvu za taifa kwa miaka mingi.

Mwaka 1568 malkia wa Uskoti Mary Stuart alikimbilia Uingereza kwa sababu alikuwa hatarini ya kuuawa kwake nyumbani aliomba msaada wa Elizabeth. Mary Stuart alionekana kama hatari kwa utawala wa Elizabeth kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa na haki za kushika taji la Uingereza. Elizabeth aliamua kumkamata na kumfunga akiendesha utafiti juu ya mashtaki dhidi yake. Mary Stuart alikaa mafungoni kwa kipindi cha miaka 18 mwishowe alishtakiwa kutokana na kushiriki katika mipango ya kumwua Elizabeth akapewa hukumuy a mauti na kuuawa 1587.

Elizabeth alikuwa amepanusha uwezo wa Uingereza baharini akishirikiana na Francis Drake na Walter Raleigh. Drake alizunguka dunia yote kama mtu wa pili baada ya Ferdinand Magellan. Baadaye alipewa kibali cha malkia cha kunedesha vita ya baharini dhidi ya meli za Hispania iliyokuwa taifa kubwa ya Wakatoliki. Drake na wenzake walishambulia mara kwa mara meli za Wahispania zilizobeba fedha kutoa koloni za Amerika na kiasi kikubwa cha fesha hii ilifika kwenye mifuko ya kifalme ya London.

Baada ya kuuawa kwa malkia mkatoliki Mary Stuart mfalme Philip wa Hispania aliamua kushambulia Uingereza. Alitengeneza kundi kubwa la jahazi manowari lililowahi kupatikana hadi wakati ule. Lakini wanamaji Waingereza waliweza kuwazuia wasipeleke askari zao kwa nchi kavu. Dhoruba iliharibu baadaye meli nyingi za Wahispania. Ushindi huu ulikuwa msingi wa nafasi kubwa ya Uingereza baharini iliyoendelea kuwepo hadi karne ya 20.

Hali ya vita na Hispania iliendelea. Kuanzia 1593 Waeire waliokuwa Wakatoliki vilevile walianza kuasi dhidi ya utawala wa Kiingereza na vita hii ilihitaji nguvu zote za ufalme; asakri wengi walikufa na malkia alipaswa kuongeza mzigo wa kodi kwa raia wa ufalme. Wengi walisikitika vita hii. Gharama kubwa za vita ya Ueire zilimlazimisha malkia kuomba mara kadhaa kibali cha bunge luongeza kodi. Kwa njia hii nafasi ya bunge la Uingereza likaongezeka nguvu.

Elizabeth aliaga dunia mwaka 1603 akiwa na umri wa miaka 69.
 
kama sinema vile,asante kwa kutuhabarisha,kimsingi hii ni shule yenyewe
 
Ukianza na story ya princes in the tower utagundua baba yake Elizabeth I aliiba throne kutoka kwa familia nyingine. Na baba yake alitamani sana mwana wa kiume ikabidi afarakane na mkewe wa kwanza na Papa ili aoe tena, Henry alikuwa mtata na mwenye hila sana.. The only honor ya Elizabeth ni ushindi wake dhidi ya Spanish Armada that her major credit.. wanaojua historia yake vyema inasemekana Elizabeth I alikuwa hapendi kuoga mara kwa mara na alikuwa ameoza meno! na kwa kuwa hakukuwepo na camera wakati ule, alikuwa makini sana na watu waliokuwa na kandarasi ya kumchora!
 
Back
Top Bottom