Malipo ya Upimaji Viwanja ni Halali au Rushwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malipo ya Upimaji Viwanja ni Halali au Rushwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mrimi, Oct 4, 2011.

 1. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  WanaJF naombeni kujuzwa uhalali wa kulipia upimaji kiwanja cha kujenga nyumba ya kuishi.
  Nimeona niweke hili jambo hapa kama kero inayoonekana kusahaulika,au basi imekuwa desturi.

  Kuna mantiki gani kulipa kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kupima kiwanja kilichopo umbali wa mita
  200 tu kutoka ofisi ya ardhi. Na mtu akishajenga nyumba analazimika kulipia kodi ya jengo,lkn pia
  haya malipo maana yake nini? Kwani wale wapimaji hawana mishahara,au ndio kusema
  hakuna bajeti kwa ajili ya shughuli hii? Na ni kwa nini hakuna flat rate,maana huduma hii hutozwa kufuatana
  na utashi wa mtu utakayemkuta ofisini.Je,tuseme polisi akienda kukamata mhalifu alipwe na mhalifu huyo?

  Tujadili.
   
 2. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Jiulize maswali haya:

  1. Kwa nini ukitaka kuunganishiwa maji ni lazima ulipie?
  2. Kwa nini ukitaka kuunganishiwa umeme ni lazima ulipie?
  3. Kwa nini ukitaka kusajiri gari na kuomba leseni ni lazima ulipie?
  4. Kwa nini ukitaka kupeleka mtoto shule ni lazima ulipie form ya maombi?
  5. Kwa nini ukitaka kusoma shule ni lazima ulipe karo?
  6. Kwa nini ukitaka kusafir kwenye dalalada/Tax ni lazima ulipe nauli
  7. Kwa nini ukienda Hospitali ni lazima ulipie matibabu?
  8. nk. nk.

  Sasa kwa nini kulipia huduma ya kupimiwa kiwanja inakuwa tabu au unaona ni tatizo?
   
Loading...