Malipo katika ajira mpya za walimu 2017, naomba kufahamishwa haya

Abuwhythum

JF-Expert Member
Jan 7, 2015
837
495
Kwa kuwa serikali imewataka walimu wapya kuwasili katika vituo vyao vya kazi walivyopangiwa kuanzia tarehe 18 mwezi huu!

1. Vipi malipo ya kufanya kazi kwa muda huu wa siku 13 za mwezi wa nne (April) yatakuwaje?

2. Huwa yanatolewa maelezo ya kurudishiwa nauli zitakazo tumika kuwasili vituoni. Kwa mwaka huu mbona maelezo hayo hayajatolewa?

3. Walimu waliomaliza masomo yao nyuma ya mwaka 2015 na kuombea kutuma maombi ya kazi , ajira zao zitatoka ndani ya mwaka huu wa fedha? Au itakuwa mwaka ujao wa fedha?

4. Mafundi sanifu wa maabara ajira zao mbona hazijatolewa ufafanuzi wowote!?

5. Kuna utaratibu gani wa mtu kuweza kubadilishiwa kituo cha kazi kabla ya kuripoti katika kituo alichopangiwa?
 
Mkuu sasa hiv serkali haiajiri kwa kuangalia mwaka uliomaliza
Inaajiri kwa kuangalia mahitaji yanayotakikana kwa wakat husika

Hii ni kwa mujibu wa wazir kairuki
Kama suala ni hilo! Kuna upungufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati zaidi ya 26,000 kwa nini Serikali haitoi ajira kwa wahitimu wa Sayansi na Hisabati kwa mwaka 2016
 
Andika barua wizara ya ajira na kazi uwajulishe kuhusu hilo watakujibu

Hiyo wizara mbona haihusiki na ajira za walimu!
Maana katika suala la ajira za walimu huwa zinasikika wizara tatu.
1. Wizara ya Elimu
2. Wizara ya Utumishi na
3. TAMISEMI
 
Maswali haya utapatia majibu mazuri utakapokwenda kuripoti huko na c kutumia mitandao ya jamii huwezi kupata majibu sahihi nenda ulikopangiwa
 
Maswali haya utapatia majibu mazuri utakapokwenda kuripoti huko na c kutumia mitandao ya jamii huwezi kupata majibu sahihi nenda ulikopangiwa
Mtu akisharipoti ndo amejipiga password! Kubadilisha kituo kunakuwa na utata ikilinganishwa na mtu ambaye hajaripoti.

Hapa kwenye mitandao ya kijamii wapo watu wengi wazoefu wa mambo hayo! Hata hao maofisa husika wamo humu kwenye mitandao. Hivyo wakiamua wanaweza kutoa msaada hapahapa.
 
Nauli unarudishiwa ila uwe na rist za gharama,

Utapewa hela kujikimu ukiwa bado hujaanza kupokea mshahara japo hutolewa kwa siku 7 tu, mfano 70,000×7=490,000/- hicho ndo chanzo cha maisha yako ktk utumishi,

Kubadilisha kituo b4 kuriport nenda wizarani, ukiriport kuhama mpaka umalize miaka 2 ktk kituo husika,

By the way nenda kapge kaz ila kuwa na adabu ya matumiz ya fedha maana mambo si shwari nafkr jibu unalo mkuu!
 
Haya yanaweza kuwa majibu ya Maswali yako (Siyo rasmi, ni kutokana tu na uelewa wangu).

1. Malipo yatafanyika kwa utaratibu uliopangwa. Wao pia walishafikiria hilo, kwa hiyo ondoa hofu.

2. Nauli pamoja na fedha za kujikimu (Per diem) hutolewa ilimradi tu uwe na tiketi. Wamesisitiza tena kuwa wale wote watakaoripoti na kuchukua fedha za kujikimu kisha kuondoka, watushughulikiwa ipasavyo.

3. Kwa vyovyote inavyoonekana, wao watafikiriwa katika mwaka ujao wa bajeti 2017/2018.

4. Siyo wao tu ndo ambao hawajatolewa ufafanuzi. Kuna watu wengi wa field nyingi za ajira hawajapata ufafanuzi juu ya swala la ajira kutoka Serikalini. Hivyo wakae watulie mpaka wakati watakapokumbukwa.

5. Ukisoma TANGAZO la kazi lililotolewa, linabainisha kuwa hakutakuwa na ubadilishaji wa vituo. Hivyo kila mtu aripoti katika kituo chake cha kazi alichopangiwa.
 
Sa hz habari za kubadilisha vituo hakuna kwanza majina yametoka huko wizaran na vituo kabisa wakati zamani ilikuwa halmashauri ndo inapanga vituo,
So ukitaka kubadilishiwa nenda wizarani

Ila ukitaka kubadilishana na mtu inabidi usubir hadi watakapo ruhusu uhamisho
 
Kwa kuwa serikali imewataka walimu wapya kuwasili katika vituo vyao vya kazi walivyopangiwa kuanzia tarehe 18 mwezi huu!

1. Vipi malipo ya kufanya kazi kwa muda huu wa siku 13 za mwezi wa nne (April) yatakuwaje?

2. Huwa yanatolewa maelezo ya kurudishiwa nauli zitakazo tumika kuwasili vituoni. Kwa mwaka huu mbona maelezo hayo hayajatolewa?

3. Walimu waliomaliza masomo yao nyuma ya mwaka 2015 na kuombea kutuma maombi ya kazi , ajira zao zitatoka ndani ya mwaka huu wa fedha? Au itakuwa mwaka ujao wa fedha?

4. Mafundi sanifu wa maabara ajira zao mbona hazijatolewa ufafanuzi wowote!?

5. Kuna utaratibu gani wa mtu kuweza kubadilishiwa kituo cha kazi kabla ya kuripoti katika kituo alichopangiwa?
*MAELEZO KUTOKA KWA KATIBU MKUU UTUMISHI.*

1. Malimbikizo ya salary, yatalipwa automatic baada ya areas kuwa approved na maafisa utumishi, kuanzia pale ulipopanda. Hakuna tena kudai area

2. Uhamisho, kuhamisha mshahara ni jukumu la mwajiri wa awali, kama umehama

3. Kuhama mkoa ni lazima jina litokee kwenye orodha ya watumishi wanaohama.

4. Kwa wastaafu wanaodai areas, wanatakiwa kujaza fomu na viambatanishi ili ulipwe.

5.Malimbikizo ya mshahara kuonekana kisha kufutika, haijapotea ila inahitaji kuidhinishwa upya.

6.Kama hujapata areas, na madai ni ya muda mrefu fuatilia kwa afisa utumishi ili ujaze form maalum.
7. Ukipanda cheo, kiri haraka.

8.Posho za safari za kikazi zinatokana na status ya mtumishi, upandishaji wa vyeo vya watumishi hutegemea vikao vya DED, upandaji cheo inategemea fungu lililopangwa, mtumishi haruhusiwi kudai cheo. Hii ni kanuni. Promotion ni motisha kwa watumishi, si automatic. Mwajiri lzm apate taarifa za utendajikazi wa utumishi ndipo aandae promotion.

9.Madai kwa watumishi waliohama, yatashughulikiwa na mwajiri wa sasa baada ya kuwasiliana na mwajiri wa awali.

10. Upatikaji wa nyaraka, www.utumishi.go.tz na www.tamisemi.go.tz utapata nyaraka na huduma kwa kutumia simu au computer.

11. Nauli za likizo, inategemea bajeti ya halmashauri, ilipwe kabla ya kusafiri, akijisafirisha atadai. Maombi ya nauli za likizo yatahakikiwa kwa kutumia nauli za SUMATRA. Marufuku kulipwa nusu nauli.

12. Kusoma nje ya nchi, kama upo kwenye mpango wa mwajiri utalipiwa na kulipwa mshahara, kama haupo mwenye mpango, utachukua likizo bila malipo. Kibali kitatolewa na katibu mkuu kusafiri nje.

13. Rufaa ya matibabu, mwajiri alipe nauli na posho ya kujikimu. Ukijigharamia, mwajiri anatakiwa kukulipa.

14. Kutofautiana kwa mishahara kwa watumishi wenye sifa zinazofanana, kuna tume ya job evaluation inafanya utafiti hatua za mwisho, pia tatizo lilikuwa tsd kutoshirikiana na mkurugenzi. Lkn tsd imekuwa tsc, tatizo litakwisha.

15. Disturbance allowance italipwa kwa 10% ya mshahara wake wa mwaka. Kwa watumishi waliohama destination, hata kama ni ndani ya km5.

16. Kumbuka kutunza nyaraka, kufuatilia mifuko ya jamii na michango ili kuhakiki uwasilishaji wa michango kabla ya kustaafu

17.Uteuzi wa wakuu wa idara huzingatia: utendaji kazi, uongozi, royality, elimu, nk.

18. Tange kwa kila kada ijazwe na kuwasilishwa kwa afisa utumishi.

19. Waliocheleweshwa kupanda daraja, wanatakiwa kwenda kwa afisa utumishi ili ajenge hoja ya kupanda kwa mseleleko na kuomba kibali kwa katibu mkuu.

20. Kama uliwekwa kwenye mpango wa mafunzo halafu ukajilipia, mwajiri anatakiwa akurudishie gharama alizotakiwa kukulipia.

21. Punguzo la kodi ya mshahara 9% linahusu wenye mishahara ya chini. Mfano katibu mkuu anakatwa 30% ya mshahara.

22.May 2016 promotion zilisitishwa pamoja na mishahara ilisitishwa kwa ajili ya watumishi hewa. Vyeo vyao vipo, ila marekebisho yao yamesitishwa. Watarejeshwa ktk vyeo vyao vipya muda si mrefu

23. Uhakiki bado serikali kuu.

24.Vyeo vya kielimu ktk nchi kimuundo ni mpaka 1st degree. Masters, phd ni sifa za ziada tu.

25. Mishahara ya watumishi italingana na uzito wa kazi, miundo ya utumishi kurekebishwa ili watu wasifike bar/vidato vya mshahara.

26. Madeni yaliyokataliwa, yafuatiliwe ili kama ni tatizo la document, zitafutwe na kuprossess upya deni.

27. Walimu wa sayansi wanaofundisha na kufanya laboratory technicians wapewe allowances. Wataalam wa laboratory wanaandaliwa.

28. Kukaimu madaraka mwisho miezi 6, athibitishwe au asitishwe.
 
Nauli unarudishiwa ila uwe na rist za gharama,

Utapewa hela kujikimu ukiwa bado hujaanza kupokea mshahara japo hutolewa kwa siku 7 tu, mfano 70,000×7=490,000/- hicho ndo chanzo cha maisha yako ktk utumishi,

Kubadilisha kituo b4 kuriport nenda wizarani, ukiriport kuhama mpaka umalize miaka 2 ktk kituo husika,

By the way nenda kapge kaz ila kuwa na adabu ya matumiz ya fedha maana mambo si shwari nafkr jibu unalo mkuu!
Mkuu mbon hadi leo hela za kujikimu haijatoka,?
 
Wewe ulikuwa na shida kubwa ya ajira nenda kafanye kazi kituo ulichopangiwa huwezi kubadilishiwa kituo kabla hujaripoti na kwanza kazi kituo ulichopangiwa
 
Ndg zangu napenda kusema kuwa kumbe mtumishi feki hata utendaji kazi huwa ni feki.Kuna mtumishi alikuwa anasumbua sana kumbe ni feki hongera sana JPM na kamati yako.na hata watendaji wa kata wamo hewa.?
 
Back
Top Bottom