Malimwengu: Mwanaume aota pua kwenye paji la uso

Malimwengu: Mwanaume aota pua kwenye paji la uso

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,114
Reaction score
34,957

Reuters
mtu mmoja ameota pua mpya katika paji lake la uso baada ya pua yake ya asili kuharibiwa vibaya katika ajali ya gari. Mtu huyo kutoka katika jimbo la Fujian nchini China, anayejulikana kwa jina moja la Xiaolian alikuwa miongoni mwa waliopata ajali mwaka jana, na baada ya kushindwa kupata matibabu ya maana kwa ajili ya pua yake hiyo, iliharika kabisa na isiweze kufanya kazi. Xiaolian mwenye umri wa miaka 22 alikuwa na chaguo moja tu kutoka kwa wataalamu wa upasuaji: kuwa na pua juu ya paji la uso. Pua hiyo imetengenezwa kutokana na ngozi ilikatwa kutoka katika mbavu zake kabla ya kutengenezwa kwa umbo la pua. Wataalamu wa upasuaji wanasma kuwa wanakusudia kuihamishia pua hiyo mahala palipokuwa pua ya awali hivi karibuni.

Chanzo: On MSN
 
Kamasi zitapandaje hapo? Au kwa sababu ni mchina itabidi aruke sarakasi?
 
mara ya kwanza nilipoiona hii habari, nikasema he muzauza gani haya....
 
Back
Top Bottom