Malimbikizo ya madai ya watumishi serikalini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malimbikizo ya madai ya watumishi serikalini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kkitabu, Jan 2, 2012.

 1. k

  kkitabu Senior Member

  #1
  Jan 2, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kupandishwa watumishi vyeo ni mpango unaoeleweka na siyo jambo la dharura wala ajali. Kwa mujibu wa utaratibu wa Serikali, mtumishi hupandishwa cheo kwa misingi miwili. Kwanza, kutimiza masharti ya muundo wake wa utumishi, na pili, kuwepo kwa fedha kwenye bajeti ya Wizara au Idara husika kwa madhumuni hayo. Hivyo iweje leo mtu apandishwe madaraja bila kulipwa mshahara stahiki? Hili halieleweki na wala halikubaliki.
  Alisema baada ya hotuba yake ya Februari, 2009 na Serikali kulipa takriban shilingi bilioni 64 kwa madai ya walimu mwaka huo, bado Serikali ililipa tena shilingi bilioni 29.8 kati ya Julai 2010 na Oktoba 2011. Hivi sasa nimeambiwa tena kuna madai mapya yaliyofikia shilingi bilioni 52.7.
  Sina tatizo na madai yanayostahili kulipwa na najua kwamba shilingi bilioni 22.5 zimetolewa na kati ya hizo shilingi bilioni 19.2 zimekwishapelekwa kwenye Halmashauri husika na shilingi bilioni 3.3 ni kwa ajili ya waajiriwa wa Wizara. Zilizobakia zitalipwa kwenye mishahara yao


  Mbona watumishi wengi wamebadilishiwa mishahara tangu mwezi June lakini mpaka sasa wanalipwa kwa rates za zamani
   
 2. n

  nyangasese Senior Member

  #2
  Jan 2, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona watumishi wengi wamebadilishiwa mishahara tangu mwezi June lakini mpaka sasa wanalipwa kwa rates za zamani[/QUOTE]
  Heri ya hao tangu june.Mwanza ni miaka 2 sasa walimu wanalipwa kwa rates za zamani ingawa majina yalikwishatumwa hazina miaka mingi.Hii ndio Tanzania acha wanasiasa wadanganye wananchi kwa matamko yenye matumaini lakini mioyoni wanasita kufanya maamuzi.
  Kama viongozi wanalalamika kila mara unategemea nini kwa watumishi wa chini.Bila shaka huenda tukasikia maneno hayahaya ktk hotuba ijayo ya kufunga mwaka 2012.Ama kweli serikali yetu ni sikivu
   
 3. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Wanadai 'SERIKALI HAINA FUEDHA'!
   
Loading...