mkalamo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 343
- 359
Ni kwenye dua aliyowaalika Dk watia Nia ya Ubunge DK Chakou Tindwa na Abdalla Ulega.
Hata hivyo Ulega alichimba hakuhudhuria
Asema jimbo linataka mtu muungwana kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ambaye pia ni mkazi wa Mkuranga,Adam Kigoma Malima,amewataka wakazi wa jimbo hilo,kutokurudia makosa waliyoyafanya miaka mitano iliyopita ya kuchagua kiongozi,asiyejihusisha na shida za wananchi.
Amesema katika Miaka mitando iliyopita wananchi wengi wamejikuta mkononi mwa Polisi kwa amri ya kiongozi waliyemchagua na kusema maisha hayapaswi kuwa hivyo kwa kuwa uongozi unakuja na kupita
Malima ,alitoa kauli hiyo jana katika wilaya ya Mkuranga wakati akifanya dua ya kuwarehemu,wazee wa mji wa Mkuranga waliotangulia mbele ya haki, ambapo aliwaalika watia nia wa nafasi za ubunge na udiwani wa jimbo hilo.
Amesema wana Mkuranga wanapaswa kumchagua mtu muadilifu,asiyetumia nafasi yake ya Madaraka kuwanyanyasa wengine kwa kuwa maadaraka yanampata mtu na kuondoka ilihali mahusiano ya kindugu yakibaki wakati wote.
“Hatuwezi kufikia ubora wa Mwenyezi Mungu,lakini huyo mtu tutakayempa uongozi ni lazima awe rahimu,awe na mapenzi na ninyi asiwe na tabia ya kuwafunga funga wenzake kila wanapomuuzi nyie mlikuwa mnaniudhi tena kuna wengine walikuwa wananitukana halafu wanakuja kuniomba nauli tena wakati huo mimi Waziri lakini sijamuita Polisi kumwambia chukua hawa waweke ndani”alisema Malima
na kuongeza
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
“Bahati mbaya sana yule mdogo wangu na huyu Mdogo wangu,wote wadogo zangu huyu maana yake huyu aliyeingia nimewakaaribisha wote yule kagoma kuja, huyu kaja nami si Simba wala Yanga,ila huyu aliyekuja anafanana kidogo tabia na mimi yule mwingien Hapana”alisema Malima.
Miongoni mwa watia Nia wa nafasi ya Ubunge waliohudhuria hafka hiyo ni pamoja na DK Chakou Khalfan Tindw,huku Mbunge aliyemaliza muda wake akishindwa kujumuika katika dua hiyo.
Akielezea sababu ya kutochukua fomu ya Ubunge Malima alisema,jukumu lililopo ni kuhakikisha wanamsaidia Rais Samia Suluhu Hassan,katika maeneo waliyokabidhiwa na kwamba hana shaka na nafasi ya Rais Samia katika jimbo hilo kwa kuwa wananchi wanamuelewa.