Malima na sheria ya kudhiditi silaha nchini

Bandio

Senior Member
Feb 19, 2012
101
12
Jana kwenye taarifa ya habari ya saa 2 usiku, TBC1, nilimsikia Mh. Malima akielezea jinsi alivyoibiwa kwenye hoteli alikokuwa amefikia huko Morogoro, na katika maelezo yake alisema katika tukio hilo silaha zake pia zilikuwa chumbani lakini waporaji hawakuzigusa.

Maelezo yake yamanipa wasiwasi wa uwepo wa hatari na kuwa yawezekana kabisa mmiliki halali wa silaha kuibiwa silaha yake na silaha hiyo kutumiwa kwenye uhalifu.

Wanasheria naomba mnisaidie. Hivi hapa Bongo kuna sheria yeyote inayodhibiti au kutoa mwongozo wa matumizi au uifadhi salama wa silaha? Je wamiliki wa silaha wanapewa muongozo wa kulinda silaha zao kabla ya kuruhusiwa kuzimiliki?

ASANTENI.
 
Back
Top Bottom