Sabato masalia
JF-Expert Member
- Oct 16, 2011
- 228
- 134
TAREHE 12/12/2012 ndio siku ya kustaafu mkurugenzi wa misitu na nyuki, bwana Felician Kilahama, lakini mtu huyu bado anaokena kuhaha aongezewe muda ili aendelee kuvuruga zaidi ikiwemo vibali feki vya uvunaji wa misitu katika shamba la Sao Hill.
Kilahama ana mtandao maalumu wa vijana wake kila msimu vinapotoka vibali basi naye hujihusisha na uuzwaji kinyume cha sheria wa vibali hivyo.
Kilahama ana madudu mengi ya kutia kichefu chefu sijui wana agenda gani kwa kumuongezea muda mharibifu huyu. tena alitakiwa kustahafu zamani sana ila alichakachua umri wake.
Tunakuomba balozi Kagasheki pamoja na kuwa huyu Kilahama ni mhaya mwenzako, tunasema hafai asipewe muda watafutwe vijana wa kuchapa kazi hapo.

Huyu ni Jamaa aliyekuwa MWADILIFU aliyepitiliza, hilo hakuna kupinga hata kidogo. Swala la uuzaji wa mitiki Longuza aliloahidiwa mamilioni na yeye kuya kataa mpaka akatishiwa, maisha ni ushahidi tosha. HUYU NI MMOJA WA WATUMISHI WA WATU WALIOKUWA WAMEBAKI. Kuhusu kuongezewa muda siungi mkono ilibidi afundishe wengine kuchukua nafasi yake.
By the way katika Sao hill hapo ndo napata wasi wasi na mleta mada, kwani kulikuwa na watu wananunua vitalu toka serikalini kwa bei ndogo, halafu wanawauzia watu wa viwanda kwa bei kubwa. Yeye alikata mirija hii na kuhakikisha kuwa serikali inauza direct viuwandani najua kuna watu walichukia sana.
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.