Mali ya urithi inateketea, Msaada na ushauri wenu muhimu

Mali ya urithi inateketea, Msaada na ushauri wenu muhimu

Porojo ndefuu unataka kuwiangiza watu "mkenge".

Huna mali wala urithi, mwenye mali anapiga porojo namna hiyo?

Wajinga Ndiyo Waliwao.
 
Ushairi mzuri sana!
...mdau kanikumbusha mambo ya "MALENGA WETU"

Ngoja na Mimi niweke verse za kwangu!

"... Naja kwenu waungwana, nawapa yangu salamu,
Nawasalimu watwana, walimu na Maimamu,
Shukurani kwa Maulana, kwangu hakuna
ugumu,
Ipi tofauti yao, kibogoyo na mapengo.
Najiona zumbu kuku, kubaini tofauti,
Namuuliza Bukuku, yupo kimya amenyuti,
Ahadi kutoa buku, kwalo jibu madhubuti,
Kibogoyo na mapengo, ipi yao tofauti.
Swali kwa Bini Zuberi, kapekue vitabuni,
Kafungue na Zaburi, kupata jibu makini,
Wala sione hatari, uliza wanazuoni.
Kibogoyo na mapengo, ipi yao tofauti.
Nawe Tedi wa Mapunda, mapengo unayajua,
Naijo yamempenda, Nesrori nae anajua,
Mlo mkuu ni matunda, na uji si tunajua,
Kibogoyo na mapengo, ipi yao tofauti.
Steji ameivuka, ankali wangu Tevini,
Mdomoni yashatoka, kayatupa shimoni,
Meno yalisha mtoka, asubiri uzeeni,
Kibogoyo na mapengo, ipi yao tofauti.
Ya mtoto yakisha toka, huota ya ukubwani,
Hata akila bazoka, hayanguki sakafuni,
Pengo hili kuzibika, kawaida maishani,
Kibogoyo na mapengo, ipi yao tofauti.
Pengo hili pengo gani,halizibiki ukubwani,
Kibogoyo mtu gani, hapa kwetu mtaani,
Meno hana asilani, babu yake Selemani,
Kibogoyo na mapengo, ipi yao tofauti.
Yamesha watoka meno, kibogoyo na mapengo,
Hakuna alo na meno, kuota hayana mpango,
Vibunye hawana meno, wazee wapinda mgongo,
Kibogoyo na mapengo, ipi yao tofauti.
Kadi tama tamatia, kalamu naweka chini,
Jibu siache patia, na kunitoa shakani,
Wengi tunayapitia, kukosa meno kinywani,
Kibogoyo na mapengo, ipi yao tofauti
".
 
Nakusoma vizuri sana, hebu hapo kwenye kubadili mchakato ndo ushindilie zaidi. Unajua mabadiliko yoyote lazima yatasumbua watu fulanifulani. Lakini kwa ujumla yakifanyika kwa heri huleta faraja jwa wote. Sitaki jamii yangu iteseke katika hilo. Nisaidie kwa ufafanuzi zaidi. Yupo na ndugu yangu FaizaFoxy kama hana mazongemazonge atarefusha fikra za hapa.

Umeanza kwa kujihami mapema, unayakinisha nilichokiandika juu hapo.

Huna mali huna urithi.

Unabwabwaja na kuhororoja bila mpango.

Wajinga Ndiyo Waliwao.
 
Barabara ukiitumia sana haikupi shida kudhibiti usalama wake.. FaizaFoxy na wahenga walisema Farasi uliyewahi kumpanda hakutishi miondoko. Kama niko sahihi unaweza kubonyeza kitufe kimeandikwa like
 
Last edited by a moderator:
Nilivoelewa..

Wazazi Wake ni JK NYERERE..

Bamkubwa zake ni MWINYI,MKAPA na J KIKWETE..

Huyu Rafiki mpya wa kike ni CHINA..

Huyu mdogo wake anaempa ushauri aachanae na huyo rafiki mpya(CHINA) ni CHADEMA..

No ni Mmarekani.
 
Barabara ukiitumia sana haikupi shida kudhibiti usalama wake.. FaizaFoxy na wahenga walisema Farasi uliyewahi kumpanda hakutishi miondoko. Kama niko sahihi unaweza kubonyeza kitufe kimeandikwa like
 
Last edited by a moderator:
Kiranga unajua hata mimi nilikuwa na mtazamo kama huo lakini nimeona kwa nini tusitumie legacy kama za akina TOYOTA hivi CAT yaani ni kizazi na kizazi na vizazi hivyo haviumii katika kusonga mbele.

Mimi sina matatizo na habari hiyo kimsingi, after all, why reinvent the wheel if the wheel is already there?

Falsafa yangu inatokana na kutotaka kufanya mali kuwa mhimili wa namna ya ninavyoweza kuwaenzi wazazi wangu. Kimsingi kwangu, urithi ni namna ya kuwaenzi wazazi. Kwa wengi ni sehemu ya kuhemea. Kwa hiyo naweza kuomba kupewa manuscripts za mshua kama urithi. Au kutaka michoro yake ya majengo. Something intellectual, not material.

Pia binafsi najiona kama ninaweza kujitafutia mwenyewe na hivyo mali za nyumbani hata huwa sizifikirii kwamba siku moja zitakuwa zangu. Naona kama kuna wengine watakaozihitaji zaidi. Ninachohakikisha ninkwamba wakihitaji msaada, kaka mkubwa nitakuwepo kuwasaidia. Maana mtu anaweza kurithi nyumba akashindwa hata kuipiga rangi, au kuilipia kodi.

Zaidi ya hapo, labda nimemsoma sana Piketty kuhusu habari za income distribution na redistribution.

Au nimekunywa sana maji ya Dhammapada yaliyobakisha kidogo tu kunifanya niishi maisha ya utawa wa ki Buddhist huko kwenye milima ya Himalaya.

Sasa ukichanganya yote haya, utaona ni kwa nini sina hulka ya kutolea macho mali ya urithi.
 
Last edited by a moderator:
Barabara ukiitumia sana haikupi shida kudhibiti usalama wake.. FaizaFoxy na wahenga walisema Farasi uliyewahi kumpanda hakutishi miondoko. Kama niko sahihi unaweza kubonyeza kitufe kimeandikwa like

Mtakuja na kila porojo, mali bila akili ni mali?

Hamna mali hamna urithi.
 
Umeanza kwa kujihami mapema, unayakinisha nilichokiandika juu hapo.

Huna mali huna urithi.

Unabwabwaja na kuhororoja bila mpango.

Wajinga Ndiyo Waliwao.

usilolijua ni usiku giza. Ushauri; unapopitia uzi pitia na koment za wengine
 
Kwa utani ulioandika tu hapa "Eti bill Gates ana ndururu za kununulia matunda au juisi ya azam hawana mpunga kabisaa" .Naona history ni fiction tupu
 
nashangaa watu wengi walikuwa wanashindwa kun'gamua jamaa kwamba alikuwa anawasilisha ujumbe kifalsafa.
 
Kwa utani ulioandika tu hapa "Eti bill Gates ana ndururu za kununulia matunda au juisi ya azam hawana mpunga kabisaa" .Naona history ni fiction tupu

katumia lugha ya mfano hakuna familia tz yenye utajiri zaid ya bill gate ila ni tz ndio ina utajiri huo na hao baba yake ni nyerere na hao wengine ni utawala wa marais wa awamu ya 2, 3 had wa 4 unaoisha
 
Mleta uzi amejikita ktk nchi yetu ya tanzania .baba yke aliefariki ni jk nyerere hao baba mkubwa na wadogo ni mwinyi.mkapa na jk.anatamani wapinzani wachukue nchi ili kuokoa rasilimali zetu zilizobaki.

FaizaFoxy
 
Last edited by a moderator:
Fasihi ktk sehemu yake.

Ushauri: Ukishaanza kuona na kutambua kwanini mali hizi ziko hivi, ujue umeshakuwa. Nakuomba ndg ujitie nguvu tayari ya kutake over kwenye kusimamia mirathi yenu rasmi. Mshakuwa wakubwa na nadhani mnaweza kujiamria mambo yenu kwa msitakabali wa familia yenu.

Wanaokubezeni kwamba hamjakuwa wana lao jambo, wanataka waendelee kusitarehe ilihali mali inaisha.
 
Mleta uzi amejikita ktk nchi yetu ya tanzania .baba yke aliefariki ni jk nyerere hao baba mkubwa na wadogo ni mwinyi.mkapa na jk.anatamani wapinzani wachukue nchi ili kuokoa rasilimali zetu zilizobaki.

Na mm ndivyo nilivyo elewa mkuu
 
Back
Top Bottom