Mali ya urithi inateketea, Msaada na ushauri wenu muhimu

Mali ya urithi inateketea, Msaada na ushauri wenu muhimu

Mwanachama Sahihi

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2015
Posts
572
Reaction score
217
Ni hivi, wazee wetu walikuwa na mali nyingi ambazo na wao walirithi toka enzi hizo. Lakini walijitahidi sana kuzilinda kwa ajili ya kizazi na kizazi.

Bahati mbaya tukiwa bado na umri mdogo wakatangulia mbele za haki. Hatunao tena Nawaombea kwa mola wapumzike kwa amani.

Bahati iliyo njema ni kwamba waliacha utaratibu wa kuendesha na kusimamia mali zetu na kana kwamba hiyo haitoshi utaratibu huo uko wazi kabisa kwa wasimamizi na warithi.

Wasimamizi wenyewe ni Baba zetu wadogo ambao ki umri kwetu ni wakubwa tu. Na katika muktadha huo ijulikane na wao wana familia zao.

Baba mkubwa katika hao aliomba kwa utaratibu uliopo asimamie kwa muda. Alikubaliwa na akafanya hivyo. Tatizo lilikuja kuruhusu marafiki zake nao wakawa na ufahamu wa ukwasi tulionao.

Kidogokidogo na wao wakaanza kuonja na kuyafahamu mema ya familia. Walengwa wa mali tupo bado wadogo kipindi hicho na tunahimizwa kupata maarifa na ujuzi wa kujisimamia, tunakula, tunalala, tunavaa, tunatibiwa na maisha yanaendelea umri nao unasogea.

Kwa utaratibu bamkubwa akamaliza awamu yake, hata hivyo dalili za kwamba misingi ya uhai wa mali zetu ilionekana kutikiswa.

Zaidi ni kwamba marafiki zake hawakutegemea kipindi cha bamkubwa kuwa kifupi hivyo. Sisi kama kawaida tupo tunaona na umri unasogea.

Shauku kubwa ni lini utaratibu utakuwa upande wetu ili tujisimamie. Tunashukuru bamkubwa aliyefuata alijaribu kupunguza kelele za wale waliotaka kuwa na uchu na mali zetu na kibaya zaidi hata sisi ndugu kwa ndugu tulianza kuwa na mvutano wa hapa na pale.

Msukumo ulikuwa mpana kiasi na sijui ni kwa vile tulianza kujifahamu zaidi maana sasa tulianza na sisi kufuatilia kwa kando. Kusema kweli mali ipo. Huu siyo uongo.

Mali iliyopo naweza nikatania kwa kusema hao akina bill gates wana ndururu za kununulia matunda sokoni au juisi za Azam. Hawana mpunga kabisa aisee.

Mali na pesa iko mingimingi. Niseme tu haraka kwamba pamoja na huyu bamkubwa-mdogo kuonyesha kwamba alikuwa mkali mdomoni katika kusimamia, lakini tatizo lake lilikuwa ni kututangaza mno.

Siku hizi ukimuuliza kwa nini matangazo kiasi kile tena kwa papara, yeye anadai ni ngumu "kufanikiwa kibiashara kama huitangazi". Nyie watoto tangu lini uliwasha taa na ukaiweka uvunguni"? Weka mezani iwang'arie pande zote.

Hamuoni mahitaji ya muhimu mnayapata? Tulieni watoto mkifikia hatua ya kujisimamia mtajua nasema nini (haachi kusisitiza).

Hofu yangu na wadogo zangu ni tofauti ya haya mahitaji ya muhimu. Wenzetu ukiwaona wanapata mahitaji ya msingi na ya lazima huku wakifanya starehe zisizo za lazima wala msingi.

Sisi tunahangaika na mahitaji ya muhimu tu. Siku moja rafiki yake akatutania akitoka ulevini huko akasema "nyie endeleeni kupata hayo ya muhimu tu maana ni muhimu kuwafanyia hivyo kwa muda hasa ukizingatia ni lazima dunia iwe na vibarua wa kufanya kazi".

Tunashukuru tupo hai maana awamu yake imepita na mali ipo japo inapungua. Yeye yuko na mambo yake na anaonyesha kutokutumbuka ipasavyo.

Huyu wa sasa hivi anatusihi kuwa na marafiki imara. Marafiki imara hasa kipindi hiki kinachoonyesha tunakwenda kukabidhiwa mikoba ya kujisimamia.

Umri umeenda na hata wadogo zangu waliokuwa "vichanga" wakati wazee wanafariki, sasa wanajitambua. Wao hupenda kujiita vijana wa dotikomu. Nikiwauliza maana ya dotikomu hunicheka tu. "Broza bana"?

Juzi kati usiku niliota ndoto. Actually nilipomaliza kuota na kumbe sikuzima taa mida hiyo ya saa nane usiku, sikupata usingizi hadi kunakucha.

Ndotoni alikuja binti mzuri sana na alijua sijaoa. Tulianza urafiki wa hapa na pale na mwishowe akawa na access ya baadhi ya mali na tu vitu twangu.

Tukaelewana na kupendana sana kiasi cha kuanza utaratibu wa kufunga ndoa. Kwetu anakuja kama kawaida na kwao nina imani nitaendaga tu.

Siku moja akaja mdogo wangu kijana-wa-ibadani akanisihi kuwa anauona urafiki wa mashaka baina yangu na huyo binti na kwamba siku nikijatanabahi nitakuwa nimechelewa kujinasua. Mali zangu zake na zake zake…Ghafla nikashtuka toka ndotoni.

Win-win situation, nilijisemea. Lakini wakuu mali inapungua sana na sijui tutakabidhiwa hali ikiwa namna gani, marafiki gani nifanye nao mahusiano.

Madogo wameanza kuhoji lini tutajiamria na kufanya yetu. Uzuri mimi napita sana huku JF na naona ushauri wa aina mbalimbali.

Nimejiunga hivi karibuni ili ikibidi mtusaidie ushauri wa jambo hili mahususi.

MALI YA URITHI INATEKETEA MSAADA NA USHAURI WENU.
 
G3T, ungesemea hapa ili darasa liwe wazi zaidi kwa wengi wetu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu ushauri wangu wa kwanza ni kua unapoandika jambo muhimu kama hili jaribu kuandika kwa kifupi na kwenye kiini cha jambo unalolotaka ushauriwe

Pili je umeongea na babako mkubwa kuwa sasa umekuwa na unataka kuchukua madaraka ya mali yenu? Je mali ilikua imeorodheshwa wakati baba yenu alipoondoka ? Kuna waraka wowote wa kisheria kuhusu hili jambo ? Umri wako kisheria unaruhusu kukabidhiwa mali yako? kama ndio unaweza kuchukua jukumu ? kama ni ndio - ommba ukabidhiwe haki yako ya urithi
 
Mimi siwezi kukushauri kuhusu migogoro ya mirathi kwani falsafa yangu haifagilii mirathi, inafagilia kila mtu kutafuta chake.

Ingawa kwa sababu hiyo hiyo sifagilii wanaotapanya mali za waliotutangulia.
 
Mleta uzi amejikita ktk nchi yetu ya tanzania .baba yke aliefariki ni jk nyerere hao baba mkubwa na wadogo ni mwinyi.mkapa na jk.anatamani wapinzani wachukue nchi ili kuokoa rasilimali zetu zilizobaki.
 
Jamaa katumia vema Fasihi..

Hapa anaongelea Nchi yetu Tajiri ya TZ..
 
Nilivoelewa..

Wazazi Wake ni JK NYERERE..

Bamkubwa zake ni MWINYI,MKAPA na J KIKWETE..

Huyu Rafiki mpya wa kike ni CHINA..

Huyu mdogo wake anaempa ushauri aachanae na huyo rafiki mpya(CHINA) ni CHADEMA..
 
Mleta uzi amejikita ktk nchi yetu ya tanzania .baba yke aliefariki ni jk nyerere hao baba mkubwa na wadogo ni mwinyi.mkapa na jk.anatamani wapinzani wachukue nchi ili kuokoa rasilimali zetu zilizobaki.

Pweinti tekin. Nami baada ya kumaliza kusoma hii ngano ningemaonika kama wewe ila umeniwahi.
 
Mleta uzi amejikita ktk nchi yetu ya tanzania .baba yke aliefariki ni jk nyerere hao baba mkubwa na wadogo ni mwinyi.mkapa na jk.anatamani wapinzani wachukue nchi ili kuokoa rasilimali zetu zilizobaki.

Huyu jamaa siku zijazo atakuwa mwanafalsafa mkubwa
 
siamini urithi naamini changu ... kama inapotea mnaweza badili mchakato mkanadi ila kwa kuwaenzi wazee mnanunua ninyi ninyi ili kuondoa huo utaratibu wa walezi wenu
 
Kiranga unajua hata mimi nilikuwa na mtazamo kama huo lakini nimeona kwa nini tusitumie legacy kama za akina TOYOTA hivi CAT yaani ni kizazi na kizazi na vizazi hivyo haviumii katika kusonga mbele.
 
Last edited by a moderator:
​hadi umri huu wa kuingia site ya GT bado hujaruhusiwa tu kusimamia mali
 
siamini urithi naamini changu ... kama inapotea mnaweza badili mchakato mkanadi ila kwa kuwaenzi wazee mnanunua ninyi ninyi ili kuondoa huo utaratibu wa walezi wenu

Nakusoma vizuri sana, hebu hapo kwenye kubadili mchakato ndo ushindilie zaidi. Unajua mabadiliko yoyote lazima yatasumbua watu fulanifulani. Lakini kwa ujumla yakifanyika kwa heri huleta faraja jwa wote. Sitaki jamii yangu iteseke katika hilo. Nisaidie kwa ufafanuzi zaidi. Yupo na ndugu yangu FaizaFoxy kama hana mazongemazonge atarefusha fikra za hapa.
 
Last edited by a moderator:
Daima kwa mfumo huu wa kufungua milango kwa wageni na wakubadilisha viongoz + vyama ving(demokras) lazima hazina hiyo iporomoke yote na mwisho familia inabaki haina kitu na kuangukia utumwan
 
Nakusoma vizuri sana, hebu hapo kwenye kubadili mchakato ndo ushindilie zaidi. Unajua mabadiliko yoyote lazima yatasumbua watu fulanifulani. Lakini kwa ujumla yakifanyika kwa heri huleta faraja jwa wote. Sitaki jamii yangu iteseke katika hilo. Nisaidie kwa ufafanuzi zaidi. Yupo na ndugu yangu FaizaFoxy kama hana mazongemazonge atarefusha fikra za hapa.

kubadili mchakato kwa namna moja au nyingine jamii yako lazima iathirike ,.. mlezi wako ni msimamizi ....kubadili aina ya utawala uliopo si kitu kirahisi kukubalika kwa waliozoea kukaa na kula wakiwa hapo juu.. hapa italeta mtafaruku na kuibui yaliyouvunguni na kuweka juu ya kitanda,.. hapo ndipo itatokea mpasuko wa kusema utawala uliopo uendelee na wengine kusema utawala uliopo usiendeleee... mnaweza kufika mbali na kuomba ushauri kwa majirani wenye hekima mwisho wa siku lazima mtafikia hatua ya kugawana mali hapa ndipo mda wa kuenzi wazazi wetu kwa kununua mali zile na kuziendeleza huku maadui wako wakitoa macho... kiukweli ni mchakato mgumu aliyezoea kula kwa kugandamiza wengine moyo wake utapa tapa na huwa hayupo tayari kuachia ngazi kwa kuwa anajua revenge its their always
 
Back
Top Bottom