Malezi ya DADA WA KAZI.

Malezi ya DADA WA KAZI.

huo ndo ujinga wa wazazi wengi wanaoelekeza akili zao katika kusako shekeli halafu wanasahu kama wanawatoto home
usilete za uswazi, acha familia zijilee, we utamtafutia msichana mwingine?
lea familia yako, achana na familia za watu

hivi we ulishapaona labour nahisi una roho za huyo dada
 
Binafsi nimekuwa mtu ambae nawapinga sana hg na hb kwa sababu hizo hizo hapo muhimu waeleze

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
mwambie ndg,wadada wa siku hz taabu tupu! mara awe na mistreatment kwa mtoto,mara atoke na mumeo,mara aje na viuchawi vya bibi yake,basi taabu tupu ndani ya nyumba. Kila siku najiuliza hv nikizaa itakuwaje na mambo ya kazi haya ndo presha inazidi kunipanda.
 
Wasichana wengi wa kazi hawapendi kazi zao wanafanya kujaribu kukabiliana na shida na ugumu wa maisha wengi hawana upendo hata kama hawana manyanyaso toka kwa muajiri wanavaa uhalisia wa utumwa na kuwa na hisia za ulipizaji kisasi ambapo matokeo huwaangukia watoto wasio na kosa lolote. Wanatakiwa kuelimishwa kwamba hii ni kazi kama kazi nyingine zisizo hitaji elimu kubwa na ni nyepesi kuliko zege na kuvuta torori wapende kazi na wawe na upendo wengine tunawatunza sawa na watoto wetu ili tuishi kwa amani na upendo lakini wapi! Wanaacha kazi kila uchao!
 
mmh! mweleze haraka iwezekanvyo.
sijajaliwa kupata mwana ila imeniuma mno
 
Mueleze bana!!! kabla hali haijawa mbaya zaidi...Huo ndio tunaita ujirani mwema...Ingekuwa ni mwanao anatendewa hivyo ungependa jirani akutaarifu kinachojiri unapokuwa hauko nyumbani...ukija kusikia huyo mtoto amefariki labda kwa mateso ayapatayo kwa huyo binti utajilaumu sana.

YAANI!
iKO TRICKY LAKINI.
Kuna watu ukiwaambia wanasema unawachonganisha na wafanyakazi wao.
Iliwahi kuntokea nikajiskia vbaya sana.DADA wa jirani alikua anamtesa mtoto - anampiga, anamwacha na wahuni kijiweni kisha yeye anaenda zake kuzurula. Nikachukua jukumu kwaarifu wenye mtoto.Jibu walilonipa nilichoka.
"Huyo dada anamwacha mtoto hapo ili kwenda kuchukua maziwa, hivyo siyo vibaya." Hawakujali hata kama kwa kumwacha kijiweni masaa 4- 6 ni hatari kwa mtoto.Mtoto angenajisiwa na wavuta bangi? Hayo ni maziwa gani yanachukuliwa kwa masaa? Na je huko kumpiga mtoto kila mara nako kulikua na sababu? Nilijiskia vibaya ile mbaya! Nikakoma kuingilia maisha nyumba za watu!
 
@TausiMzalendo....Pole sana aisee duh!!!! Kuna kipindi kimoja nilikuwa naangalia kwenye TV ya wazazi wenye watoto wachanga ambao wazazi wote ni wafanyakazi. Sasa wanakuwa na wasiwasi kuwaacha watoto wao na maHG. Wengine wakafikia uamuzi wa kutegesha video ambayo inaweza kurekodi kila kitu plae sitting room yao na huiweka katika namna ambayo HG hawezi kuistukia. Sasa waliyoyaona ndiyo yaliyowafanya wapeleke hizo video zao kwenye kipindi cha TV kama onyo kwa Wazazi wengine na wasaidizi wa ndani.

Nakumbuka mmoja aliachiwa mtoto wa miezi mitatu kamweka kwenye kiti cha watoto chenye bembea kuanzia alipoachwa naye saa 1 na nusu ya asubuhi hamkugusa wala kumpa chakula au hata kumbadilisha mpaka ilipofika saa 10 jioni alipojua Wazazi wake karibu kurudi ndio akamshughulikia wakati yeye mwenyewe alirekodiwa akiwa anakula, kuna wakati alipotea pale sitting room kama masaa mawili sijui alikuwa anajirusha kwa raha zake au alitoka kabisa ndani ya nyumba. Mwingine yeye alikuwa anaangalia movie za wakubwa saa zote na yule mtoto alikuwa akilia alikuwa anambabua vibao vya uhakika na kumsukuma bila ya huruma yoyote ile wakati yeye yuko busy na blue movies zake. Mtoto alikuwa analia mpaka analala usingizi. Yaani hawa wasaidizi wa ndani baadhi yao ni hatari sana.

YAANI!
iKO TRICKY LAKINI.
Kuna watu ukiwaambia wanasema unawachonganisha na wafanyakazi wao.
Iliwahi kuntokea nikajiskia vbaya sana.DADA wa jirani alikua anamtesa mtoto - anampiga, anamwacha na wahuni kijiweni kisha yeye anaenda zake kuzurula. Nikachukua jukumu kwaarifu wenye mtoto.Jibu walilonipa nilichoka.
"Huyo dada anamwacha mtoto hapo ili kwenda kuchukua maziwa, hivyo siyo vibaya." Hawakujali hata kama kwa kumwacha kijiweni masaa 4- 6 ni hatari kwa mtoto.Mtoto angenajisiwa na wavuta bangi? Hayo ni maziwa gani yanachukuliwa kwa masaa? Na je huko kumpiga mtoto kila mara nako kulikua na sababu? Nilijiskia vibaya ile mbaya! Nikakoma kuingilia maisha nyumba za watu!
 
Nna jirani yangu mwenye mtoto wa mwaka mmoja. Ye na mume wake wote wameajiriwa kwahiyo huwa wanamuacha mtoto na dada wa kazi.

Kitu cha kwanza kunotice ni kwamba siku mmoja wao akiwepo nyumbani mtoto halii lii sana.Mpaka kuna wakati hua nadhani labda wametoka kwa ukimya kumbe wapo. Ila wakiwa hawapo mtoto analia kila saa, na dada wa kazi full kumfokea na kumtisha kumpiga(pengine hua anafanya kweli).

Sasa juzi ndio alinichosha kabisa. Nilimkuta kakaa barazani alafu kamlaza yule mtoto juu ya miguu yake, kichwa kimegusa sakafu alafu anamnywesha uji. Uji mwingi unaishia chini na puani, mtoto analia, dada ni kelele tu "ntakupiga!!!"kwa wingi na kulalama kuhusu uji unaomwagika.

Sikusema neno ila leo nimefikiria weee nikaona kuwa mimi nisingependa mtoto wangu awe analishwa kwa style hiyo au kupigwa hata kufinywa na mtu yeyote yule katika umri huo. Sasa najiuliza kama nimweleze jirani namna mwanawe anavyokuwa treated akiwa hayupo au la. Kama jibu ni ndio, nianzeje????

Maoni tafadhali.
Mwambie bwana huwezi utaokoa maish ya huyo mtoto kunyweshwa uji naman kuna mtoto alikufa hivi hivi nakwambia. Tafadhal sana. Wambie hata ingekua ni mimi mama wa mtoto ningependa niambiwe
 
Back
Top Bottom