Mkulima na Mfugaji
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 1,056
- 1,869
Habar wanajamvi, mimi ni muajiriwa katika shirika lisilo la kiserikali na pia najishughulisha na kilimo cha machungwa na mahindi na pia ni mfugaji wa kuku wa kienyeji chotara aina ya kuroiler. Kutokana kwamba kazi niliyokuwa nayo ni ya mkataba na mkataba unaelekea mwishoni ila mpaka mwisho wa mwaka nitakuwa nimekusanya kiasi kisichopungua milioni tano ila malengo yangu ni haya yafuatayo kwani niko Muheza Tanga ambapo mazao mengi yanakubali
Kununua poli la ekari tano kwa Tsh milioni mbili
Kufyeka na kulima kwa trekta kwa Tsh laki tano
Kununua mbegu za mahindi hybrid kwa garama ya Tsh 250000
Gharama za kupandia mahindi ni TSh 200000
Gharama ya palizi mbili ni laki tano
Gharama za madawa ni TSh 20000
Pia baada ya hapo natarajia ekari Tatu nipande michungwa kwa Gharama ya Tsh 250000
Na ekari mbili kasoro Robo nipande mikorosho na pia nitaacha Robo ekari kwa ajili ya makazi na ufugaji wa kuku.
Jumla ya garama ni 3770000
*mimi mwenyewe ni mtaalam wa kilimo na mifugo hivyo shughuli nyingine kama kupuliza dawa na kuandaa miche nitakuwa nafanya mwenyewe.
Pesa iliyobaki ni ya dharura na pia nitakuwa bado nipo kazini kwa mwaka mmoja mbele hivyo pesa ya kutumia nitakuwa napata
Naombeni ushauri kwa hilo wazo langu kama lina mapungufu au halifai
Ahsanteni