Malengo ya mwaka 2026

jblus

Member
Joined
Nov 27, 2024
Posts
22
Reaction score
57
Kwa juhudi na kumuomba Mungu, nina imani mambo haya nitayatimiza mwaka huu 2026. Jua liwake mvua inyeshe inabid niyatimize kwa namna yoyote...

1: Kuimarika kiroho,

Natamani kuwa karibu na Mungu wangu zaid mwaka huu kuliko kuliko chchte. Amekua akinionekania kwenye mambo mengi sana hivo natamani mwaka huu niwe nae karbu zaid.

2: Kuimarika kiuchumi,

Natamani sana mwaka huu kuongezeka kiuchumi. Nina maisha ya kawaida sana, nimepanga, sina nyumba nina kiwanja tu, nina biashara ndogo ya kuniwezesha kula. Natamani mwaka huu nivuke level hii na kwenda level nyingine kwa kuongeza njia za kuniingizia kipato.

3: Nipate mahusiano imara,

Huu mwaka naomba sana Mungu anipatie mwanamke mwenye uchungu na maisha kama mm, aliyetulia na aliyemaliza ujana. mwanamke ambae tutaongozana nae kwenye safari ya kuwa na familia.

Kwa JUHUDI, IMANI NA MALENGO naamini kabla ya mwaka 2026 kuisha nitakua nimetimiza.

Ndugu yangu, malengo yako ww ni yapi kwa huu mwaka, hebu tuainishie hapo chini huenda tukapata nyongeza na kutiana moyo.
 
Utimize malengo yako mkuu πŸ™πŸ™πŸ™
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…