Malema huenda akasababisha vita South Africa

70% Of arable land, if I'm not mistaken boss
 

Hapo ajasababisha vita, wanaosababisha ni hao wanaoonea watu!
 
Nyerere sijui alitumia style gani kuhakikisha ardhi ina bakia mikononi mwa watanzania,Tanzania mapori kibao kuna sehemu nyingine yaani unaambiwa jikatie mwenyewe.
Tanganyika halikuwa koloni kamili la Uingereza kama Kenya na Zimbabwe hivyo hakukua na walowezi wakubwa wa kizungu wenye kuhodhi ardhi kubwa.

Hivyo baada ya uhuru ardhi yetu ilibaki mikononi mwa wazawa na serikali mpya.
 
Tanganyika halikuwa koloni kamili la Uingereza kama Kenye na Zimbabwe hivyo hakukua na walowezi wakubwa wa kizungu wenye kuhodhi ardhi kubwa.

Hivyo baada ya uhuru ardhi yetu ilibaki mikononi mwa wazawa na serikali mpya.
Halikuwa koloni kamili HOW?
 
Sisi tulikuwa koloni la mjerumani mkuu

Baada ya Vita yadunia mjeruman aliporwa makoloni yake pamoja na Tanganyika SO SISI TUKAPEWA KWA MWINGELEZA
Sijakataa manake kila kilichokuwa cha wajerumani kikachukuliwa na waingereza.

Ndio na jiuliza Nyerere alifanya nini .ambacho kinatu tofautisha na SA au Zimbabwe upande wa ardhi.

Sababu kama uhuru nchi zote zimepata uhuru,ila SA na Zimbabwe ardhi yao sio huru kwa asilimia kubwa inamilikiwa na Makaburu.
 
Bongo vituko balaa, mwingine alisema muamar gadafi alikuwa rais wa kuwait na watu walimwamini
 
Hakuna uhalisia kwa kilichotokea

Sent from my BLA-L29 using JamiiForums mobile app
 
Kiongozi hapo juu amekujibu vyema sana.

Sisi Tanganyika hatukuwa koloni kamili la Muingereza kama ilivyo kwa Kenya na Zimbabwe.

Baada ya Vita ya Dunia, mwaka 1919 Tanganyika alipewa Muingereza na League of Nation.
Muingereza alipewa nchi yetu kama muangalizi tu "Protectorate" kwamba watizameni hawa kwa niaba ya League of Nation(Tanganyika) na wakisha jielewa basi muwape uhuru wao.

Kwa hiyo Muingereza kwetu hakuwa na interest sana ni vile tu alipewa kutulinda na kututazama.
Ndio maana hata settlers, walowezi na mabwanyenye wa mashamba makubwa hawakuwepo, sana tulilima kwa ajili ya chakula tu.

Na ndio maana unaweza kusema Muingereza hakufanya lolote nchi hii tofauti na Mkoloni wetu Mjerumani.

Mjerumani yeye ndio aliyejenga barabara, reli, majengo mengiii na mashule, hata ikulu yetu (Government House) ikiitwa wakati huo walijenga Wajerumani.

Itoshe kusema Scenario yetu na wenzetu Afrika kusini na Zimbabwe ni tofauti sana.
 
Hilo ni kweli kabisa wengi wanadhani sisi tulikuwa koloni la Waingereza, kitu ambacho sicho.

Kwa kuongezea tuu, baada ya vita ya kwanza kuisha, the league of nations wakawa ndiyo wamiliki wa makoloni ya Mjerumani. Na katika mikataba waliyoiweka ilikuwa ardhi yote ya Tanganyika irudishwe kwa wanyeji chini ya msimamizi ambaye ni mkuu wa nchi (Gavana). Ndiyo maana waingereza hawakuwa na uwezo (kisheria) wa kumiliki ardhi ya Tanganyika, kwa kuwa ilikuwa teyari imetamkwa kisheria kuwa inamilikiwa na wenyegi.

Nyerere sijui alitumia style gani kuhakikisha ardhi ina bakia mikononi mwa watanzania,Tanzania mapori kibao kuna sehemu nyingine yaani unaambiwa jikatie mwenyewe.

Nyerere alichofanya baada ya uhuru ni kuirithi ile sheria iliyowekwa na the legue of nations (iliyokuja kuwa UN). Hata hivyo tushukuru Mungu kupata mtu kama Nyerere, angekuwa ni Kenyatta angeweza kujimilikisha nchi yote, kwa kuwa kisheria yeye ndiye msimamizi.
 
Nimekuelewa πŸ‘πŸ‘ πŸ’―.
 
Umefafanua vizuri asante nimekuelewa.
 
Hakuna kiongozi Bora aliyewahi kutokea katika bara hili Kama Nyerere, alikuwa sio mnafiki, nina wasi wasi Mandela aliyeapishwa mwaka 1994 pale Pretoria hakuwa Innocent Bali alikuwa clone yule, nimeishi south Afrika yaani haiingii akilini ukiniambia south Afrika iko huru Aiseee
 
Itoshe kusapoti hoja yako.
 
At least SA unaweza kusema kuwa ni Kwasababu ya ukoloni, waliporwa na hawajarudishiwa.

Sasa Tanzania nini kimesababisha uchumi kuwa mikononi mwa watu wachache, wahindi ambao hata hawakututawala.

Tena wameigawana kabisa nchi hii:

1. Iringa - ASAS

2. Kanda ya kati - Gulamali

3. Tanga - Binslum

4. Mwanza/ Shy - Jambo, Manji

5. Dar - Cha wote
 
Wanamiliki km ngapi Kati ya 945000 kms za ardhi ya tanganyika hao uliyowataja mkuu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…