Malema huenda akasababisha vita South Africa

kirikou1

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
4,011
2,000
Huwa sielewi ANC na Mandela walikuwa na wanapigania nini hasa? Haingilii akilini watu milioni 4 wanamiliki ardhi kwa zaidi ya 70% huku weusi wakimiliki kasehemu kadogo. Cha kushangaza wazuru wenyewe huwaanzishia fujo waafrika toka nchi zingine. Mandela na ANC sijawahi waelewa.
70% Of arable land, if I'm not mistaken boss
 
uttoh2002

JF-Expert Member
Feb 3, 2012
5,204
2,000
CIC Malema mwanasiasa mwenye misimamo mikali ameleta hali ya wasiwasi huku SA, hii ni baada ya kuwaambia wanachama na mashabiki wake kujiandaa kuuvamia mji unaokaliwa na Wakulima weupe uitwao SENEKAL. Malema kwa kujiamini amesema ni lazima atakeleze hilo na hamna namna nyingine. Vuguvugu la kuivamia Senekal linakuja baada ya mfanyakazi mweusi kuuliwa na boss wake ambae ni mkulima mweupe. Msikilize hapa chini

View attachment 1602012

Hapo ajasababisha vita, wanaosababisha ni hao wanaoonea watu!
 
Proved

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
9,886
2,000
Nyerere sijui alitumia style gani kuhakikisha ardhi ina bakia mikononi mwa watanzania,Tanzania mapori kibao kuna sehemu nyingine yaani unaambiwa jikatie mwenyewe.
Tanganyika halikuwa koloni kamili la Uingereza kama Kenya na Zimbabwe hivyo hakukua na walowezi wakubwa wa kizungu wenye kuhodhi ardhi kubwa.

Hivyo baada ya uhuru ardhi yetu ilibaki mikononi mwa wazawa na serikali mpya.
 
joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
5,958
2,000
Sisi tulikuwa koloni la mjerumani mkuu

Baada ya Vita yadunia mjeruman aliporwa makoloni yake pamoja na Tanganyika SO SISI TUKAPEWA KWA MWINGELEZA
Sijakataa manake kila kilichokuwa cha wajerumani kikachukuliwa na waingereza.

Ndio na jiuliza Nyerere alifanya nini .ambacho kinatu tofautisha na SA au Zimbabwe upande wa ardhi.

Sababu kama uhuru nchi zote zimepata uhuru,ila SA na Zimbabwe ardhi yao sio huru kwa asilimia kubwa inamilikiwa na Makaburu.
 
nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
8,808
2,000
Sio Lissu ambaye alitaka mali zetu za asili ziliwe na wazungu. Huyu nguchiro alikuwa anasema tutapelekwa MIGA rtc. Tundu Lisu ni kibaraka kama huyo mtangazaji aliyekuwa anamuhoji Malema.

Angalia hapa chini uongo wa Tundu Lisu ati London kuna basi moja ....... ..... ... hapa chini mtaa moja tu ulioko London hesbu hayo ni mabasi mangapi?

View attachment 1602420
Hapo ni Regent Street London kwa haraka tu utaona mabasi 5 sasa TL anawaaminisha Watanzania kwamba London kuna basi moja la ghorofa …. ujinga mtupu wa kumwamini hayawani.
Bongo vituko balaa, mwingine alisema muamar gadafi alikuwa rais wa kuwait na watu walimwamini
 
Bantugbro

JF-Expert Member
Feb 22, 2009
4,138
2,000
CIC Malema mwanasiasa mwenye misimamo mikali ameleta hali ya wasiwasi huku SA, hii ni baada ya kuwaambia wanachama na mashabiki wake kujiandaa kuuvamia mji unaokaliwa na Wakulima weupe uitwao SENEKAL. Malema kwa kujiamini amesema ni lazima atakeleze hilo na hamna namna nyingine. Vuguvugu la kuivamia Senekal linakuja baada ya mfanyakazi mweusi kuuliwa na boss wake ambae ni mkulima mweupe. Msikilize hapa chini

View attachment 1602012
Hakuna uhalisia kwa kilichotokea

Sent from my BLA-L29 using JamiiForums mobile app
 
THOMASS SANKARA

JF-Expert Member
Nov 13, 2014
1,779
2,000
Sijakataa manake kila kilichokuwa cha wajerumani kikachukuliwa na waingereza.

Ndio na jiuliza Nyerere alifanya nini .ambacho kinatu tofautisha na SA au Zimbabwe upande wa ardhi.

Sababu kama uhuru nchi zote zimepata uhuru,ila SA na Zimbabwe ardhi yao sio huru kwa asilimia kubwa inamilikiwa na Makaburu.
Kiongozi hapo juu amekujibu vyema sana.

Sisi Tanganyika hatukuwa koloni kamili la Muingereza kama ilivyo kwa Kenya na Zimbabwe.

Baada ya Vita ya Dunia, mwaka 1919 Tanganyika alipewa Muingereza na League of Nation.
Muingereza alipewa nchi yetu kama muangalizi tu "Protectorate" kwamba watizameni hawa kwa niaba ya League of Nation(Tanganyika) na wakisha jielewa basi muwape uhuru wao.

Kwa hiyo Muingereza kwetu hakuwa na interest sana ni vile tu alipewa kutulinda na kututazama.
Ndio maana hata settlers, walowezi na mabwanyenye wa mashamba makubwa hawakuwepo, sana tulilima kwa ajili ya chakula tu.

Na ndio maana unaweza kusema Muingereza hakufanya lolote nchi hii tofauti na Mkoloni wetu Mjerumani.

Mjerumani yeye ndio aliyejenga barabara, reli, majengo mengiii na mashule, hata ikulu yetu (Government House) ikiitwa wakati huo walijenga Wajerumani.

Itoshe kusema Scenario yetu na wenzetu Afrika kusini na Zimbabwe ni tofauti sana.
 
Chamoto

JF-Expert Member
Dec 7, 2007
5,900

Hilo ni kweli kabisa wengi wanadhani sisi tulikuwa koloni la Waingereza, kitu ambacho sicho.

Kwa kuongezea tuu, baada ya vita ya kwanza kuisha, the league of nations wakawa ndiyo wamiliki wa makoloni ya Mjerumani. Na katika mikataba waliyoiweka ilikuwa ardhi yote ya Tanganyika irudishwe kwa wanyeji chini ya msimamizi ambaye ni mkuu wa nchi (Gavana). Ndiyo maana waingereza hawakuwa na uwezo (kisheria) wa kumiliki ardhi ya Tanganyika, kwa kuwa ilikuwa teyari imetamkwa kisheria kuwa inamilikiwa na wenyegi.

Nyerere sijui alitumia style gani kuhakikisha ardhi ina bakia mikononi mwa watanzania,Tanzania mapori kibao kuna sehemu nyingine yaani unaambiwa jikatie mwenyewe.

Nyerere alichofanya baada ya uhuru ni kuirithi ile sheria iliyowekwa na the legue of nations (iliyokuja kuwa UN). Hata hivyo tushukuru Mungu kupata mtu kama Nyerere, angekuwa ni Kenyatta angeweza kujimilikisha nchi yote, kwa kuwa kisheria yeye ndiye msimamizi.
 
joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
5,958
2,000
Kiongozi hapo juu amekujibu vyema sana.

Sisi Tanganyika hatukuwa koloni kamili la Muingereza kama ilivyo kwa Kenya na Zimbabwe.

Baada ya Vita ya Dunia, mwaka 1919 Tanganyika alipewa Muingereza na League of Nation.
Muingereza alipewa nchi yetu kama muangalizi tu "Protectorate" kwamba watizameni hawa kwa niaba ya League of Nation(Tanganyika) na wakisha jielewa basi muwape uhuru wao.

Kwa hiyo Muingereza kwetu hakuwa na interest sana ni vile tu alipewa kutulinda na kututazama.
Ndio maana hata settlers, walowezi na mabwanyenye wa mashamba makubwa hawakuwepo, sana tulilima kwa ajili ya chakula tu.

Na ndio maana unaweza kusema Muingereza hakufanya lolote nchi hii tofauti na Mkoloni wetu Mjerumani.

Mjerumani yeye ndio aliyejenga barabara, reli, majengo mengiii na mashule, hata ikulu yetu (Government House) ikiitwa wakati huo walijenga Wajerumani.

Itoshe kusema Scenario yetu na wenzetu Afrika kusini na Zimbabwe ni tofauti sana.
Nimekuelewa 👍👍 💯.
 
joseph1989

JF-Expert Member
May 4, 2014
5,958
2,000
Hilo ni kweli kabisa wengi wanadhani sisi tulikuwa koloni la Waingereza, kitu ambacho sicho.

Kwa kuongezea tuu, baada ya vita ya kwanza kuisha, the league of nations wakawa ndiyo wamiliki wa makoloni ya Mjerumani. Na katika mikataba waliyoiweka ilikuwa ardhi yote ya Tanganyika irudishwe kwa wanyeji chini ya msimamizi ambaye ni mkuu wa nchi (Gavana). Ndiyo maana waingereza hawakuwa na uwezo (kisheria) wa kumiliki ardhi ya Tanganyika, kwa kuwa ilikuwa teyari imetamkwa kisheria kuwa inamilikiwa na wenyegi.Nyerere alichofanya baada ya uhuru ni kuirithi ile sheria iliyowekwa na the legue of nations (iliyokuja kuwa UN). Hata hivyo tushukuru Mungu kupata mtu kama Nyerere, angekuwa ni Kenyatta angeweza kujimilikisha nchi yote, kwa kuwa kisheria yeye ndiye msimamizi.
Umefafanua vizuri asante nimekuelewa.
 
Omary Ndama

JF-Expert Member
Apr 16, 2017
3,345
2,000
Huwa sielewi ANC na Mandela walikuwa na wanapigania nini hasa? Haingilii akilini watu milioni 4 wanamiliki ardhi kwa zaidi ya 70% huku weusi wakimiliki kasehemu kadogo. Cha kushangaza wazuru wenyewe huwaanzishia fujo waafrika toka nchi zingine. Mandela na ANC sijawahi waelewa.
Hakuna kiongozi Bora aliyewahi kutokea katika bara hili Kama Nyerere, alikuwa sio mnafiki, nina wasi wasi Mandela aliyeapishwa mwaka 1994 pale Pretoria hakuwa Innocent Bali alikuwa clone yule, nimeishi south Afrika yaani haiingii akilini ukiniambia south Afrika iko huru Aiseee
 
kawoli

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
5,733
2,000
Mandela tulidaganywa tu mkuu ndio sababu Malema anamheshimu Winnie Mandela kuliko Mandela
Mandela orijino aliuwawa wakatuletea wa kufanana nae ndio Mana alikuwa anawasikiliza wazungu kwa kila kitu
Screenshot_20201013-231721.jpg
 
kawoli

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
5,733
2,000
Hakuna kiongozi Bora aliyewahi kutokea katika bara hili Kama Nyerere, alikuwa sio mnafiki, nina wasi wasi Mandela aliyeapishwa mwaka 1994 pale Pretoria hakuwa Innocent Bali alikuwa clone yule, nimeishi south Afrika yaani haiingii akilini ukiniambia south Afrika iko huru Aiseee
Itoshe kusapoti hoja yako.
Screenshot_20201013-231721.jpg
 
Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
13,394
2,000
Huwa sielewi ANC na Mandela walikuwa na wanapigania nini hasa? Haingilii akilini watu milioni 4 wanamiliki ardhi kwa zaidi ya 70% huku weusi wakimiliki kasehemu kadogo. Cha kushangaza wazuru wenyewe huwaanzishia fujo waafrika toka nchi zingine. Mandela na ANC sijawahi waelewa.
At least SA unaweza kusema kuwa ni Kwasababu ya ukoloni, waliporwa na hawajarudishiwa.

Sasa Tanzania nini kimesababisha uchumi kuwa mikononi mwa watu wachache, wahindi ambao hata hawakututawala.

Tena wameigawana kabisa nchi hii:

1. Iringa - ASAS

2. Kanda ya kati - Gulamali

3. Tanga - Binslum

4. Mwanza/ Shy - Jambo, Manji

5. Dar - Cha wote
 
Omary Ndama

JF-Expert Member
Apr 16, 2017
3,345
2,000
At least SA unaweza kuwa ni Kwasababu ya ukoloni, waliporwa na hawajarudishiwa.

Sasa Tanzania nini kimesababisha uchumi kuwa mikononi mwa watu wachache, wahindi ambao hata hawakututawala.

Tena wameigawana kabisa nchi hii:

1. Iringa - ASAS

2. Kanda ya kati - Gulamali

3. Tanga - Binslum

4. Mwanza/ Shy - Jambo, Manji

5. Dar - Cha wote
Wanamiliki km ngapi Kati ya 945000 kms za ardhi ya tanganyika hao uliyowataja mkuu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom