Malecela, Kilango watema cheche | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malecela, Kilango watema cheche

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Aug 6, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,736
  Trophy Points: 280
  Malecela, Kilango watema cheche
  Imeandikwa na Maulid Ahmed; Tarehe: 6th August 2009 @ 16:53 Habari Leo

  Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango amesema, kuna udini na ukabila katika Bunge la Tanzania.

  Kilango amesema kuwa, wabunge wameanza kuonyesha wazi kuwa wanataka kuwachagua viongozi kwa kuzingatia dini na makabila yao.

  Mumewe, Mbunge wa Mtera, John Malecela ametahadharisha kwamba, upo uwezekano wa kutokea machafuko nchini kwa kuwa kuna watu wachache wanaohodhi mali nyingi.

  Wameyasema hayo leo nyumbani kwao, Sea View, Dar es Salaam, wakati wanapokea msaada wa vifaa vya walemavu kutoka Shirika la Hope Project for Disable Tanzania (HOPD) kwa kushirikiana na Kanisa la Christian Mission Fellowship kwa ajili ya majimbo ya Mtera na Same Mashariki.

  “…katika uchaguzi mdogo tunapokwenda unakuta wanasema tumchague fulani kwa sababu ni muislamu au mkristo mwenzangu …hiyo ni sumu kubwa ya amani na mshikamano wetu tulioishi kwa pamoja kwa muda mrefu mfano mimi ni mlutheri lakini baba yangu aliyenilea aliitwa Ally na tuliishi vizuri akinipeleka kanisani na kuninunulia nguo za pasaka…” amesema Kilango.

  “Sisi viongozi hatupaswi kupalilia udini na ukabila…” amesema Mbunge huyo aliye mstari wa mbele kupiga vita ufisadi.

  Kilango amewasihi viongozi wa dini wawafahamishe wananchi wa kuwapa mifano ya namna udini na ukabila vinavyoweza kupoteza amani ya nchi.

  Ametoa changamoyto kwa watuhumishi hao wa Mungu kuhakikisha hilo linafanikiwa kama wanavyopiga vita ufisadi.

  Malecela, amesema, machafuko yanaweza kutokea Tanzania kwa kuwa, watanzania wengi ni masikini, wachache wana mali nyingi.

  Waziri Mkuu huyo Mstaafu amesema, kama Tanzania inataka iendelee kuwa nchi ya amani, lazima kuwe na mgwanyo sawa wa mali.

  “Nimekwenda katika chaguzi ndogo 32 tangu kuanza vyama vingi na ukiwahubiria watu juu ya amani wanafurahi lakini sasa watu wachache wanamiliki mali nyingi na hiyo itaondoa amani inayofurahiwa”, amesema Malecela , Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Tanzania bara.

  “Nawaomba vijana na viongozi wa dini pigeni vita ufisadi, uonevu na wachache kuhodhi mali nyingi” amesema Malecela.

  Askofu Mkuu wa kanisa la Christian Mission Fellowship, Mgullu Kilimba amewataka viongozi wa Serikali pamoja na wabunge kuzingatia Katiba na kutoingiza ukabila na udini kwenye sheria hiyo mama.

  “Udini na ukabila umeanza kuitafuna nchi yetu…kama udini unaanza kuingia kwenye Serikali yetu utatumaliza, taifa hili lisije kuondoka madarakani watoto na wajukuu zetu wakatulaumu kutokana na kupata taabu baada ya udini kuingizwa kwenye katiba” amesema.

  Mkurugenzi wa HOPD Izengo Paul amesema wakati akikabidhi msaada huo kuwa, shirika hilo linapeleka msaada huo mikoani kwa sababu walemavu wa huko wanapata taabu.

  Shirika hilo limetoa vitanda 30 vya wagonjwa, baiskeli 50, magongo 10, vyoo 10, vifaa vya kutembelea walemavu 10 na baiskeli za walemavu 20 kwa kila jimbo vikiwa na thamani ya sh milioni 58.   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Mungu ibariki tanzania
   
 3. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Watu wana fisadi makusudi na wanajulikana halafu mnamuomba Mungu!
   
 4. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Kumwomba Mungu lazima
   
Loading...