Malawi: Wananchi wataka Rais wao arudi nyumbani

Malawi: Wananchi wataka Rais wao arudi nyumbani

Mr Antidote

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2015
Posts
955
Reaction score
1,315
Wakuu hii habari iliwahi kuletwa humu ndani lakini watu wengi tulidhani ni masihara. Sasa katika pitapita zangu kwenye page ya BBC swahili nimekutana nayo hii habari.

10 Oktoba 2016

Rais Mutharika aliondoka Malawi wiki mbili zilizopita na hadi sasa hajarudi.

copyrightREUTERS

Rais Mutharika aliondoka Malawi wiki mbili zilizopita na hadi sasa hajarudi. Serikali ya Malawi imekanusha ripoti kuwa Rais wa nchi hiyo Peter Mutharika yuko mgonjwa sana nchini Marekani.

Raia wa Malawi kwenye mitandao ya kijamii wanatumia [HASHTAG]#BringBackMutharika[/HASHTAG], wakitaka Raia wao arudi nyumbani baada ya kuondoka nchini humo wiki mbili zilizopita kuhudhuria mkutano wa umoja wa mataifa mjini New York.

Serikali ilisema kuwa bwana Mutharika yuko na afya nzuri na alikuwa akikamilisha shughuli za serikali ambazo hakuwa na muda wa kuzishughulikia akiwa kwenye Umoja wa Mataifa.

Ukurasa wa serikali kwenye mtandao wa Facebook ulisema kuwa tarehe itatangwazwa ya kurudi kwa rais nchini Malawi.

Source: BBC
 
Tangia tarehe 25/09 mpaka sasa kuna utata alipo

Sitashangaa kusikia kuwa anaumwa/kalazwa au itakuwa ...........
 
ingekuwa nyumbani hata nisingesubutu kuulizia maana tayari nimechoma na huyu baba swissme.

swissme
 
Tangia tarehe 25/09 mpaka sasa kuna utata alipo

Sitashangaa kusikia kuwa anaumwa/kalazwa au itakuwa ...........
Hawa Marais wa Africa na shida zao za maradhi ni taabu sana. Nikimuangaliaga Rais wa Nigeria huwa naona huruma sana, iko shida kuubwa sana.Na huyu wa Malawi hukawii kuambiwa hali yake ni tete!!
 
Mbona wamekosa subra!
Mkuu wiki mbili bila update yoyote anafanya nini? Mfano we uage unaenda kwenye kikao cha harusi halafu mpk asubuhi hujarudi na wala hutoi taarifa we unadhani home hawatapiga simu home kukuulizia umekumbwa na nini......
 
ingekuwa nyumbani hata nisingesubutu kuulizia maana tayari nimechoma na huyu baba swissme.

swissme
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] mkuu minya kidogo huoni tuta hilo mbele
 
Mkuu wiki mbili bila update yoyote anafanya nini? Mfano we uage unaenda kwenye kikao cha harusi halafu mpk asubuhi hujarudi na wala hutoi taarifa we unadhani home hawatapiga simu home kukuulizia umekumbwa na nini......
Watu wakubwa wale, anajua anachokifanya
 
Si angetangaza tu ana tezi dume wananchi wajadiliane yeye aendelee kula pande Marekani.
 
Back
Top Bottom