Malawi to take border dispute with Tanzania to ICJ

Ni utoto kushabikia vita. Pengine inatokana na ukweli kwamba tunaamini tutashinda ila vita, kama ulivyo mpira, huwa havitabiliki. Tutajiongezea umasikini kwa kushabikia vitu vya kipuuzi. Ukweli ni kuwa vita vya bara la Afrika siku hizi siyo waafrika wenyewe wanaopigana bali ni nchi kubwa duniani zenye misimamo tofauti kimfumo wa siasa na uchumi. Kwenda mahakamani siyo mwisho wa mazangumzo kwani mahakamani ni chombo cha kuleta haki. Binafsi naamini mahakama haiweki ikatuondolea haki yetu. Naamini itatenda haki kwani hakuna rushwa kule, labda tuangushwe na wanasheria wetu na kama watatuangusha basi ni bora kwani wataingia katika orodha ya watu walioifanya Tanganyika ikapoteza sehemu iliyokuwa halali yake na hivyo kutufanya watanganyika tufikirie mara mbili kabla ya kuwaweka madarakani.
 
Mkuu kwanini ujiulizi nchi kubwa na yenye nguvu kubwa ya kijeshi kama China hawataki kukimbilia vita dhidi ya nchi ndogo sana ya Japan kwenye mzozo wa kugombea visiwa?
Mkuu Concrete ... hivi unajua unachokiongea?! .... hebu jitahidi soma kwanza kuhusu Mataifa hayo mawili ndio uje ku-comment hapa.

Japan alikuwa mkoloni wa Korea zote mbili pamoja na China.

Hivi ina maana hujui kuwa most of the coastal cities were colonized by Japan by 1942, which means Japanese control of nearly all of the major port cities. This is also where a good chunk of the population resides as well.


map-japan.gif

combined with a map of population density of today
Population_Density_2000_China.jpg
 
Sio rahisi kama unavyofikiri, jiulize kwanini DRC wanashindwa kuivamia Rwanda ambayo ni nchi ndogo sana?

Congo ina vita ya ndani itapata wapi ubavu wa kuanzisha vita na nchi nyengine? Hata kama ni ndogo?
 
Anachokifanya Banda ni kutafuta exit strategy. Ameshaona hana hoja na anajua iwapo atakubali kwa mazungumzo basi wananchi wake watamshambulia na kisiasa atakuwa kajimaliza. Sasa kilichobaki anataka apoteze kwa kesi ili aseme wameheshimu amri ya mahakama...
 
inamaana alikua hamjui baba riziwani? Masihara mengi hata kwenye mambo muhimu.
 
Ndo mana tunalipa kodi ili wale waTZ wenzetu wa LUGALO,MONDULI,MAFINGA na NGERENGERE wapate mishahara haya sasa na wenzetu nao waingie kibaruani kama sisi tunavyofanya kazi.

Inakubalika kabisa. Wanajua kuwaonea raia hapa, sasa waende wakumbane na wa size yao. Nakubaliana na wewe. Tukifikahapo eti ulinzi ni kwa kila mtanzania, ikija posho na bia za bei chee, ni kwa wao tu!! Mweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Hii issue isingelifika popote...bora wameamua kuachana na kuzunguka zunguka mbuyu kwa mazungumzo ambayo yasingezaa anything
 
Kuwa maskini ni hatari sana. Mtu fulani akija na mawazo kuwa utakuwa tajiri mkubwa sana nawe kwa sababu umesota sana unayapokea hata kama litakufanya ukosane na ndugu/jirani yako. Waingereza wanamdanganya huyo mama watampa kuwa kuna gas kiasi kadhaa na mafuta kiasi kadhaa lakini huo utajiri watauchukua wote kwa mikataba mibovu hatima yake atabakia hivyo alivyo na kuzidi na alichotegemea hatakipata.
 
hivi sasa kuna taarifa malawi inapanga kuitenga tanzania katika kundi la SADC
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom