Sasa wewe unataka kuwafundisha Tanzania ambao wamepigana vita vyao na vya wengine? usitake ncheke!
Si tu kwamba Tanzania
haina viongozi, bali pia hata wananchi wa kuongozwa hakuna. Akili matope
kabisa! Nashawishika kuamini kuwa waanzisha thread hizi na masapota
wake ni watu wenye interest na Malawi lakini si watanzania.
binafsi yule Mwanajeshi
alitudanganya sana na inapaswa afanye hvy kwan silaha za nchi ni siri ya
jeshi, ile kambi ya Gongo la Mboto sio kubwa sana kati ya Kambi kubwa
Tz. Ninaweza nikasema hata Lugaro ni kubwa sana kwa hiyo kambi ya
M/mboto.
Nimeamini Malawi ni kiboko kwa kukusanya habari za kiintelijensia hasa baada ya huu mgogoro wa mpaka maarufu kama mgogoro wa ziwa Nyasa.
Toka Lowassa, Membe na Sitta walipotangaza kuwa Tanzania iko tayari kupigana ili kulinda mipaka yake, haiishi siku bila kuona delegation mbalimbali kutoka Malawi zikiwa hapa nchini eti kuongea mara na Tume ya uchaguzi, mara bunge, n.k.
Kwa taarifa yenu kama hamjui, delegation hizi zinakuja maalum kuangalia the state of art! wanajaribu kuangalia kama kuna any movements zinazoweza kuonyesha kuwa tuko tunajiandaa kivita.
Mipangilio hiyo ambayo wanaweza kuangalia ni pamoja na bulk procurements za vyakula, mambo ya silaha na mobilization za majeshi kutoka eneo moja hadi lingine hasa kuelekea maeneo karibu na huko kwenye mgogoro.
Wakati wakiangalia hayo, wanajaribu pia kuangalia weak spots za kwetu ili kama kweli ikitokea, basi watuzime ghafla na kwa haraka zaidi.
Kwa taarifa yenu, Malawi tuwa-underestimate eti na ka nchi kadogo, hata chura alimuua tembo!
Let us be extra careful guys.
Tatizo ni kwamba watu wanataka waambiwe kila kitu.kwa taarifa yenu kuna habari ambazo hata ndani ya majeshi wanaifahamu wachache,kwa ajili tu ya usalama wa nchi,sasa nyie wamalawi mnaojaribu kuleta habari zenu hapa,jidanganyeni na malawi yenu!
Ni kweli kabisa ndugu yangu. Jumanne hii pia kuna watu wa Interpol wameingia hapa kutoka Malawi, yaani wamalawi.
check na hii ramani kutoka google earth...inaonekana tz hatuna chetu pale...ila tukomae tu huenda tukaambulia kipande japo kidogo...View attachment 61983
Ni kweli kabisa. Wanakuja kuweka mambo sawa na si ujasusi. Ujasusi gani unafanywa kishamba namna hiyo? Kwani ile brigadia ya kusini imeishiwa mpaka tuhamishe kila kitu kutoka sehemu nyingine?
kwa taarifa yenu hawa jamaa wanatumia hiyo advantage ya kuwaona washamba kupata taarifa wanazozitakana mwisho wa siku utaona kinachotokea...we jiulize, kwa nini such immediate frequent visits?
Kwahiyo tufanyaje sasa? Tuanzishe vita na Malawi? Tuwakatalie wasitutembelee kwasababu wanadai ziwa ni la kwao? Maana tusiongee bila kujua tunaongea nini. Hata sisi majasusi wetu wapo wengi tu Malawi na ujasusi unavyofanyika sio kwa staili rahisi kama hizi.
ukisoma zaidi btn lines, ktk vita ya uganda Tanzania ndiyo iliyoshindwa. Taarifa za uchunguzi wa kivita ilionesha kuwa Uganda ilikuwa na war intelgence kali zaidi, ushahidi unaonesha kuwa watanzania walipofika kampala na entebe walikuta mipango yote ya vita ya tanzania ikiwa mezani. Amini aliondoka nchini kwa kuwa wananchi wake na jeshi lake hawakumuunga mkono kwa kuwa walikuwa wamechoshwa na udikteta wake. Wamalawi wanalitaka ziwa Malawi kwa kuwa kisheria nila kwao na hawana eneo lingine lenye resources nyingi kama hili. Watanzania tungejua kupigana vita tungekuwa tulisha appeal mapema kwani si mara ya kwanza kwa malawi kutangaza kuwa ziwa ni lao. Hata tukienda mezani tuapeleka silaha gani, mtanzania hupi atatetea hoja?!, nikupe mifano inayoonesha jinsi tanzania tusivyokuwa na wazalendo khasa kwenye international arena: tulipeleka wawakilishi kule japani kuzungumzia mpango wa uvunaji wa samaki aina ya Tuna, TZ kama moja yenye tuna wengi, iliandikwa kuwa wawakilishi wetu walihongwa vidosho na kukubali mpango wa uvunaji wa tuna uliokuwa umebuniwa na walafi. Fikiria hata kisa cha ml. Kili kuingizwa ktk maajbu ya dunia, wahusika waliuchuna ili makampuni yetu ya simu yapate kipato kwa text, nchi nyingine kupiga kura ilikuwa bure na hatimaye table mountain ya S.A ikashinda. Unayaona haya?.
check na hii ramani kutoka google earth...inaonekana tz hatuna chetu pale...ila tukomae tu huenda tukaambulia kipande japo kidogo...View attachment 61983
Zomba we sema tumepigana tu na tuna uzoefu....kwa taarifa yako kwa sasa tumebaki na intelijensia ya kuwapeleka watu mabwepande, mpaka tunashtuka jamaa watakuwa wameshamchukua Vasco na kuondoka nae...
unachokisema ni ukweli mtupu na ni cha mantiki sana...kuna hali inafika hizi delegation zinaogeza majasusi ili wapate details zaidi kwa majasusi walioko ndani tayari...hivi unadhani hizi delegation zinazokuja sasa hivi kwa wingi leno ni kutuliza munkari wa tz? binafsi siamini hivo...kwa sababu wanajua tunaweza kuhack mawasiliano ya watu wao walio ndani ya nchi, ndio maana wanapenyeza watu wao ili wawape taarifa za undani za hali ilivo hapa ndani...believe or not kuna aina nyingi za kufanya intelijensia na hii ni mojawapo...
Wamalawi wako makini sana katika kuamua hatima yao. Nimesoma magazeti na blogs zao nyingi za kwao nimegundua wamalawi wengi wako against vita baina yao na sisi, na wengi wanatutambua kama majirani zao wa karibu na wa siku nyingi. Wapo walevi wachache kama i(ilivyo huku) pia wanaoshabikia vita. Nionavyo serikali yao imepima upepo na kuligundua hilo, kwamba vita kamwe haitakuwa kwa maslahi ya wamalawi wala watanzania; ndiyo maana wameamua kulipeleka suala hili mbele ya vyombo vya kisheria vya kimataifa ili kupata suluhu. Binafsi nazipongeza hatua za hivi karibuni za serikali ya Malawi kuongeza mahusiano yake na sisi na nashauri sisi pia tufanye hivyo ili kuepusha uhasama usio wa lazima uliozalishwa na historia yetu ya kutawaliwa. Wote, wamalawi na watanzania wana madai ya haki kabisa kudai kama wanavyodai; Mkoloni alikabidhi Nyasaland ramani inayoonyesha nchi hiyo kumiliki ziwa lote, kwetu alikabidhi ramani ambapo Tanzania ilionekana kumiliki nusu ya eneo la maji ya ziwa na UN baadae walithibitisha nadharia ya umilikaji wa nusu ya eneo la maji pale ambapo mipaka ya nchi inakutana na ziwa au maji. Ni kwa mantiki hayo inapaswa pande zote kuketi na kuzungumza nini kifanyike ili udugu na ushirikiano uliodumu karne nyingi uendelee. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.Really hata mm nimekuwa shocked na ujumbe uliokuja leo, eti wanakuja kujifunza uzoefu wa uchaguzi.
Why now?
Miaka mingine wanajifunziaga wapi!
Ingawa siamini kuwa intelijensi inaweza kufanywa kwa siku tatu, mimi hisia zangu zinanituma kuwa wanachofanya ktk ziara zao ni namna ya kuomba mazingira ya amani na kusihi Tanzania iachane na mpango wa vita.