Malawi imeibuka tena sakata la mpaka Ziwa Nyasa

Malawi imeibuka tena sakata la mpaka Ziwa Nyasa

emmanuel mhecha

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2015
Posts
933
Reaction score
547
Kuna habari Leo BBC Swahili Malawi wanaanzisha ule ugomvi wa mpaka kule ziwa Nyasa hivi wanatambua kwamba kwa sasa tuna Mr Presida ambaye hajaribiwi

=============================


Wengi wakisikia kuna mgogo hapa Tanzania na nchi nyingine watakuwa wanashangaa sana haswa kutokana na ukweli kwamba nchi hii ni nchi pekee ambayo haijapitia misukosuko ya mgongano wa uvunjifu wa amani tangu taifa hili lizaliwe, lakini hata historia inatuambia kuwa tumepata uhuru kwa amani kabisa bila ya kutumia bunduki mwaka 1961.

MGOGO UMEZUKA TENA

Kama ulikuwa hujui Malawi na Tanzania zilikuwa katika mgogoro tangu mwaka 1890. Mapema miaka ya sitini, Malawi ilidai umiliki wa ziwa hilo kwa kuambatana na makubaliano ya mwaka 1890 Heligoland kati ya Uingereza na Ujerumani ambayo yalisema kuwa mpaka kati ya nchi hizo uko upande wa Tanzania.
JUU NI RAMANI IKIONESHA MPAKA UNAO GOMBANIWA KATI YA MALAWI NA TANZANIA

Mgogoro huo unatoka na ziwa Nyasa ambalo kwa mujibu wa Tanzania Ziwa hilo limekatwa katikati upande Tanzania upande Malawi, lakini cha ajabu Malawi wanalitaka lote liwe lao wengi walikuja kujua mgogoro huu mwaka 2011 wakati Jakaya Kikwete akiwa madarakani jitihada zilifanyika na zilikoma sasa wameibuka tena.
Malawi wameandika barua umoja wa Afrika kwa lengo la kutatua mzozo huo ambao unaelekea kuwa mkubwa sasa kumbuka Kwa Tanzania, ziwa hilo linajulikana kama Nyasa, wakati nchini Msumbiji inajulikana kama Lago Niassa.
Mwaka 2012 Tanzania ilisema kuwa ingelinda mipaka yake hivyo kuibua hofu baina yao lakini kwa taifa letu bado liko na amani na mzozo huu utapatiwa ufumbuzi, lazima wakae chini iliipatikane suluhu iliyokuwa na mwisho.


CHANZO: BBC
 
hawa jamaa nao wangetafuta tu kazi nyngne ya kufanya.....
 
Bila kuzichapa mgogoro hauwezi ukaisha,tutakapo zichapa ndipo mazungumzo ya mezani yatakuwa na nguvu.
 
those who are with us, we will support them, and those agaist us we will defeate them..

bampami quote
05.12.2016
 
kamalawi bhana, au hakana vyanzo vingne vya mapato na utalii mpka kupgania kaziwa! anyway kwa makosa yoyote yakimipaka walaumiwe wazungu.
 
Malawi hatuna haja ya kupeleka jeshi letu la jwtz tutapeleka mgambo wa jiji wakisindikizwa na vijana wa mzee Sirro watadamka asubuhi saa kumi na mbili asubuhi hadi saa nne na nusu asubuhi tumesha iteka Malawi yote

Saa 6 kamili mchana tunaanza kubadilisha baadhi ya majina ya miji ya Malawi na tunayabatiza majina mapya!

Na rais tutamsimamisha hapo Mh: Paul Makonda huku tukisubiri mchakato wa kuitisha uchanguzi mkuu
 
Mimi naona tuhamishe mkondo wa mito yote inayoelekeza maji kwenye hilo ziwa ndio ili wapate akili nini maana ya mpaka kuwa katikati.

The same: tunaweza pia kuchimba mikondo inayohamisha maji ziwani. Watapata akili tu
 
adui tunaye humuhumu tz anaye initiate huu mzozo,lakini tusiombe tuingie katika war,nchi sahivi haiko stable economically.
 
Back
Top Bottom