MALASUSA, iokoe Junior Seminary!

MALASUSA, iokoe Junior Seminary!

Zacharia Kifyasi

Senior Member
Joined
Dec 23, 2012
Posts
135
Reaction score
24
Nimesikitishwa sana na taarifa kuwa shule ya sekondari inayomilikiwa na kanisa la KKKT ya Junior Seminanry ya mjini Morogoro imefungwa kwa mda usiojulikana! Hatua hiyo imekuja baada ya wanafunzi kugoma kwa madai ya kutoridhishwa na uongozi wa shule hiyo.
Ni wakati sasa wa Askofu Malasusa kuingilia kati suala hili kwani linatia doa Kanisa na taasisi zake!
 
Nilipata hasira sana nilipoona hii habari kwenye tv jana.
Nikajiuliza, kanisa limekosea wapi mpaka hali inafikia hapo.
Nikazidi kuona kuwa kanisa limepoteza dira,
linaanzisha miradi mingi ambayo linashindwa kuisimamia,
la sivyo ni hii ya kupeana ajira ambayo matokeo yake ni kuoneana aibu.
 
Nadhani walikosea kumwacha retired MKURUGENZI pale. kiuongozi siyo jambo mzuri kumwacha mtu aliye staafu kituo kilekile kwasababu wakati mwingine asiengependa kuona mtu aliye chukua nafasi yake akifanya positive changes angetamani mrithi wake awe conservative na awe muumini wa mambo aliyo yaasisi yeye. Aweza kuwa ndio source ya sintofahamu nyingi zinazotokea pale.Alikuwepo mkuu wa shule mmoja pale mzuri tu akafanyiwa zengwe mpaka wakamtoa.
 
JERUSALEMU mimi ni mlutheri
lakini makosa madogo madogo kama haya yananifanya nikumbuke hata makosa mengine yaliyofanyika siku za nyuma halafu yananipa hasira.

Let say: kanisa lilipofanya yubilee ya miaka 50; kwenye gazeti la kanisa walitoa ukurasa mzima ukiandika maoni ya askofu malasusa kwenye hitimisho la yubilee. ajabu ni kwamba page nzima ya gazeti askofu hakukoti hata mstari mmoja wa kwenye bibilia, alisema kidogo sana mwishoni tena akiweka maneno yaliyosemwa na mtu mwingine,

hapa nafikiria hivi kweli wanafanya kazi ya Mungu au kanisa nalo limekuwa chama cha siasa;

wamekaa ofisini hadi shule ya sekondari inafungwa kwa ajili ya migogoro, haya sasa wenzetu wakifanya mnasema
sie tumefikia huko, ni picha gani tunayoipeleka kwa jamii inayotuzunguka, na wale wasiomjua Mungu kabisa watafanyaje.

Nadhani walikosea kumwacha retired MKURUGENZI pale. kiuongozi siyo jambo mzuri kumwacha mtu aliye staafu kituo kilekile kwasababu wakati mwingine asiengependa kuona mtu aliye chukua nafasi yake akifanya positive changes angetamani mrithi wake awe conservative na awe muumini wa mambo aliyo yaasisi yeye. Aweza kuwa ndio source ya sintofahamu nyingi zinazotokea pale.Alikuwepo mkuu wa shule mmoja pale mzuri tu akafanyiwa zengwe mpaka wakamtoa.
 
Last edited by a moderator:
Tokea mwambashi alipostaafu ndio migogoro ikaanza ,huduma mbovu, mishahara duni na kufanya walimu wazuri wote kuondoka na kuleta bora walimu na pale kuna A level karibia combination zote na nahisi hawa ndio walifanya vuguvugu lote, mwaka jana waligoma tena wakataka kuchoma shule. Shule haina tena wahisani km zamani hivyo kunaitajika uongozi makini wa kuweza kuendesha shule kwa mapato binafsi chini ya dayosisi ya moro km ilovyosasa. Kila dayosisi shule za kkkt zinazorota hali ni mbaya hata ile ya kisarawe ljs.
 
nadhani something has to be done maana kadri miaka inavyozidi kwenda matokeo yanazidi kushuka...
 
Poleni, kuna muda wa kuyumba na muda wa kusimama
Nawatakia heri tu.
 
hii shule ilikua bora miaka ya nyuma, hata huyo Malasusa ni zao la shule hiyo, inasikitisha kuona ikiyumba, elimu ni jambo la kutilia mkazo wala si la kupuuza hata kidogo
 
Nina masikitiko ya kutosha kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kwa namna ambavyo limeshindwa ku handle mgogoro wa Junior Seminary Morogoro kufikia hatua ya kuwarudisha nyumbani wanafunzi wote baada ya mgomo wa kutaka uongozi wa shule hiyo ubadilishwe. Madai ya wanafunzi hayakupewa nafasi ya kusikilizwa licha ya kwamba ni mara ya pili kuzuka mgogoro shuleni hapo.

Kwanini nasema ni aibu TUPU kwa KKKT; Kwanza naamini kabisa kuwa waumini walio wengi wanapeleka wanafunzi wao katika shule zinazoongozwa na Kanisa la Roman Catholic. Ambazo zilizo nyingi zinaongoza kwa kufanya vizuri katika masomo pia wana uongozi mahiiri wa usimamizi wa shule zao.Licha ya kwamba zinaongozwa na mashirika ya Kikanisa lakini msingi wake ni mmoja tu MAADILI MEMA.

Swali langu kwa Kanisa la Kilutheri kwanini shule zake hazifanyi vizuri ukilinganisha na Roman? Na Je uongozi wa juu hawaoni haja kubwa kutilia maanani ELIMU kwanza kuliko hata ujenzi wa mahekalu na vitega uchumi ? Ambvyo wame excel kwenye kukusaya michango?

Sina nia ya kulaumu KANISA bali uongozi wa juu unapaswa kutilia maanani zaidi katika kuimarisha shule zake zilizopo hata na kuanzisha zingine nzuri zaidi ili kuleta ufanisi zaidi.

Najaribu kuelewa kuwa migogorop mingi kwenye shule zetu hasa ni upungufu wa mahitaji ya msingi,kama vile Uongozi usio kidhi matakwa ya Elimu,maadili mema,miundombinu nk nk.
Najisikia aibu sana mimi mwenyewe nikiwa muumini wa Kanisa hilo pale naenda kupanga foleni katika shule za Roman Catholic kupata nafasi ya mtoto ili hali sisi tunao uwezo wa kuboresha shule zetu na hata kushindana na hawa wenzetu,Tena basi kwa mtizamo huo huo naliona KKKT kama lina wasomi wengi wazuri na viongozi wenye upeo mpana sana.Je hili la Elimu linatupigaje chenga?
Jana watoto walirudishwa majumbani wakiwa wengine hawana hata nauli ya kurudi makwao wala mawasiliano na wazazi wao, kwani wametoka likizo siku si nyingi tuu.Mheshimiwa Baba Askofu Dr.Alex Gehaz Malasusa angalia jambo hili kwa makini kanisa lina matarajio mengi sana kwako katika hili. UBARIKIWE NA BWANA.
 
Malasusa ni mwelewa. Kiongozi makini mpeni mda.
Hizi habari zishasikika
 
Malasusa hebu sikiliza kilio cha Kondoo wako....Nimeikumbuka Agape Seminary na St. Dorcas zote za Kilimanjaro shule hizi zipo imara sana....
 
Nadhani walikosea kumwacha retired MKURUGENZI pale. kiuongozi siyo jambo mzuri kumwacha mtu aliye staafu kituo kilekile kwasababu wakati mwingine asiengependa kuona mtu aliye chukua nafasi yake akifanya positive changes angetamani mrithi wake awe conservative na awe muumini wa mambo aliyo yaasisi yeye. Aweza kuwa ndio source ya sintofahamu nyingi zinazotokea pale.Alikuwepo mkuu wa shule mmoja pale mzuri tu akafanyiwa zengwe mpaka wakamtoa.
. Mwambashi baada ya kustaafu alibaki pale pale. Mkuu wa shule unayemsema alifanyiwa zengwe ni Merisali?
 
Je, wakurugenzi wa Elimu wapo wapi? Je, shule ina miradi ya kujiendesha? Kwa mwendo wa MAPATO, MATUMIZI NA FAIDA huwezi kufika mbali hata siku moja.
Ushauri kwa kanisa husika: kuangalia mfumo wa madaraka, Mhusika wa Elimu secondary/ Msingi/ vyuo wanapaswa wawe karibu na sehemu mahalia. mf. shule ipo morogoro mhusika yupo Arusha, ni sawa kweli? anafanya kusubiriwa aje! Ina maana inashindikana kumweka/kumpata msaidizi kutoka hapo Morogoro?

Mwisho:Linapotokea tatizo kama hili ktk shule si lazima kuwapa wanafunzi kile wanachotaka hapohapo, unaweza kutumia hata saikolojia tu kuweza kuwatuliza.Na kuwaeleza kwa kina jinsi hali ya fedha ilivyo shuleni.
Kuendesha shule si kazi ndogo hata kidogo inahitaji moyo wa kujituma na ukaribu wa viongozi wa juu hasa kama ni ya Taasisi.
cop.ULUMI, Zacharia Kifyasi
 
baada ya mwambashi kuondoka,shule ilipata mkurugrnzi mzuri sana ambae kiukweli alikua na vision alikua ni Rev Dr Fihavango...lakini baada ya dayosisi yake kumchukua kwenda kuwa msaidizi wa askofu huko,shule imekua ikiyumba kila idara
 
Shule hii ilishawahi kuwa kwenye top ten bora miaka ya nyuma. watoto waliosoma hapo walikuwa wazuri darasani na kwenye jamii waliyorudi. nilitamani kuwapeleka watoto wangu kusoma hapo lakini nilishindwa taratibu zake. kanisa halikuwa na nia mbaya kuwa na mradi wa shule zetu za sekondari. ila tunapaswa kujitahidi kupata huduma muhimu za kuendesha shule na kuifanya ionekane ni shule tofauti na nyingine. waalimu bora na wenye malezi mema na mahitaji yote yanayofaa kwa wanafunzi tena vijana. Ikiwa vijana hawa wamedai haki yao na huduma muhimu shule inayoendana na ada yao kulikuwa na haja gani ya kuwafukuza yaani kuwafungia shule? Vijana hawa ndio mnaowategemea kesho na siku zijazo kuwa taa ya kanisa na jamii kwa ujumla. Ninaomba Baba Askoffu Malasusa uwasikilize Vijana na Uwapatie haki yao ya Elimu inayoendana na Ada yao. Niliwaona Channel Ten nikaumia sana kwa jinsi wanavyolalamika. Walivaa Uniform zao na walipendeza. Plse usituangushe Askofu. Kuna Waalimu wengi tuu wazuri wangependa kufundisha shule hiyo ikiwa watalipwa vizuri na kuheshimiwa.
 
. Mwambashi baada ya kustaafu alibaki pale pale. Mkuu wa shule unayemsema alifanyiwa zengwe ni Merisali?

Kuna bwana mmoja anaitwa MR malekela, ukiondoa mapungufu madogomadogo alikuwa ni mtu mwenye malengo na mchapa kazi. kwasasa sijui yuko wapi.mimi nilifanya nae kazi zamani kidogo wakati huo alikuwa IRINGA GIRLS.
 
  • Thanks
Reactions: mka
Malasusa hebu sikiliza kilio cha Kondoo wako....Nimeikumbuka Agape Seminary na St. Dorcas zote za Kilimanjaro shule hizi zipo imara sana....

unajua maana ya seminary au ni kusema tu kama ka mtindo?
 
Back
Top Bottom