MALALAMIKO YANGU KWA KAMPUNI YA SASATEL (www.sasatel.co.tz)

Godlisten Masawe

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
738
283
Mimi ni mteja wenu toka mwaka 2011, ofisi yangu inategemea internet yenu. Tokea mwanzoni mwa mwaka huu 2013 uanze internet yeni imekuwa siyo reliable, kuna kipindi nakosa internet siku nzima au pengine hadi siku mbili, ukiuliza sababu mnadai kuna itirafu ktk mitambo, kibaya zaidi leo naitaji internet napiga namba ya customer care toka asubuhi mpaka sasa haipokelewi, kupiga namba ya customer care na kutokupokelewa siyo leo tu, ni tabia inayojirudia rudia.
 
Sasatel imefilisika si utafute provider mwingine?unawakomalia hao wameshafulia!!
 
hawa jamaa ni wababaishaji ile mbaya, mimi nimewahama
 
Daaaaah Tanzania mpaka makampun ni ya kijanja janja!!!!
Mbwembwe zote zile now wapo
Chaliiiiii..........duuuuuuuuuuuuh
 
Tangu nilipoona bandiko humu kuwa Sasatel imeanza kufilisika niliwahama mazima.... Kwanza kupata tu vocha zao ni ishu!
 
Breaking News:Sasatel yafa Rasmi.
Noma sana kuna mshikaji flani namjua aliacha kazi kwa mbwembwe akaenda Sasatel nadhani na yeye atakuwa anapumulia mashine,vijana wengi wanapenda sana maendeleo ya harakaharaka yakija makampuni mapya anakimbilia tu bila kutafakari anaacha sehemu aliyekuwepo miaka miwili anaenda kwenye kampuni ambayo haijui ina background gani anatema Big G kwa karanga za kuonjeshwa,Kuna kampuni ilikuja miaka ya 2008 inaitwa Hits Tanzania kampuni ya simu ilikuwa na prefix 0741xxxxxx ilinyang'anya wafanyakazi wengi kutoka kampuni za simu watu walikimbilia kisa walikuwa wanaenda kulipwa $3000 wakaacha kazi za huku walipokuwa wanalipwa 1.3m baada ya miezi mi3 wakakumbana na mtikisiko wa uchumi kampuni ikafa wakaanza kuemea mashine ahmad wengine wakapata zari wakaenda Equatorial Guine ndio ikawa manusura otherwise ilikuwa aibu maana walikuwa wamekaa miezi mi3 bila mshaara ikabidi wengine wakaanza kuuza magari yao haya makampuni mapya yanayokuja ni majanga sio mazuri kukimbilia...RIP sasatel
 
Daaaaah Tanzania mpaka makampun ni ya kijanja janja!!!!
Mbwembwe zote zile now wapo
Chaliiiiii..........duuuuuuuuuuuuh

Halafu unakuta wamamualika waziri wa mawasiliano kama mgeni rasmi kwenye uzinduzi kumbe...........!
 
cdma technology imewaangusha,

angalia hata mobile cdma za ttcl nazo chali,

zantel ndio mjanja pekee ana mix cdma na gsm,

huwa najiuliza ttcl kuna vilaza kiasi gani why na wao wasingemix ??!!!
 
Back
Top Bottom