Malalamiko ya watumishi juu ya Utawala wa miaka mitano

Kasegela

Senior Member
Mar 24, 2019
127
261
1. Hakuna nyongeza ya kila mwaka tangu mwaka 2015

2. Hakuna Nyongeza ya mshahara.

3. Muda wa Kupanda madaraja umeongezwa kutoka miaka 3 ya sheria aliyoacha Kikwete hadi miaka 4.

4. Madaraja ya watumishi kwa sasa imekuwa mbinde mpaka uwe na ndugu Tamisemi (Connection)

5. Watumishi wakistaafu kwa sasa zaidi ya nusu wanakufa bila kulipwa kiinua mgongo chao,wanaishi kwa madeni na stress mpaka wanakufa kwa kihoro.

6. Watumishi waliwekea Kikokotoo cha Kinyonyaji mpaka baadhi wakaanza kufa baada ya kupewa fedha kichele kwa madai kuwa Kikokotoo kimeboreshwa.hata hivyo Magufuli allkirudi aliahidi kukirudisha 2023 na ndio maana sasa kila mtumishi anafoji vyeti vya ugonjwa ili astaafu kabla ya kikokotoo Kipya endapo Magufuli atarudi Madarakani(Jiandaeni kufa maskini)

7. Watumishi wanadhalilishwa na wanasiasa mbele ya camera na familia zao zinawaona wanavyodhalilishwa.

8. Hakuna mtumishi anaefanya kazi tena kwa kujiamini,kila mmoja haitambui kesho yake.

9. Watumishi waliojiendeleza kwa kupata mkopo bodi ya Mikopo serikali hii ilivunja mkataba wa kulioa rejesho la asilimia 8 lililoachwa na Kikwete na kuweka rejesho la 15% ,sasa watumishi wana mishahara ya laki mbili halafu naisha ndio haya ya Kg ya sukari 2800.

Uchaguzi umefika, watumishi ndio wasimamizi wa uchaguzi, kazi kwenu kuweka mtawala atakaewasikiliza au atakae zidisha mateso yenu.

Wenye vyeo na mishahara mikubwa wasiwaponze ninyi wenye mishahara iliyosheni mikopo.

Hatima ya maslahi yenu ipo mikononi mwenu,mimi nimefikisha ujumbe.
 
Magufuli huwaga anafurahi sana pale anapoona wengine wanataabika. Hiyo ndiyo hulka yake.

Kwa hiyo, watumishi msitarajie neema hata kwa miaka mingine mitano kama hiki kiumbe mtakichagua tena.

Dawa yake ni kumnyima kura tu.

brother brother polee
 
We bwege mlivyo ambiwa kila mtu ataguswa hamkuelewa sasa hivi ndio mnajifanya kushtuka!

Kila mtu nani sasa! Tatizo la Watanzania wa aina kama yako ni kusumbuliwa tu na magonjwa ya kutokujiamini na kukaririshwa! Huwezi ukawaweka Watumishi wote wa umma kwenye kundi moja la kutokujitambua!!

Ungekuwa una akili timamu, ungegundua mapema tu ya kwamba hao hao watumishi wa umma unaowaponda bila ushahidi wowote, ndiyo hao hao wengi wao nikiwemo Mimi, tulichagua mabadiliko mwaka 2015! kitu ambacho kimechangia pakubwa kumfanya huyo magufuli kujenga bifu la chini kwa chini dhidi yetu.

Punguza wivu na chuki dhidi ya watumishi wa umma! Na pia usiwe kama kasuku. Kila unachoambiwa na kusikia, unakiamini na kukisemea hadharani. Vingine ni vya kufikirika.

Magufuli anapendwa na wanafiki. Hayupo mtumishi wa umma mwenye akili timamu, anaweza kumkubali magufuli.
 
Kila mtu nani sasa! Tatizo la Watanzania wa aina kama yako ni kusumbuliwa tu na magonjwa ya kutokujiamini na kukaririshwa! Huwezi ukawaweka Watumishi wote wa umma kwenye kundi moja LA kutokujitambua!!

Ungekuwa una akili timamu, ungegundua mapema tu ya kwamba hao hao watumishi wa umma unaowaponda bila ushahidi wowote, ndiyo hao hao wengi wao nikiwemo Mimi, tulichagua mabadiliko mwaka 2015! kitu ambacho kimechangia pakubwa kumfanya huyo magufuli kujenga bifu la chini kwa chini dhidi yetu.

Punguza wivu na chuki dhidi ya watumishi wa umma! Na pia usiwe kama kasuku. Kila unachoambiwa na kusikia, unakiamini na kukisemea hadharani. Vingine ni vya kufikirika.

Magufuli anapendwa na wanafiki. Hayupo mtumishi wa umma mwenye akili timamu, anaweza kumkubali magufuli.

Endeleeni kujipa moyo! Ninachoamini Magu ndiye atakatangazwa kushinda urais hata kama hukumchagua!

Sio rahisi kiihivyo mnavyofikiria ccm kukabidhi madaraka upinzani pasipo katiba ya wananchi, kwa sasa itakuwa bora kwa ccm kuona damu inamwagika kwa wasiojua katiba tuliyonayo maana ndio watakaoonekana wavunjifu wa amani!
 
Ushenzi huu unakubalika Afrika tu.
 
Hongera mkuu umeandika kweli kweli tupu...watumishi saizi wanaishi kama wakimbizi hawana hakika ya kesho
 
Mimi huwa nawashangaa kweli mnaolalamika mitandaoni kuhusu nyongeza ya mishahara na kupanda vyeo. Napenda kusema hivi kupanda cheo sio automatic inategemea ujuzi, weledi, bidii, uaminifu n.k kuhusu ajira hii ni siri kati ya mwajiri na mwajiriwa kama upande mmoja hauridhiki unavunja mkataba. Sasa kama ndugu yangu hujaridhika na unachopata acha kazi alafu uone maelfu wtakaonga'nga'nia nafasi yako acha kutisha mwajiri ndugu yangu ata mimi pia nipo standby uache hiyo nafasi nije kuiziba.
 
Hujui kitu wewe.
 
Back
Top Bottom