Malalamiko ya wanawake JF Too Much

Selwa

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
543
524
wakuu habari zenu...... nimeona nianze thread upya badala ya kujibu kila thread nayoiona, mbona malalamiko ya wanawake JF yamezidi? Mara wanawake akili sawa, mara wanawake hiki wanawake kile wanawake hawana akili wanawake hawafai...mabrooo mnakosea wapi?

Me nipo mbioni kuoa mwezi ujao na najua unajisikiaje baada ya kutendwa...kila mwanamke unamwona taka taka ila tusifanye hivo wakuu tunamkosea sana hata Muumba wetu. Hiyo stage ya frustration inapita kwetu sote ila usirushe lawama kwa wanawake wote. Mimi personally sipendi kusikia statements kama 'men are trash' au 'wanawake wana akili sawa' najua nikisikia statement kama hii kutoka mabroo kuna demu kachomoa moyo wa mtu apo nimeamua leo kutoa tips kwa mabroo ili malalamiko yaishe na uhakika atatokea mwanamke pia kutoa tips ile wanawake nao waache kulalamika
ukiwa unatafuta long termn uhusuiano au hutaki wanawake mbofu mbofu fanya hivi.

1. Tafuta hela brooo yani saka hela tena isake kiukweli kweli si masihara...mahusiano ni very expensive hiki ni kitu wazazi wetu hawatuambi but women are expensive na huwezi kimbia hii expense kama unataka mahusiano na mtu anaejielewa. itabidi siku moja moja muende lunch...dinner hasa miezi ya kwanza, ukishamsoma mnaweza enda hata rose garden hahaha ila miezi ya kwanza show mwanamke wako class so usifikirie kutafuta mwanamke kama bado hujatafuta hela utakuwa unajiumiza wewe mwenyewe. (wanawake wanataka uhakika wa security, kwamba akizaa na wewe leo kuna pesa ya mtoto kwenda shule nzuri na kupata chakula kila siku, kama hauna hii usihangaike kutafute mwenza kwanza tafuta pesa maana kila utaempata atakuacha ) Na sio kwamba wanawake wanaangalia hela tu hapana ila wanapenda mambo mazuri mazuri na mtu ambae atafanya juu chini kumuimpress, mwanamke ambae siku ya kwanza unamtoa out anakubali kwenda sehemu ya ajabu sio mwanamke ataekufaa trust me.. huyo mwanamke hatakufanya upige hatua maana hana high expetions of u wala high ambitions lakini katika hili kuwa makini pia...usiende kwa mwanamke ambae huwezi kummudu. Mzuri ana shepu ila kila siku anataka kula serena tupa kule. Wengi wetu pesa zikitutembelea tunataka mwanamke mwenye lacewig iphone 7 viatu laki3...kama ana kazi na anajimudu na unammudu kwa gharama zake sawa. Kama hana kazi na ana vitu vya gharama na brevis lako kimbia..hizo gharama very soon zitakuwa zako. angalia mwanamke ambae yuko katika price range yako na ambae anauwezo wa kujihudumia. Ukitetereka kwa hawa wadada wa mjini ndugu yangu ukiwa hauna hela anasepa vizuri tu. We mwanamke hana kazi ana lacewig laki 3 anatoa wapi hela. Muulize dogo janja ndoa ipo wapi sasa. usijitafutie headache...hao wazuri kuwaangalia tu . Mwanamke anatafuta security kwamba ata leo akizaa na wewe watoto mnaweza wapeleka shule nzuri. Kuna pesa ya kule. I u cannot provide wen a man who can walks by she will def walk by him. Tusake tonge

2. Mpime mtu ulienae, sio unajitoa mpaka senti ya mwisho ye anakunulia boxa zawadi. Nenda kwa speed yake. Kama yeye anakuhudumia anakupikia anakupa vizawadi vidogo vidogo na wewe fanya vivyo hivyo. usijitoe kwa mwanamke ambae hajitoi kwako

3. epuka wanawake ambao kila siku wana shida. Kimbia. usiangalie nyuma. atakufilisi huyo. Mwanamke akiwa anakupenda hatakuambia shida zake..utaziona wewe mwenyewe na utaamua kumsaidia kwa kiwango chako na sio lazima kifedha hata mpe mawazo ya kuyachanganua. Hivi mmesikia interview ya Nandy kuhusu Boss Ruge? Demu kajenga nyumba kamaliza Ruge hajatoa hata senti alikuwa anamtafuta show anapiga kazi anapta hela anajenga...ebu tuache haya mambo ya kusomesha watoto wa watu kumbe tunaliwa kama unataka kumsomesha muoe kabisa huyo. Nina washkaji wamelia sana kusomesha mademu zao usidondoke kwa hio trap mkuu.

4. Soma vitabu uweze zibua vizuri huo mdomo wa chini hahahah sijui kwanini wengi hatupendi soma unajua hayo mambo ndio yanamtuliza mwanamke yani dah..ukijua kumzibua mdomo wa chini mdomo wa juu unaachaga kelele

5. Usipende mwanamke mvivu anaetaka kukaa ndani ..broo utalia. Tafuta mwanamke mchakarikaji mambo magumu sa hivi kuishi na mtu anakutegemea kwa sukari hadi chumvi utachanganyikiwa

6. Mwanamke ambae anapenda sana vitu ambavyo havimlipi huyo hakufai... kama anashinda mitandao sijui facebook insta na haimlipi achana na huyo..anashinda kwenye mambo ya udaku...achana nae .. hamna mwanamke ataekupotezea muda kama mwanamke ambae haogopi kupoteza muda.

7. Hii ni serious..mwanamke ambae hana hofu ya Mungu HAKUFAI. simaanishi utafute mlokole au swala tano hapana. pima hofu ya Mungu kwake. Wengine wanajificha makanisani kumbe wana makucha mfuatilie nyendo zake kama anaenda kweli bible study makanisani..mpime. Mwambie akufundishe na wewe biblia akufundishe anachojifunza utajua tu kama ni feki au la

8. Broo sali aise. Me nilivoanza kutafute Mke nilienda kwa mchungaji wangu tukaomba kila mwanamke nikawa namsimulia aise. Dunia imebadilika sana..siku tena ukiwa na mafanikio madogo anajitwisha mimba au utaishia endewa kwa mganga. Sali sana upate mwanamke sahihi usiende mwenyewe kwa akili yako wanawake wanaoumiza watu wako wengi sana

9. Hili la mwisho ni muhimu kuliko lote. SAMEHE WANAWAKE WOTE WALIOKUUMIZA NA OMBA MSAMAHA KWA WOTE ULIOWAUMIZA. Hutopata mtu yeyote sahihi mpaka ufanye hilo. Maisha yanachekesha sana aise ..kila unaemuumiza anakuzibia riziki na kila hasira au kinyongo ulionayo juu ya waliokuumiza itakufanya ushindwe kuhudumia penzi jipya amini hilo, kuna mambo mambo nilifanya ujanani athari zake naziona ukubwani muda ingine unahisi kama ndoto ila niamini mimi hamna kitu kibaya kama kuchezea hisia za mtu utajutia tu... na wanawake hii ina-apply kwenu pia usithubutu chezea hisia za mtu Mungu mkali sana..msione vijana wanashinda humu kutukana wanawake wana maumivu yasiosimulika.

10. Kwa ataeona mwanga kwa haya ani-PM kwa mrejesho...
11. Wahenga wazoefu wa haya mambo rushieni points kwa chini tuwasidia mabroo zetu aise hali ni mbaya hali ni tete idadi ya wanaume wanaojinyonga imeongezeka Tanzania...sababu ya kwanza wa hili ni magufuli ya pili ni wanawake ebu tuokoe jahazi
 
Back
Top Bottom