Malalamiko kuhusu uongozi wa NSSF

Ila hii km ina kaukweli fulani hivi. Manake pale bhana Menejimenti yote ni ile iliyokuwa ya PPF. Erio kachukua akina yes yes tu. Hata hivyo msijali kama sio yule mama Mhagma na Mkapa tayari mbona angeshatumbuliwa Erio. Siku zake Erio zinahesabika.
 
Nimewafuatilia sana Wadau kwenye changizo zenu lakini bado nashindwa kuelewa hapa lengo lenu ni kumu attack mtu, kuusaidia Mfuko mkongwe kabisa wa NSSF unaotunza michango yetu ama lengo lenu ni nini hasa maana ninavyofahamu mimi hapa ni uwanja wa kutoa mawazo yenye tija na sio vijembe, majungu na chuki binafsi yaaani na kerwa mnoo na watu wa JF wenye mlengo huo ....mara ooooh mama Mhagama oooh Erio ....mimi ningetarajia mtu aje atoe wasifu wa mama Mhagama jinsi alivyo mama mpambanaji na jinsi alivyosimamia taasisi za Hifadhi ya Jamii, mimi nilitarajia mtatoa maelezo jinsi alivyosimamia bungeni pamoja na vyama vya wafanyakazi mpaka mifuko iliyokuwa luuuuki ikabaki miwili tu na si hivyo tu huyu huyu mama Mhagama mnayemsema ndiye mwanamke mahiri mwenye uweledi katika kazi yake hebu tuweke ubinafsi pembeni tuangalie maslahi mapana ya Taifa na si kuwa vibaraka wa watu au mtu kwani haujengi zaidi unabomoa na kupotosha umma wa Tz

Huyu Erio mnayemsema ningewaelewa mngekuja na namba za jinsi gani kaiangusha hiyo NSSF nijuavyo Mimi pamoja na kwamba nimejiajiri lakini najua vile ambavyo siku hizi huwezi ukaenda pale ukapewa mchango ambao hauna kibali au eti unapangana na baadhi ya wafanyakazi ili mgawane hela yaaani nasikia sikku hizi ule uhuni uhuni wa kupiga deal pale haupo hivyo najua Erio hawezi kukwepa hizo chuki na najua hata kwa waganga wenzangu na Mimi mnaenda hahhhahha....hali kwa kweli ni tete kwa wale mliozoa pesa za chap chap.
Pale sasa ni mifumo tu mianya ya uvujaji wa mapato hakuna. Hale kazi tu
Ila hii km ina kaukweli fulani hivi. Manake pale bhana Menejimenti yote ni ile iliyokuwa ya PPF. Erio kachukua akina yes yes tu. Hata hivyo msijali kama sio yule mama Mhagma na Mkapa tayari mbona angeshatumbuliwa Erio. Siku zake Erio zinahesabika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Erio sio kiongozi anaishi kiujanja ujanja tu. Hajiamini na ndio maana anafikiri kufanya kazi na watu aliokuja nao tu.

Na mara nyingi atekelezi maagizo ya viongozi wa juu. Ameacha DEGE vimeibiwa vitu ambavyo basically na mali ya NSSF.

Raisi ajamjua huyu mtu ni hatarii. Anaficha mambo yake mabaya na kuonyesha msafi.
 
Maskini vilaza wangu haoooo unaleta udini kwenye kazi....eti Ndalichako kavuruga wizara ya elimu na wewe umevuruga wizara yako ya majungu, chuki na uzandiki ...hovyo kabisa wewe jamaa

Kuna mtu ana ujasiri wa kuwagusa Wanawake MAHIRI kama Mhagama na Ndalichako ...? Hivi macho yako yanaona kama yangu nauliza tena hivi kuna mtu ANATESEKA na jinsi Wanawake wa shoka hawa wanavyosimamia wizara hizi nyeti zenye maslahi mapana ya Taifa....?

Nani asimame aniambie kama ufaulu haujapanda nani asimame aniambie ikiwa siku hizi Kuna wanafunzi Wanaandamana kwa ajili ya MIKOPO??? Nani asimapme NANIII NAULIZA???? Kudadekii hebu tuache majungu wakubwa kila mtu ageukie shughuli yake ya msingi kuliko kufanya bla bla bla
Wakristo. Mmmmmmmmmmmhh hata ndalichako kavuruga wazara ya elimu

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee baba hivi uko timamu kweli mtu mwenye uweledi hata siku moja huwezi kumweka kwenye kundi la eti "anaishi kiujanja" hao wanaoishi kiujanja kiujanja kama ulivyosema ni wale wanaoitwa 'misheni town' yaaani unawezaje kumuweka kundi hilo Mzee baba...eti hajiamini hebu tutumie tu hata akili za kuzaliwa maana najua za darasani ndio hivo tena nimekwama nimekuwa nawafuatilia sana hawa wakuu wa Taasisi huyu jamaa Erio ni mtu jasiri na mwenye kujiamini tena akiielezea Hifadhi ya Jamii utapenda aendelee nilishawahi kuudhuria kongamano fulani basi alikuwa anaongea utasema Hifadhi ya Jamii kazaliwa nayo

Kwa taarifa yenu huyu jamaa Erio hafanyi kazi na mtu asiye na msimamo, sasa naona mshikaji pale juu anasema watu wa yes yes, yes....mimi nitatuma intelejinsia yangu nipate kujua hapo kina yes yes wamefanya nini na kwa kiasi gani.
Halafu na wewe utumie intelejinsia yako kuhakikisha data hazijapikwa au la.
Sisi watanzania tumezoea majungu kwa watenda kazi.
Ila hii km ina kaukweli fulani hivi. Manake pale bhana Menejimenti yote ni ile iliyokuwa ya PPF. Erio kachukua akina yes yes tu. Hata hivyo msijali kama sio yule mama Mhagma na Mkapa tayari mbona angeshatumbuliwa Erio. Siku zake Erio zinahesabika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi wandugu hii issue ya Dege bila kumung'unya maneno inatakiwa ifanyike intelejinsia yenye akili kwani Erio hayupo kabisa katika movie waliohusika hamuwataji ...hebu acheni uzandiki wenu tuwe huru tusiwe watu wa kutumika na kutamka kauli nzito zisizo na chembe ya ukweli kwani unawezaje kusema Erio kamdanganya Rais wakati hata kwenye movie hayupo ....hebu tujitathmini halafu turudi huku JF tuandike taarifa zenye kuleta maana kwetu sote na sio kujibu tu "
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeandika kweli - lakini je ni sahihi alichofanya kuhamishia watu wake wote wa PPF kwenye Mfuko wa NSSF? Halafu pia ina maana wale wa NSSF aliowasambaratishia kule Halmshauri ni kweli walikuwa wakosaji tu?
 
Too low
 
Team Elio ndio nini?Haya sio majungu ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
poleni sana wazee wa vitengo huko NSSF sema bandiko lako nimelisoma nikagundua matatizo kadhaa ya msingi ambayo umekwepa kwepa kuyaweka bayana ngoja nidadafue uhalisi huo mana hata kichwa cha uzi kilipaswa kuwa NSSF SASA WATUMISHI NJAA KALI
-sababu za msingi naliona kwenye kulia lia kwako ukijifichia kwenye kimvuli cha ufanisi wa kazi na kuukwepa ukweli wa ulaji umekuwa unasuasua kwa sasa kama mlivyozoea hapo kabla KUPIGA MIPIGO (labda sasa keki inatafunwa na wateule wacheche).
-kilicho nisikitisha zaidi ni kwa watumishi wa umaa wa ofisi moja kulalama kutotaka kupelekwa ofisi nyingine yani unapingana na mwajiri wako ambaye ni serikali ana maamuzi ya kimkakati kwa sababu zake atazo ziona kukupeleka popte hata huko halmashauri (mnapo paogopa sana nyie wazee wa kupiga mamilioni kwenye hayo mataasisi 😂)
hili nimeliona bayana kwa kauli zako mwenyewe kama navyo zianisha hapo chini:
1.)Kutishia kuhamisha wafanyakazi kwenda halmashauri. Hili amekuwa akitamba waziwazi kwamba anaweza akahamisha staff yeyote kwenda halmashauri (mkuu hata hao waliopo huko halmashauri elimu hizo hizo ufanisi huo huo na wanahamu ya viyoyozi juu ya mijengo ya ghorofa ofisi za umma nikupeana nafasi tu pale majukumu yakilazimisha iwe hivyo)

2.)Huduma mbovu si kwa wateja wa nje tu bali hata kwa wafanyakazi. Imekuwa ni jambo la kawaida mfanyakazi kusafiri kikazi bila kulipwa masurufu ya safari kwa wakati, mfanyakazi anaweza akalipwa hata baada ya siku kumi au zaidi toka kumaliza safari ya kikazi.( Poleni sana sema siamini hii ni huruma kwa wateja wa nje mana uzi ungeshakujaga hata miaka 5 iliyopita, hapa mzee baba nihayo malipo yenu tu ya safari ya kikazi kukawia ndo msisimko wa huu uzi wako)

3.) Sasa hivi ni kitu cha kawaida kwa gari la shirika kupaki kwa mwezi mzima eti matairi yameisha, fedha zipo ila ‘wafalme” wa makao makuu wako busy na mambo mengine. Ni aibu na kurudisha nyuma taifa.(unaona hahahaha PESA)

4.) Sasa hivi ni jambo la kawaida japo ni aibu ofisi za NSSF, kukatiwa maji, kukosa/kukatiwa umeme.( kichaka cha kufichia hoja ila dhumuni ni lile lile ukata pesa za posho tu.)

5.) Tembelea ofisi za NSSF hali ni mbaya wanashindwa hata kufanya matengenezo ya vitu vidogo kama vitasa, fedha zipo ila “wafalme” wamejifungia makao makuu na kutengeneza gap kwa kutotoa, miongozo inayoeleweka( hahaha as usual ni tatizo PESAAAAAA , Dah sema vijana lazima mkubali dhama zinabadilika na mbadili pia mazoea ya maisha mliyoishi ndani ya hizo taasisi mzoee tu hali)

....HITIMISHO: Umeongea vitu vingi na lawama kubwa kwa wakuu wenu wa kazi hizo changamoto zipo tu mashirika yoyote yale hata binafsi haswa mabadiliko ya kiungozi yakitokea na yakashindwa wiana na mahitaji ya aina ya maisha mliyowahi yazoea sijaona cha ajabu sana ila ajabu niliyoiona ni kupiga uchochezi wenu hadi kwa mh. Rais kisa mtimize ndoto za maisha yenu ya kale mliyo yazoea 😂😂😂😂 ( haya bhana alamsiki.)
 
Hahahahaha,mianya imebanwa siyo?Bata zimepungua na heshima mtaani imeshuka.Hela za pango nazo issue,inabidi ahamie Tandale kwa Mfuga Umbwa.

Michepuko nayo inadai pango na matumizi inakuta holaaa.Wavumilie tu vijana,kila zama na wakati wake,sio lazima waishi kifahari kama enzi zile,wabadili mifumo wa maisha kuendana na tone za muziki kwani hakuna za bure na michongo ya kiboni town kama zamani.

Kwani halimashauri wanaofanya kazi huko sio watumishi wa Serikali?Wanapadharau huko?

Yaani Bw.Erio changamka upesi uwahamishie huko maana wanaleta dharau utadhani waliandikiwa katika utumishi wao wa umma watafanya NSSF na makao Makuu tu.Hawajui sasa hivi mwajiri ana uamuzi wa kukupeleka kokote anapoona kuna uhitaji?.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaonyesha unaandika tu kishabiki kwa kuwa ulishajikatia tamaa tokana na kumezwa na mazingira uliyopo. Hovyo kabisaa! Mie pamoja na kujiajiria mwenyewe lkn naona yanayofanyika sio kabisa. Ndugu yangu amestaafu tangu Julai Mwaka jana hivi ninavyoandika hajapata hata pensheni yake Mfuko huo mpya. Erio sio kuwa ananyanyasa wale wafanyakazi wa NSSF tu, Erio ndiye mwaribifu wa kwanza wa sekta ya pensheni. Erio aliuharibu sana Mfuko wa PPF, Erio huyu kamshauri Rais kuhamisha wafanyakazi kutoka Mifuko mingine ili wapelekwe NSSF ili aue kabisa Mfuko Mpya. Erio huyo huyo amemshauri vibaya Rais na kumpigia debe Mashimba (pot wa Magu) awe CEO wa Mfuko mpya ili waweze kuficha taarifa kuwa Mfuko huo upo na hali nzuri wkt ukweli unaonesha Mfuko upo hoi bin taabani. Ingekuwa Erio hanufaiki na nafasi yake ingekuwa sawa - ndugu ongea na wafanyakazi wa Mifuko yote miwili kilio ni Erio tu. Endekeza ushabiki wa kisiasa ila subiri wastaafu watakapoanza kuandamana ndipo itajulikana nani ameharibu sekta ya pensheni!
 
Yani we jamaa kilaza kweli maana unaonekana ni mmoja wa waliokaziwa ulaji
maana mawazo yako yamekaa ka una ishu personal sana acha uzuzu arifeee. Sasa jamaa amenyanyasa au amewakazia walaji, Tanzania ya sasa hivi haitaki watu aina yenu wanaotaka slope. Mwacheni Jamaa anyooshe Shirika maana hata sisi wanachama tunayaona live. Mimi nilifungua madai yangu ya fao la kukosa ajira mwaka jana na nimelipwa pesa zangu fresh na fasta tu. Ujue tuache mambo ya uongo uongo wakat sikuhizi mambo yapo wazi sana. Mpeni jamaa ushirikiano aendeleze mazuri yake, achen roho za kwanini. Pia Ukiandika tena mawazo yako usiyafananishe kama jina lako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Urio ana kismeti cha kupata vyeo. Ila kusema kweli kiutendaji ni Zoba kabisa. Sijui Kwa nini Rais alimpeleka huko. Pale PPF nilikuwa namkubali Kashimba.
 
Issue sio kumpenda ww, issue ni utendaji wake, ingekua issue ni kubebwa asingedumu miaka yote kwenye haya mashirika. Kwenye ukweli tuseme ukweli tu. Tujifunze ku appreciate na kubadilika.
Urio ana kismeti cha kupata vyeo. Ila kusema kweli kiutendaji ni Zoba kabisa. Sijui Kwa nini Rais alimpeleka huko. Pale PPF nilikuwa namkubali Kashimba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Urio ana kismeti cha kupata vyeo. Ila kusema kweli kiutendaji ni Zoba kabisa. Sijui Kwa nini Rais alimpeleka huko. Pale PPF nilikuwa namkubali Kashimba.
Aliingizwa na Ben Mkapa - mjombake! Ngoja aendelee tu kuendekezwa na Magu ila mambo yatakuwa hadharani sio muda mrefu kachukua wale wafanyakazi waliokuwa Mifuko ya zamani kawapeleka NSSF na kusababisha ule Mfuko kuwa hoi kwa kukosa michango.
 
wanatapa tapa tu 😂 😂 wakaziwe hivyo hivyo dadeki
 
hakuna ushabiki hapo soma tena uafanye ufikirishi ujionee mwenyewe tatizo mleta mada kalamikia sana maswala ya mpigo na vitengo kuliko uhalisia wa wateja (ambao kawagusia kidogoooooo kama kichaka cha kuficha tu ajenda yake)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…