Carnivora
JF-Expert Member
- Jan 26, 2018
- 3,644
- 6,028
Habari za usiku huu wakuu.
Nina imani viongozi na wahusika wa suala hili wanapita katika forum hii, maana kwetu watu kama sisi ndio sehemu pekee ya kutolea maoni, kero, na vitu kama hivyo.
Mimi ni mtumiaji wa barabara za jijini Dar es Salaam kwa kiasi kikubwa. Kazi zangu zinahusu kutembea na chombo cha moto barabarani nikikagua hili na lile na kutolea rwports. Kwa hivyo naandika kwa uzoefu wangu wa muda mrefu.
Kwanza kabisa, makutano ya barabara za Morogoro na United Nations pale Fire. Kunakuwa na sintofahamu sana hasa kukiwa na magari mengi nyakati za asubuhi na jioni. Watu wanaotoka Muhimbili wakielekea jangwani (Magomeni Mapipa) kwa kupinda kulia huwa wanazua kizaa zaa sana mahali pale. Kwa utaratibu wa taa hazioneshi kuna kupinda kulia, cha ajabu hata wakiwa askari huwa wanaruhusu right turning katika mazingira hatarishi. Na huku wanakotokea sijawahi kuona alama ya kukataza kupinda kulia (naomba nisahihishwe kama ipo). Kwa maoni yangu mahali pale hapafai magari yanayotoka Muhimbili kupinda kulia, ni hatari, na wanaotoka Kariakoo nao wanataka kupita pale pale. Lifanyieni kazi hili.
Pili, makutano ya barabara za Ali Hassan Mwinyi/Bagamoyo na Mwai Kibaki/Kawawa pale Morocco. Niseme ukweli, polisi wa pale wana upendeleo uliopitiliza katika kuongoza magari. Wamekuwa wakipendelea wanaotumia A.H. Mwinyi Road kwenda Bagamoyo Road na kuwaacha wanaokatiza toka Kinondoni kwenda Oysterbay/Mikocheni-kwa kutumia Kawawa na Mwai Kibaki Roads hasa nyakati za jioni. Inasemekana watumiaji wanaotoka Posta wanatoka "makazini" na jioni wanarudi nyumbani kupumzika. Lakini kimsingi muda wa jioni kila mtu anajitahidi kurudi kwake. Hata wanaotoka Masaki, Mikocheni, Kawe, Mbezi beach ya chini n.k nao wanakwenda nyumbani. Pia inasemekana bara bara zinazopewa kipaumbele zinatumika na viongozi wengi muda ule. Mnataka kutuaminisha viongozi wengi wanaishi Mbezi Beach, Goba, Tegeta, Kunduchi..n.k? Mi sijui, lakini nao ni watu kama namba acha tusome wote. Mtu anaweza toka Bamaga akaja kupita Morocco wakati aliyeko ubalozi wa Marekani hajakatiza Morocco. Huku Kinondoni foleni inafika Manyanya afande hana habari kabisaaaa. Anapeta tu one way.
Kama kweli kuna viongozi wengi basi wawe wanajaribu kubalance muda...kama dk 5 kwa 3 au 7 kwa 5 ili kuweka mambo sawa. Wakati mwingine tunalalamika foleni lakini foleni zinaletwa na askari wanaoongoza magari kwa kujifanyia mambo watakavyo wao si namna hali inavyotaka. Ndio maana wanajeshi wanaamuaga kushuka na kujipitishia magari yao na sometimes kuwapiga vibao polisi kwa kupendelea upande mmoja.
Ni hayo tu. Afande anayehusika ongea na watu wako tafadhali, tuifanye Dar iwe mji mzuri kwa usafiri.