Makutano Show,
..muulize kuhusu suala la MUUNGANO wa Tanganyika na ZNZ.
..je, bado CUF inasimama ktk hoja yake ya serikali 3, au inaunga mkono hoja ya Maalim Seif kuwa na muungano wa mkataba?
..kama anaunga mkono serikali 3 unatakiwa umuulize kwanini? kwanini anaona serikali 3 ni bora kuliko serikali 2, au "muungano wa mkataba"??
..kama anaunga mkono muungano wa mkataba, unapaswa kumuuliza faida za muungano huo, haswa kwa wa-Tanganyika. pia umuulize kwanini mahusiano yetu yasiwe kupitia EAC, au SADC, au kuna ulazima gani wa kuwa na mkataba kati ya Tanganyika na Zanzibar??
..kuhusu muungano pia, unaweza kumuuliza kuhusu faida zake kwa WATANGANYIKA. kuna baadhi yetu ambao tunaamini muungano huu UNATUNYONYA wananchi wa-Tanganyika. Ushahidi wa madai hayo upo ktk tafiti mbalimbali kama ule uliofanywa na PROF.TEDDY MALYAMKONO. sasa tunaomba kujua ni nini mtizamo wa Prof na chama cha CUF kuhusu madai ya wa-Tanganyika kwamba muungano umekuwa-burden kwao??
..kuna suala la madai ya Radio Imaan kwamba hapa Tanzania kuna MFUMO KRISTO. Je, msimamo wa CUF na Prof kuhusu madai ya kuwepo MFUMO KRISTO.
..kuna suala la Shekhe Ponda. Huyu bwana alishatokea kule ZNZ ktk mikutano ya Uamsho. Pamoja na mambo mengine, mikutano hiyo inasifika kwa kutoa matamshi ya kashfa dhidi ya wa-Tanganyika, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, na muungano kwa ujumla. Sasa nini msimamo wa CUF na Prof kuhusu kashfa hizo??
..mwisho, maadamu Prof ametoa offer ya kumdhamini Shekhe Ponda, je yuko tayari kutoa mkono wa pole kwa kukarabati walau kanisa moja liliotiwa kiberiti, au kufidia mali zilizoibiwa??
NB:
..waandishi wengi wa habari huwa mnashindwa kuuliza maswali magumu, and follow up questions.
..pia ktk kila interview uhakikishe kwamba wananchi wanapata kitu kipya kutokana na interview hiyo?