Makutano Show: Alichokisema Mhe January Makamba

Makutano Show

Member
Aug 3, 2012
21
65
Wana-JF

Kama nilivyowaambia Jumamosi nilikuwa na Mhe January Makamba ambapopamoja na kuelezea maisha yake ya kawaida ya kisiasa pia alijibumaswali yenu.

Moja ya vitu alivyosema ni kuwa hana mpango wa kugombea Urais. Alisema anaamini nafasi ya urais inahitaji mtu ambaye amejiandaa Kisaikolojia, Kisiasa na Kifikra na kumalizia kwa kusema kuwa Urais sio uamuzi wa mtu mmoja kwa sababu nchi haiendeshwi na mtu mmoja nainahitaji watu ambao wanashauriana, kuandaa dira ya pamoja na kupeleka ujumbe wa kuwaunganisha Watanzania.

Alipoulizwa Rais anayekuja anatakiwa aweje alisema anatakiwa awe ni mtu atakaewaunganisha Watanzania huku akisema mianya ya ukabila, udini na rushwa ambayo babawa taifa Mwalimu Nyerere aliitaja imeanza kuonekana.

Pia Makambaalisema rais ajaye anatakiwa asiwe mtu mwenye hulka ya visasi na anatakiwa awe na uwezo wa kuwaambia wananchi kuwa yeye sio masiha wa kuyafanya maisha yao yabadilike papo kwa hapo kwa kuwa nchi ni ya watu wote, hivyo kila mmoja ana wajibu wa kutumia nafasi yake kuleta mabadiliko.


Alipoulizwa katika wanasiasa wa upinzani ni yupi anamkubali, alimtaja Zitto Kabwe kwa sababu ana uwezo wa kusema na kusimamia kile anachokiamini, ujasiri wa kuomba ushauri kama kuna jambo ambalo halielewi na pia anapenda kusoma na kujifunza. Pia alitaja kuwa anamheshimu sana Profesa Ibrahim Lipumba na wanasiasa wengine wa upinzani.

Pia alizungumzia nguvu ya mitandao ya kijamii, alikubali kuwa imekuwana nguvu katika kuwaunganisha wananchi kudai haki zao na pia kuwakutanisha watu wenye msimamo mmoja na kujadili mambo mbalimbali na akakiri kuwa chama cha mapinduzi kiliachwa nyuma katika hili lakini kwa sasa wanawasisitiza viongozi wote wilayani kujiunga na kuitumia mitandao ya kijamii.

Mahojiano zaidi yanapatikana katika YouTube channel hapa chini



 
Last edited by a moderator:
Nimependa hapo kwenye kauli yake kuhusu uraisi kwamba si uamuzi wa mtu mmoja na umuhimu wa matumizi ya mitandao ya jamii kwani wanasiasa wengi wanaigopa wakati hii ni sehemu ya kujifanyia tathimini ikiwa kama yatasemwa mabaya dhidi ya uongozi wako yawe ya kweli au la kikubwa unatakiwa uyafanyie kazi yale ambayo unaona kweli yamesababisha utendaji kazi wako kuwa mbovu, mengine chukulia kuwa tetesi kwani mwisho wa siku muda utafika yatadhihirika tu
 
Fina Kipindi unachoendesha ni kikubwa, na pia status yako si ndogo. Ushauri

1. Unapoandika jitahidi kuweka paragraph vizuri (kwa wajuaji wa kusoma "Kiswahili vizuri" wanakereka wanapoona mpangilio huo.

2. Jitahidi kutounganisha maneno kwa mfano kwa uchache umeandika (kugombeaUrais, anayekujaanatakiwa), na haya makosa yameonekana sana.

3. Kama umeamua kuandika "Urais" kwa herufi kubwa mwanzo tumia hivyo pia sehemu nyingine.

4. Usichanganye "fonts" kwa mfano ( kuwaambia wananchi kuwa yeye sio masiha wakuyafanya maisha yao yabadilike papo kwa hapo kwa kuwa nchi ni ya watuwote, hivyo kila mmoja ana wajibu wa kutumia nafasi yake kuletamabadiliko. Alipoulizwakatika wanasiasa wa upinzani ni yupi anamkubali, alimtaja Zitto Kabwe)

5. Jitahidi kuweka koma ama dot panapohusika, na pia jaribu kutenganisha sentensi moja na nyingine.

Najua haujanuna ila utazingatia........Elimu bahari ati!
 
smart as always Fina, January Makamba ni mbinafsi na nilijua atamtaja Zitto Kabwe ila alipoongeza Prof. Lipumba? Kwa lipi kwa Lipumba kudanganywa na akina Seif Shariff Hamad na Hemed Sharid kwa maslahi yao na yeye kuwa kama bendera inayofuata upepo, Zitto kwa kipi kwa kutangaza nia ili hali wenzake wanajenga chama?
 
Fina this is what makes u different from the others. Good feedback and u make us the true owners of the show! Keep up the good work. I was/am still your fan. Big up sana.
 
Fina,

Nimesikitika umeshindwa kumwuliza huyu bwana maswali ya msingi kutokana na majibu aliyoyatoa! Kwa hiyo CDM wangesubiri siku nne basi yasingetokea....Makubwa, na wewe umeshindwa kabisa kumuuliza follow-up questions? Siku nyingine usijikite kwenye maswali uliyoyaandaa bali jitahidi kuuliza maswali kutokana na majibu ya mgeni wako. Wanahabari wote mashuhuri duniani hiyo ndiyo sifa yao kubwa.
 
Safi sana fina tuna shukuru sana kwa mrejesho! Nimeyapenda majibu ya j.makamba sipingi maana ni mawazo yake binafsi!

Naomba utwambie mapema kipindi kijacho nani atakuwepo ili tuandae maswali mapema!
 
mimi mliniboa sana jana ,mlitumia muda mwingi kuongelea mambo yake binafsi ya kuuza pombe ya kinyeji (lubisi) bukoba wakati akiishi na bibi yake, matokeo yake maswali mengi na ya msingi juu maendeleo na elimu jimboni kwake, yaliyo ulizwa na wana jamvi hukumuuliza.

NEXT TIME kama unajua huna uwezo wa kumuuliza maswali yote uwe unasema watu wasihangaike kupost vitu ambavyo unajua huwezi kumuuliza!
 
Safi sana fina tuna shukuru sana kwa mrejesho! Nimeyapenda majibu ya j.makamba sipingi maana ni mawazo yake binafsi!

Naomba utwambie mapema kipindi kijacho nani atakuwepo ili tuandae maswali mapema!
Mimi majibu yake yalinikera, huyu dogo MAKAMBA ni msanii, mfano :jana wakati fina anatoa shukrani kwa JF kwa kutuma maswali yeye january alidai eti haijui jamii forum na hajawahi kuisikia akawa anauliza hivi , i quote “inaitwa jamii forum au JAMBO FORUM”
Huu ni usanii na uongo kujidai haijui Jf ,na binafsi alinikera.
 
Umemhoji ki-professional ila jinsi ulivyoandika!! ... labda awe ni mfanyakazi wako, but there's no way a journalist can write that poorly, oh my god!!!
 
Mimi majibu yake yalinikera, huyu dogo MAKAMBA ni msanii, mfano :jana wakati fina anatoa shukrani kwa JF kwa kutuma maswali yeye january alidai eti haijui jamii forum na hajawahi kuisikia akawa anauliza hivi , i quote "inaitwa jamii forum au JAMBO FORUM"
Huu ni usanii na uongo kujidai haijui Jf ,na binafsi alinikera.

Kwani ni lazima aijue JF?? Try to be open minded. Acha kutuboa na wewe.

 
Mimi majibu yake yalinikera, huyu dogo MAKAMBA ni msanii, mfano :jana wakati fina anatoa shukrani kwa JF kwa kutuma maswali yeye january alidai eti haijui jamii forum na hajawahi kuisikia akawa anauliza hivi , i quote "inaitwa jamii forum au JAMBO FORUM"
Huu ni usanii na uongo kujidai haijui Jf ,na binafsi alinikera.

Waziri wa wizara kama yake asiijue Jamii Forums? by the way mkuu soma signature yangu hapo chini!!!
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom