Makundi yenye dalili kujitokeza ndani ya CHADEMA

Ngoja moto uwake hapo ndiyo tutajua kama CDM ina uongozi thabiti au la?vinginevyo yatatokea kama ya ................ Sisi yetu macho na masikio!

Mkuu umeona mbali.....cha msingi CDM imara itajenga CCM dhaifu.
 
Nyie ndio mnaosema Chama kijitangaze vijijini lakini kimefanya hivyo na kimeanza kupata wanachama wengi sasa imekuwa tatizo tena kwenu du sijui mnataka wafanyeje

Fikra tulivu ndio huzaa Fikra na Mitazamo sahihi...rudi kwenye mada tafakari kisha endelea kuchangia kwa mtazamo chanya.Tatizo hapa sio kujitangaza na tatizo hapa sio kuwa na wanachama wengi kwani hii ni neema kwa chama,kinachozungumziwa hapa ni kwa jinsi gani chama kinapaswa kujipanga kimfumo na kimkakati kuweza kudhibiti wanachama wake katika chaguzi za kichama kuepusha misuguano inayoweza kudhoofisha chama basi, na sio kingine!
 
Dada yangu Eliza, mimi sikusema majundi nimesema makundi.Ukweli una hulka moja hautaki kupuzwa, CHADEMA kama ilivyo CCM vyote ni vyama vya siasa vilivyoanzishwa na watanzania wenye utamaduni unaoendana, tofauti yao ipo kwenye mitazamo. Kukubalika au kutokubalika kwa chama kunatokana na nyakati husika. CCM ya kipindi cha nyuma ilikuwa inakubalika kama CDM inavyoanza kukubalika sasa, kinachowaponza CCM sasa ni dhana nzima ya kimfumo na kimkakati (WAMEKATAA UKWELI KAMA WEWE UNAVYOUKATAA SASA). Yapo makundi ya kufikirika ndani ya CDM ambayo yanaweza kujitokeza na kuathiri chama kama ilivyo sasa kwa CCM.Ninapozungumzia makundi nina maana ya misuguano ya kimaslahi(yawe ya kiuongozi, fedha n.k.) ambayo yana nia ya kudhoofisha chama. Pamoja na CCM kuwa na viongozi imara kipindi cha nyuma kama ilivyo kwa CDM sasa, kimeshindwa kujipanga kimfumo na kimkakati kukabiliana na changamoto za nyakati, Na usidhani CDM itakubalika tu kimujiza bila kufocus kimfumo na kimuundo. Viongozi wa CDM ni binadamu tu kama walivyo wa CCM,ni wajibu wetu kukumbushana.

Tambua uongozi wa chama hauanzii makao makuu ya chama. Unaweza kujikumbusha tu kwa mfano ni kwa nini baadhi ya maeneo ya Tanzania CDM walishindwa kusimamisha wagombea? Kujipanga! Narudia kwa kuwa wagombea udiwani na ubunge wanatoka katika ngazi ya jimbo na kwa kuwa mwaka kesho kuna uchaguzi na kwa kuwa 2014 kuna uchaguzi wa kiserikali na 2015 uchaguzi mkuu ipo haja ya kujipanga kimfumo na kimkakati kuepusha misuguano ya kimaslahi na rushwa ndani ya chama.

Naomba ushambulie hoja
.

Unajuaje kwamba CDM hajipangi au haijajipanga? Halafu tatizo la CCM sio la kimfumo wala kimkakati kama ulivyoandika. Tatizo la CCM na Serikali ni kukumbatia "ufisadi na watoto wake".Kumbuka EPA,Meremeta,Deep Green, Radar n.k. Wapi hatua imechukuliwa? Hii ndio kansa inayoitafuna CCM na Serikali yake.Naona unajichosha bure kuandika vitu vya kufikirika. Je wanaojiunga na CDM nini kinchowasukuma? Na wanaojiunga au kuwepo ndani ya CCM nini kinachowasukuma? Kamwe hamna chama ambazo hakiwezi kuwa na makundi,ila "chemistry" ya makundi hayo ndio inatofautiana.Hata CDM nayo itakuwa na makundi tu hilo haliepukiki ila yatakuwa ni makundi yatakayotofautia kwa mambo ya msingi.Na sababu ya msingi ninayo. Nguvu kubwa iliyo nayo CDM kwa hivi sasa inatokana na dhamira ya dhati itokayo miyoyoni mwa watu ambao wamechoshwa na hali ngumu ya maisha na kutokuwajibika kwa CCM na serikali yake,haisukumwi na nguvu ya ukwasi kama ile ya Tsunami ya 2005 ambayo zao yake ndio haya makundi yanayoimaliza CCM na serikali yake! Hiyo ndio tofauti ya makundi ndani ya CCM na CDM
 
Ndugu yangu, aksante sana kwa mtazamo wako, sina nia mbaya na CDM ila nina mtazamo wa mbali kuhusu CDM. Jambo la msingi unalopaswa kutambua ni kwamba jukumu la kujenga chama sio la Dr.Slaa, Mbowe, Lissu na Zitto, ni jukumu la watanzania wote wapenda mabadiliko. Tunapozungumzia mfumo kwa maana ya mada hii nazungumzia ni kwa jinsi gani chama kinajipanga kushughulikia misuguano mbalimbali inayoweza kudhoofisha chama kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Umeandika vizuri sana, kwamba ufisadi ndio umetafuna chama cha mapinduzi na umeandika "Tatizo la CCM na Serikali ni kukumbatia "ufisadi na watoto wake""je hili sio tatizo la kimfumo? na je ufisadi huo hauwezi kujipenyeza CDM iwapo hakutakua na mkakati wenye utashi timilifu? Tambua uongozi wa chama hauanzii makao makuu ya chama, kuna viongozi wa wilaya na majimbo, hawa wasipoandaliwa kisaikolojia, kimbinu na kupewa ethics za uongozi wanaweza kabisa kudhoofisha chama. Kumbuka 2015 jukumu kubwa la kuchuja na kuteua wagombea wa CDM utaanza katika ngazi ya chini kabisa. Kiongozi au mpenda mabadiliko yoyote lazima awe na vision ya mbali, usifikirie kesho tu bila kufikiria na keshokutwa. Na usidhani CDM itakubalika tu kimujiza bila kufocus kimfumo na kimuundo. Viongozi wa CDM ni binadamu tu kama walivyo wa CCM,ni wajibu wetu kukumbushana.

Chaguzi ndogo hizi zisikuvimbishe kichwa, kumbuka viongozi makao makuu ya chama wanahama kwenye jimbo husika, je jiulize mwaka 2015 kwenye majimbo zaidi ya 180 Tanzania bara tu, yataweza kusimamiwa na viongozi toka makao makuu kwa ukaribu?Na usi-prejudge tu kwamba makao makuu wanajipanga, kama wewe ni mpenda mabadiliko mawazo yako wanaweza kawasaidia wa kina Dr. Slaa, Mbowe na wengine katika kukidhi malengo ambayo kwa mtazamo wako wanayatambua na mimi sina shaka na hilo ila sote tunawajibu wa kutoa mapendekezo yetu.
 
Back
Top Bottom