Mbelwa Germano
JF-Expert Member
- May 7, 2011
- 789
- 289
Hali ya sasa ya kukubalika kwa kasi kwa CDM inatoa tafsiri nyingi kuhusu mustakabali wa baadaye. Wingi wa Wanachama ni ishara ya kujitokeza kwao kushiriki katika kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama. Lakini kikubwa zaidi cha kutazama ni kwa jinsi gani uteuzi wa wagombea nafasi za udiwani na ubunge zitafanyika. Ni ukweli usiopingika kama CDM wasipokuwa makini kutatokea makundi kama yaliyopo ndani ya CCM na kusababisha loopholes kwa CDM na kutoa mwanya kwa wapinzani(CCM) hivyo kuna kazi ya kujijenga kimuundo na kimkakati.
Kama nilivyotahadharisha awali kunahitajika umakini wa kuwaandaa viongozi wa chama wa wilaya na majimbo ambazo ndio wanasimamia upatikanaji wa wagombea kwa nafasi nilizoeleza awali. Bila kuweka mazingira mazuri makombora ya ufisadi yataelekezwa CDM na kurudisha imani kwa CCM.Ni ukweli usiopingika kama vita ya kuwania uteuzi kwa nafasi hizi itakuwa motomoto kwa CDM.
Kama mdau, unadhani nini kifanyike kuepusha makundi haya.
Nawakilisha