kibol
JF-Expert Member
- Apr 24, 2012
- 4,636
- 2,885
Na Frey Cosseny
Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa Vyama vya vingi hapa nchini ndani ya Chama Cha Mapinduzi kulitokea makundi yanayohasimiana katika Vita ya kutafuta kuongoza dola.
Makundi haya yapo kuanzia ngazi ya Urais hadi vijiji/mitaa.
1994 ndani ya ccm iliasisiwa makundi matatu muhimu ktk Vita ya kusaka urais.
Muasisi wa makundi haya ndani ya ccm naweza kusema ni aliyekuwa Waziri Mkuu na makamu wa Kwanza na pia makamu Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Tanzania Bara Mzee Dr Samuel John Malecela.
Makundi makuu yako matatu ndani ya ccm mpk Leo.
Kundi la Wazee ndani ya Chama ndani, kundi ili iliyongozwa na Mzee malecela na shemeji yake Prof Mark Mwandosya kundi ili kwa jina lingine linajulikana kama Mtwara Corridor.
Kundi lingine ni lililokuwa likiongozwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa sasa kundi limebaki pale Nyerere Foundation.
Kundi la mwisho ilijukana kama kundi la Vijana ili ndilo kundi la akina Jakaya kikwete, Edward Lowassa Abdurahaman Kinana akina Marehemu Dr Didas Masaburi akina Marehemu Mzee Samuel Sitta.
Mwaka 1994 kuelekea 1995 makundi mawili yalikuwa na fedha za kutosha yaani kundi la malecela ambayo ilikuwa imekamata wakuu wa Mikoa, Madc wenyeviti wa ccm ngazi ya mikoa na Wilaya na watendaji wa chama ktk ngazi zote.
Na kundi la vijana ambao walijikita ktk Umoja wa Vijana wa ccm na wafanyabiashara.
Kundi la Nyerere ilikuwa kundi la watu maskini lakini wakimtegemea sana Mwalimu Nyerere kujenga hoja na ushswishi mwisho wa siku kundi ilifanikiwa kutoa mgombea wa Urais Dr Benjamin William Mkapa.
Toka wakati huo haya makundi hayajawahi kufa ndani ccm, uchaguzi wa kumpata mgombea unapoisha ndani chama waasisi wa makundi haya uyafufua.
Wafuasi wa makundi haya uwa mara nyingi unufaikaa na uwepo wa makundi haya ndani ya chama kwasababu vinara wa makundi haya uambulia pesa na wakati mwinginemadaraka ndani ya serikali iwapo kundi unalouunga ikifanikiwa walau kuingiza mgombea wao ndani ya serikali au Kamati Kuu ya ccm.
Makundi mara ujikusanyia mapato na kuwapa wafuasi kuchafua kundi lingine.
Na vyombo vya habari hasa Magazeti utumika sana kuwachafua wapinzani wao.
Ili la January Makamba na Bernard Membe kuhusishwa kumpinga Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa JMT Dr John Pombe Magufuli inawezekana kuwa ni sehemu ya Vita ya makundi ndani ya ccm kuelekea 2025.
Ninavyomfahamu Mzee Yusuph Rajabu Makamba na misimamo yake kuhusu uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi sidhani ili lililoandikwa kwenye gazeti la tanzanite anaweza kuliunga mkono hata kwa chembe .
Nakumbuka hata January Makamba kuomba kugombea uraisi kupitia 2015 Mzee ilimchukua muda mrefu kukubali January Makamba kuingia ktk kinyang'anyiro ilitumika nguvu ya vijana kwenda kumshawishi Mzee mpk akakubali kutokana na msimamo wake.
Kama 2015 Mzee Makamba alimgomea mwanae hivi itaingia akilini Mzee Makamba kumuunga mkono January Makamba kupambana na mwenyekiti wake 2020?
Nimemfahamu Mzee miaka 22 iliyopita akiwa Rc Morogoro ni Moja ya wazee wenye msimamo ndani ya Chama.
2010 nakumbuka Mzee Makamba akiwa Katibu Mkuu wa Ccm Taifa pale Mzee Magale Shibuda akiwa Mbunge wa Maswa kupitia Ccm aliamua kuchukua ya kugombea uraisi kupitia Ccm kushindana na Jakaya Kikwete nadhani mnafahamu kilichompata Shibuda mpk akakimbilia Upinzani hivi leo Mzee aamuunge mkono mwanae kuchukua kupingana na Magufuli 2020?
Natambua kuwa kuna Wakuu wa mikoa watatu na mawaziri wawili ambao wanajifanya wao ndiyo watoto wa Magufuli na Hawa walikuwa watoto kindakindaki wa Mzee Bernard Membe
Hawa ndiyo wanaotengenezea wenzao Vita na Mwenyekiti na Rais wa JMT Dr John Pombe Magufuli.
Ushauri wangu mdogo kwa Mwenyekiti wetu akae na Mtangulizi wake Jakaya kikwete atamueleza tabia ya Hawa vijana wanaojifanya sasa kuwa wafuasi kindakindaki wake tabia ya Hawa vijana.
Sisi tulilelewa ndani ya Chama cha Mapinduzi tulifundishwa kujenga chama kama taasisi na siyo Mtu.
Mimi kwangu chama ni Bora zaidi kuliko mtu.
Nampenda sana Magufuli kwasababu ni Mwenyekiti Wangu wa chama na mwanachama mwenzangu nje ya hapo sina unasaba na Magufuli.
Tatizo linalolikumba chama cha Mapinduzi sasa kuna wafuasi wa watu ndani ya chama badala ya wafuasi wa Chama.
Athari ya chama kuwa na wafuasi wa mtu ni kwamba tunapata wanachama wachumia tumbo ambao wako kwenye chama kwa maslahi ya tumbo lao na watu wakipata ya kuwa viongozi wanawatengeneza wapambe wa kuwasifia na kuwapigia makofi hata wakifanya mambo ya Kijinga.
Namini haya yakiyoandikwa kwenye gazeti la Tanzanite kuhusu Bernard Membe na January Makamba ni muendelezo sehemu ya Vita ndani ya wasaka Urais ndani ya Chama kuelekea 2025 ila wameanza mapema kuvunja nguvu wenzao.
Ninachoaminj Urais utolewa na Mungu.