Shule ya sekondari makumira inayopatikana maeneo ya Usa River jirani na chuo kikuu makumira kimetapeli baadhi ya wanafunzi akiwemo ndugu yangu, walikua wanasoma hapo kama school candidates lakini ilipofika wakati wa usajili wakawasajili vijana hao( hasa wa michepuo ya science) kama private candidates. Nimeshangazwa na hili hasa baada yakutaka kujua matokeo ya ndugu yangu huyo. Nilipojaribu kumuuliza kwanini hakulisema hilo mapema ameniambia walisisitizwa kwamba hakuna shida yoyote kupewa namba za private candidates. Wanajamvi nahitaji ushauri wenu namna yakushughulikia hili jambo kwa mamlaka zinazohusika.