Makumira moto bado wawaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makumira moto bado wawaka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mzee wa inshu, Jan 28, 2011.

 1. m

  mzee wa inshu Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 49
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Moto wa mgomo uliowashwa jumatatu na wanachuo wa mwaka wa kwanza wakilalamikia ukiritimba unaofanywa na uongozi wa serikali ya wanachuo katika kufuatilia mikopo yao bodi bado haujazimika japo safari hii ni mwaka wa pili ambao hapo juzi walikutana na kupanga kupeleka hoja yao mbelee ya uongozi wa chuo kupinga kulipishwa tsh100000/= wannazolipishwa na chuo kila mmoja kwa kila semista . Kila mwanafunzi hutakiwa kulipa tsh100000/=(lakimoja) kilamwaka kuanzia mwaka wa kwanza hadi wa pili kwa ajili ya field(BTP). Kiasi hiki kinallalamikiwa na wanachuo kwa sababu kwanza ni kikikubwa, pili field (teaching practice) ni miongoni mwa masomo (kozi) zilizo sajiliwa na chuo hivyo ilisha lipiwa kupitia ada ya chuo na sio sahihi kuwalipisha wanachuo kwa ajili ya kozi hiyo. Tatu kama ni halali kwa nini gharama hizo hazipo kwenye orodha ya gharama zilizopelekwa bodi ya mikopo ya wanafnzi ili zijumuishe pamoja kwenye gharama za chuo? Lakini wakati wanachuo hao wakijiandaa kuwasilisha malalamiko yao kwa uongozi wa chuo kupitia wakilishi WASALITI wakiongozwa na makamu wa serikali ya wana chuo aliyejulikana kwa jina la Zamaka aliwazunguka wenzie na kwenda kusiliba kwa uongozi wa chuo kuwa mwaka wa pili wanaandaa mgomo. Baada ya kupata habari hizi ndipo uongozi wa chuo ulianza kuhaha kuwasaka wawakilishi hao kwa madai ya kupanga kuchochea mgomo. Hapo jana saa 4 asubuhi uongozi wa chuo uliiitisha kikao cha dharura ambapo wawakilishi wa wanachuo mwaka wa pili waliitwa na kusomewa mashitaka ya kula njama za kuanzisha mgomo nakupewa vitisho vya kufukuzwa chuo kama wataendelea kufuatilia madai haya. Baada ya kikao hicho wawakilishi hao wa mwaka wa pili walinekana kuwa kimya kutozungumza lolote huku wakionyesha kuchanganikiwa ikiwa ni ishara ya kupigwa mkwara mzito! TAFAKARI! Hivi kuandaa hoja za kuwasilisha mezani kujadiliwa ni kuandaa mgomo? Je, kama ni mgomo kwanini waandaliwe wawakilishi kukutana na uongozi? USHAURI. Uongozi wa chuo uache uoga kwa kutumia vitisho na udikiteta badala yake unatakiuwa kutoa majibu kwa kutumia hoja za msingi zilizo jengeka ili kuleta suluhu ya kudumu pia kujenga taifa lenye viongozi wanaojiamini katika kuleta mabadiliko ya kimfumo, kiutawala na kifikra. Kama madai haya hayana msingi kwanini uongozi uogope kulizingumzia wazi suala hili? Mathalani , tsh100000000/=(milioni miamoja) zinatarajiwa kukusanywa kutoka kwa wanafunzi wa mwaka wa pili na wa kwanza mwaka huu wa masomo 2010/2011. Je kiasi hiki(milioni 100) ni kwa ajili ya gharama zipi katika gharama za teaching practice zaidi ya posho za wakufunzi wakati wa zoezi lisilo zidi wiki tatu?
   
Loading...