Makubaliano yamefanywa Muungano umevunjwa rasmi bila maandishi wala tangazo na Zanzibar inaruhusiwa kujifanyia kila kitu isipokuwa kuwa na jeshi

Wenye akili tunajua kuwa huu muunganao wa mchongo umeshavunjika kitambo sasa hivi kuna utumwa wa Tanganyika ndani ya Ukoloni wa Zanzibar.
 
Bara kuna ufisadi ndio, na hizo zinazofisidiwa zingesaidia kutatua baadhi ya mambo, lakini haiondoi ukweli kwamba mikopo hii inapochukuliwa lengo ni kuipatia Zanzibar fedha za maendeleo kupitia mgongo wa Tanzania.

Na kama kuna ufisadi, kwani anaesimima nchi ni nani? Si huyo huyo anaechukua mikopo kwa ajili ya Zanzibar? Kwa nini hadhibiti huo ufisadi? Au ndio tuseme ana maslahi katika ufisadi unaofanywa bara ndio maana anauachia bila kuchukua hatua?

Unasema bara kuna ufisdi sana, nje nje, sasa tuambie, tangu huyu raisi achukue madaraka, wangapi umesikia wamekamatwa kwa ajili ya ufisadi? Huo ufisadi ambao hadi wewe unauona yeye hauoni kwa sababu anajiita chura kiziwi?
 
hasa kuimarisha KMKM na JKU, Zanzibar tayari ni free state, kombo akiamua kufanya kama diria huko nje kwa kiburi tu cha zanzibar kujiona ni nchi kamili kuna wa kukataa zanzibar isivunje katiba ya JMT?
Labda wafanye hivyo sasa wakati Samia wa Zanzibar ndio raisi. Kwa sababu wakifanya hivyo inakuwa ni uasi wa kama vile tu Kilimanjaro au Mtwara kujitangazia jeshi na uhuru wake. Amiri jeshi atachukua hatua ya kupeleka JWTZ kwenda kuzima uasi.

Sasa wakiasi sasa wakati Samia ndio raisi, yeye kama amiri jeshi mkuu anaweza kukataa kupeleka JWTZ Kuzima uasi wa Zanzibar. Lakini hiyo haitazuia baada ya kipindi cha Samia raisi ajae toka bara kuwaambia JWTZ nendeni mkarudishe madaraka kamili ya Tanzania kule Zanzibar - shoot to kill kama walivyofanya KMKM huku bara 29 October 2025. Sasa KMKM na JKU wataweza kupambana na JWTZ? Kwanza kuwapiga huhitaji hata kuweka boots on the ground in Zanzibar. Unawatwanga ukuwa huku huku bara - Bagamoyo hapo.

Unaona basi palivyo pagumu? Na ole wa Zanzibar hilolitokee na raisi ajae awe mtu asiempenda Samia. Mbona watakoma!
 
wakifanya uasi ndani ya utawala wa samia rais ajaye ataweza vipi kuirudisha kwenye muungano?
 
wakifanya uasi ndani ya utawala wa samia rais ajaye ataweza vipi kuirudisha kwenye muungano?
Kwa sababu unaweza ukafanya uasi, na uasi ukaendelea kwa kipindi fulani lakini haitahalalisha uasi wako kwa sababu umetawala nchi chini ya uasi kwa kipindi hicho. Kwa mfano. Urusi imeteka maeneo ya Ukraine na inayakalia kwa sasa. Anaweza kuja raisi miaka kadhaa baada ya Zelensky na kuyarudisha.

Na uasi wowote unaofanywa na nchi isitambuliwe kama nchi halali na Umoja wa Mataifa, basi bado inakuwa sio nchi. Jiulize, Zanzibar wakifanya uasi, UN watawatambua kama nchi kamili? Oman wanaweza kuwatambua, lakini bila UN kuwatambua bado wanakuwa si nchi halali, ni waasi.

Kwa hiyo ukifanya uasi, kupita kwa muda ukiwa katika nchi ya uasi hakuhalalishi uasi wako. Nchi uliyoifanyia uasi itakupa kibano kwa wakati na kiongozi muafaka

Nigeria, jimbo la Biafra lilijitenga, na hata Tanzania tukawaunga mkono. Lakini baadae Nigeria ilikuja kulirudisha chini ya himaya yake.
 
Wakuuu karibu Sana ugari dagaa nyasa na maji baridiiiiiii Sana! Hizi mbio sio za kushiba ukipata nafasi tembea hata peku inapunguza magojwa ya kisukal. Afya ni bora!
 
Inasikitisha sana
 
Sawa.
 
@Whocares!!? Who fkn caress.!??
 
Ndipo mnapojifichia, kuuita ukweli unaosemwa kuwa ni chuki na ubaguzi. Mnataka siku moja watu wa Pemba na Zazibar wachinjwe kama kuku huku bara ndio mtajua tulikuwa tunawaambia kuna tatizo nyie mnsingisia chuki na ubaguzi
Wachinjwe kwa kosa lipi?. Hizi akili ndizo Nyerere alituonya mwaka ule wa 1995 pale Kilimanjaro Hotel.

Unaweza ukawaondoa kwa vurugu wapemba na waunguja halafu ukishamaliza utatafuta kabila jingine la kunyooshea vidole.
 
Huyo muungwana alitakiwa ajue kwamba huku bara kuna miradi mikubwa zaidi ya hiyo ya huko visiwani.

Uwanja wa ndege wa Tabora mradi mkubwa.

Daraja la Pangani na lile la Magomeni miradi mikubwa.

Ujenzi wa meli nne kule Karemi Ziwa Tanganyika miradi mikubwa sana.

Ndege nne zinakwenda kununuliwa mwaka huu zikiwa nyongeza ya zile 16 zilizopo, miradi mikubwa sana.

Ujenzi wa bandari ya Bagamoyo mradi mkubwa sana.

Zanzibar inajengwa lakini Bara inajengwa zaidi na zaidi.
 
Ni sawa lakini toka lini ukasikia Zanzibar wananyosheana vidole juu ya ufisadi,kule watu kidogo Wana hofu ya mungu kwa pesa ya walipa Kodi ndio maana miradi inaonekana ikifanyika sio bara,huku watu wanawaza upigaji tu ko hata tukipewa trl 100 zitakazo enda kwenye lengo husika ni trl 20 tu.
Kuhusu yeye kuchukua hatua ni kwanini yeye ndo achukue hatua?labuda ungesema anatakiwa asikilize sauti za wachache wanaodai katiba mpya ambayo italeta taasisi imara hapo ndo kila mmoja atawajibishwa na mifumo bila kumtegemea mtu mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…