Makubaliano ya Kakonko: Mbowe na Zitto walisema nini

Makubaliano ya Kakonko: Mbowe na Zitto walisema nini

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Joined
Mar 2, 2007
Posts
1,562
Reaction score
10,896
Mnamo tarehe 30/5/2018 Viongozi wa Vyama 2 vya upinzani nchini ndg. Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto na Bwana Freeman Aikael Mbowe walitamka dhamira ya kushirikiana kwa kuanzia kuweka mgombea mmoja wa ubunge Jimbo la Buyungu Mkoa wa Kigoma na hatimaye nchi nzima. Makubaliano haya ambayo yanarejewa kama MAKUBALIANO YA KAKONKO) hatimaye yatafikishwa kwenye vikao vya Vyama vya ACT Wazalendo na CHADEMA ili kupata baraka za wanachama.


Kuna watu kadhaa wamekuwa wakihoji kwa uzuri au Kwa ubaya makubaliano haya. Ndugu Ado Shaibu ameweka Maelezo ya Viongozi hao ‘ verbatim ‘ ili wanachama na Wananchi Kwa ujumla wajue kiini chake Nini haswa.


Chama cha ACT Wazalendo Katika Kikao chake cha January Mwaka 2018 kiliazimia Katika mwelekeo wa Chama Mwaka 2018 kuwa ni Muhimu kujenga mashirikiano na Vyama vingine na makundi mengine ya kijamii. Mwelekeo huo umewekwa hapa pia. Tunataka kujenga a DEMOCRATIC FRONT kwa kuhusisha wana Demokrasia nchini kwa madhumuni ya 1) kutetea, kuimarisha na kulinda Demokrasia yetu ya Vyama vingi 2) kujenga Uchumi shirikishi wa Wananchi ( inclusive economy).



MAKUBALIANO YA KAKONKO ( YAMINI YA FREEMAN MBOWE NA ZITTO KABWE JIMBONI BUYUNGU ).


Na Ado Shaibu


Msiba wa Mwalimu Bilago, Mbunge wa Jimbo la Buyungu, Naibu Waziri Kivuli Wa Wizara ya Elimu, Mwenyekiti wa Kanda ya Magharibi na Mjumbe Wa Kamati Kuu ya CHADEMA ulikuwa wa aina yake. Kubwa ni mnyukano wa dhahiri baina ya Spika na Mwenyekiti wa CHADEMA kuhusu tarehe ya mazishi ya marehemu. Spika akisisitiza marehemu azikwe Jumatano, CHADEMA walisisitiza na kusimamia Marehemu azikwe Alhamis ili kuwapa nafasi wananchi wa Buyungu Kumuaga mwakilishi wao. Baada ya mvutano wa muda mrefu, mwishowe Spika alisalimu amri na kuwaacha CHADEMA waendelee na utaratibu waliojipangia na familia. Akitoa hotuba yake wakati Wa kumuaga marehemu, Mbowe alimwita Zitto jukwaani na walichokifanya kinaelekea kubadili mwelekeo wa mambo Katika siasa za Tanzania. Lakini, hadi sasa, watu wengi bado wana maswali;


Nini hasa kilitokea?


Nini kilisemwa kwa mapana yake?


Yaliyosemwa yana matokeo gani Katika mwenendo Wa siasa za nchi yetu?


Nini kinafuata?


Baadhi ya maswali haya yanatokana na ukweli kwamba kutokana na kutokuwepo na vyombo vya habari vya kitaifa vilivyoripoti tukio zima msibani Kakonko, baadhi ya watu wameshindwa kupata picha kamili ya kilichotokea. Ili kuziba sehemu ya pengo hilo nimelazimika kuandika (transcribe) yaliyosemwa ili kuwawezesha wachambuzi, wadadisi na wapenzi wa demokrasia nchini kuelewa kilichotokea ili kushiriki vyema Kwenye mjadala huu. Kwa wapenzi wa video wanaweza kuirejea hotuba yote kwenye ukurasa wa CHADEMA Wa Kanda ya Magharibi ()

.......


Freeman Mbowe, Mwenyekiti, CHADEMA


"Mikoa iliyotangulia kwenye mageuzi ilikuwa mikoa ya Kilimanjaro, Kigoma na Mara. Hii ndiyo iliyokuwa mikoa kinara ya mageuzi nchini"


"Mkoa Wa Kigoma umezalisha wanasiasa wengi. Kama kuna Mkoa.. ninarudia na Zitto ananisikia..Kama kuna mkoa majimbo yake yote yalistahili kuwa ya upinzani ni Mkoa Wa Kigoma"


"Lakini, tofauti za kimitizamo, tofauti ambazo tunaweza kusema zimekithiri labda, zimeugharimu mkoa Wa kigoma, zimeigharimu Tanzania"


"Tukaacha kupambana na Chama cha Mapinduzi tukaanza kupambana wenyewe kwa wenyewe. Hili ni kosa lililougharimu Mkoa wa Kigoma na kuigharimu nchi yetu"


"Lakini misiba ni fursa ya upatanisho, ni fursa ya watu kutafakari; Tofauti zetu zinaweza kuwa kubwa kuliko za adui yetu?"


"Leo Zitto na ACT, tumelia nao Dar es salaam, tumelia nao Dodoma, tumelia nao Kakonko na tutalia nao kijijini kesho"


"Zitto na ACT hawawezi kuwa wagomvi na wabaya Wa CHADEMA kuliko Chama cha Mapinduzi"


"Kwa misingi hiyo, ninachotaka Kukieleza kwa viongozi wangu Wa Chama na ninataka Mheshimiwa Zitto usimame na kutuhakikishia...Njoo hapa. Unajua huyu ni Mwanangu nimemlea mwenyewe na ninamjua" (Anamwita Ndugu Zitto jukwaani. Zitto anasimama na kupanda jukwaani)


"Huyu ni kijana wangu, ninamjua sana"


"Ninachokisema ni hiki; kwa mambo waliyotufanyia CCM leo Kakonko; kwa mambo waliyoifanyia familia ya Bilago na waombelezaji wote hawa na Watanzania kwa ujumla, hatuna sababu ya kutofautiana katika harakati zetu"


"Tunastahili kulia pamoja, kucheka pamoja na kuumia pamoja"


"Hili jimbo litarudia uchaguzi. ACT, CHADEMA na Chama kingine chochote cha upinzani kinachotaka kushirikiana, tutashirikiana kuhakikisha tunaweka mgombea mmoja. Kama Zitto anakataa, akatae hapa mbele ya watu"


"Sisemi mgombea lazima atoke CHADEMA. Hapana. Ninachosema tunaweka mgombea mmoja katika umoja wetu. Na muungano huu utakwenda nchi nzima"


"Toa kauli Kamanda.." (Kisha anamkabidhi Kipaza sauti Zitto)

.......


Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo.


"Mwenyekiti wa Mkoa Wa Kigoma na Katibu wako njooni hapa" (Ndugu Sendwe Mbaruku, Mwenyekiti wa Mkoa na Juma Ramadhani, Kaimu Katibu Wa Mkoa Wa Kigoma wanapanda jukwaani)


"Maelekezo yangu (Anawageukia Katibu na Mwenyekiti wa Mkoa wa Kigoma) hapa Buyungu, kwa heshima ya Mwalimu Bilago, liwalo na liwe, tutaweka Mgombea mmoja"


"Hata ikitokea wengine wakakengeuka, sisi na CHADEMA tunalishana yamini tutaweka mgombea mmoja ilimradi awe ni mgombea anayekubalika na anayeweza kushinda ili tulinde heshima ya Mwalimu Bilago na heshima ya Mkoa Wa Kigoma"


"Haijalishi atoke Chama gani na sitaki hadithi za konakona. Tunachoangalia ni mgombea mwenye ubora. Wote tutafanya kampeni pamoja"


"Mwenyekiti toa ahadi yako hapa" (Anampa kipaza sauti Mwenyekiti wa Mkoa Wa Kigoma wa ACT Wazalendo)

......


Sendwe Mbaruku, Mwenyekiti wa Mkoa Wa Kigoma, ACT Wazalendo


"Habari ya jioni wananchi Wa Buyungu. Kauli ya Kiongozi wetu wa Chama tumeichukua na tutaifanyia kazi. Asanteni sana"

.....


Zitto Kabwe, Kiongozi wa Chama ACT Wazalendo.


"Mwenyekiti (Mbowe) mimi nimemaliza kwa upande wangu".


........


Freeman Mbowe, Mwenyekiti, CHADEMA


"Ngoja kwanza niwaulize (Anawageukia Mwenyekiti na Katibu Wa Mkoa Wa Kigoma Wa ACT). Wewe (Mwenyekiti wa Mkoa) ulikuwa CHADEMA? (Mwenyekiti anakubali). Wewe ulikuwa CHADEMA? (Katibu Wa Mkoa anajibu alikuwa CUF kabla ya kujiunga na ACT). Tumemaliza. Asante sana Mheshimiwa Zitto na tutaweka mgombea mmoja"


"Tusiishie Buyungu. Tusiishie hapo. Hatuwezi kuendelea kujenga siasa za mifarakano katika nchi hii. Lazima tutafute namna ya kumaliza tofauti zetu na tuendelee kuwa wamoja"

........

Transcription hii imefanywa na Ado Shaibu, Katibu Wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi, ACT Wazalendo

Simu: 0653619906


—————————


Mwelekeo wa Chama cha ACT Wazalendo Katika mwaka 2018


1. Kupigania Haki za Wafanyakazi kupitia Vyama vya Wafanyakazi na haki za raia kupitia vyama vya Wakulima, Wavuvi, Wafugaji na Wafanyabiashara wadogo kwa kujenga ushirikiano wa kipambano na Jumuiya hizo za Wananchi.


2. Kuongoza juhudi za Ushirikiano na Vyama vingine vya upinzani kwa shabaha ya kuimarisha Demokrasia ya vyama vingi nchini kwa kufanya vikao vya Mara kwa Mara na Viongozi wa Vyama vingine na kufanya shughuli za pamoja.


3. Kuendelea kusemea Haki za Kijamii kama Elimu na Afya na kuongeza juhudi za kupigania Haki ya Hifadhi ya Jamii kwa Wananchi wote hasa Wakulima kwa kushawishi kuanzisha Fao la Bei katika mfumo wa Hifadhi ya Jamii nchini na Bima ya Afya kwa kila Mtanzania.


4. Kuendelea kushawishi Sera za Uchumi zinazomkomboa mwananchi wa kawaida kwa kukosoa Sera zinazodidimiza Maendeleo ya Uchumi na kupendekeza Sera mbadala.


5. Kujikita Katika Uimarishaji wa Chama kwenye ngazi zote na kufanya Mkutano Mkuu wa Chama Mwezi Agosti Jijini Mbeya sambamba na Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia 2018.


Imetolewa na


Kamati Kuu ya Chama Cha ACT Wazalendo

Januari, 2018


———————————
 
Kuongoza juhudi za Ushirikiano na Vyama vingine vya upinzani kwa shabaha ya kuimarisha Demokrasia ya vyama vingi nchini kwa kufanya vikao vya Mara kwa Mara na Viongozi wa Vyama vingine na kufanya shughuli za pamoja.
Hongera sana Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe Freeman Mbowe kwa kuamua kuunda Umoja mmoja ni maslahi mazito ya nchi yetu ni imani yetu huu Umoja utakuwa na mafanikio kwa maendeleo ya Taifa letu
Zitto ni imani yetu umeamua kujiunga ndani Umoja huu kwa ajili maslahi mapema ya nchi yetu
 
Zitto Mkutano huu wa akina Mbowe kwenye majimbo ya wenzao ulipata kibali kweli?
au waliamua kuasi.
 
Sawa sawa tunataka muwe na umoja wa kitaifa ivyo ivyo hongereni sana
 
Hakuna mwanasiasa anayejali maisha ya wananchi wanajali maslahi yao tu.Wanapiga hesabu za kuchukua.madaraka na si shughuli ya msiba iliyowapeleka.
 
Pamajo na ushirikiano vyama vya upinzani kuwa muhimu priority is/should be katiba mpya katiba mpya katiba mpya.
 
Tunawapa ushirikiano.. Ila tutawapa ushirikiano zaidi mkiipigania Katiba mpya na Tume huru.

Never lose hope.
 
.....
....Democratic Front ...Moto wa Kakonko angaza Tanzania

KUMEKUCHA ...lumumba jipangeni
 
Mimi ndugu, yule bwana,ubinafsi ni jambo baya sana likimkaa mtu rohoni na haswa pale anapojaribu kutabanaisha kuwa yeye ni bora zaidi kwenye jambo linalohitaji umoja na uaminifu.

Busara na hekima na kujishusha ni silaha kubwa na daraja la upendo!!
 
Hawa majamaa ni ma-bogus kweli kweli. Hawana makakati wa maana isipokuwa ujanja wa kisiasa tu. Ni watu wa matukio. Unasubiri mtu kafa ndipo utangaze mipango yako ya kisiasa badala ya mipango ya mazishi! Ni upuuzi tu. Kwa wasiojua, Chadema ndio inaelekea kuzimu hivyo. Kwa utaratibu wa UKAWA, mwaka 2015, jimbo ya Buyungu lilikuwa limegawiwa chama cha NCCR -Mageuzi. Na mgombea wa chama hicho alikuwa anakubalika kwani kwenye uchaguzi wa 2010 alisemekana kushinda lakini alidhurumiwa na CCM. Alifungua kesi na alipokuwa akielekea kuona ushindi, Mbatia akamuamuru afute kesi. Kisa? Mwenyekiti wake James Mbatia alikuwa amepewa Ubunge wa kuteuliwa na Kikwete. Kwa hiyo mgombea huyo alipogombea tena mwaka 2015 waha wa Kakonko walijawa matumani ya kumchagua tena kupitia UKAWA. Chadema walimwekea mgombea na kisha kumfanyia fujo. Hakushinda. UKAWA ulikuwa na mkakati, hii Front ni ujanja. Hakuna kitu hapo. Tujipe muda tu kabla ya kusikia wahusika wakilumbana na kulalamikiana. Usaliti!
 
Mimi Zitto huwa sikupendi kwa vitabia vyako fulani ambavyo unaweza kujirekebisha, kiburi na ego.

Kama ni kweli mmemaanisha badi jiandae kikamilifu kuwa mgombea Urais wa UKAWA mwaka 2020, UKAWA haina mgombea urais mwenye sifa zako na mahitaji ya wakati, tena mwambie kabisa Freeman Mbowe Lowasa game yake is over.

Hamasa ya uchaguzi uliopota kama Lowasa angekuwa na uwezo wa kulitawala jukwaa kama wewe hata kama kura zinachakachuliwa lakini undecided voters wote wangempigia Lowasa.

Msirudie makosa, hakuna mgombea ajaye mwenye sifa za kukuzidi wewe hasa kutokana na mahitaji ya wakati na Rais aliyepo madarakani anahitajika mtu mwenye uwezo wa kuongea na akaeleweka.

Pointi nyingine muhimu, mimi ni mkristo tena kindakindaki ila awamu hii waislamu wanasomeshwa namba huenda si kwa makusudi lakini huo ndio ukweli nina imani kura za waislamu zitaangukia kwako.

Kama kuna mpumbavu ataniona mimi ni ni mdini huyo ni fala tu hajui siasa, Raila Odinga wakati akipambana na Mwai Kibaki aliingia MoU na waislamu wa Kenya na akamchukuwa Najib Balala akaiteka Mombasa na akashinda uchaguzi.

Unachotakiwa kufanya ni kucheza na weakness za ksheria kadi ya Chadema unayo ilipie miakab10 mbele, huyo Mbowe na Chadema wenzake kama siyo wanafiki wewe ndio mgombea wa UKAWA.

Ila ndugu yangu ulikuwa na papara mno na yule bogus Kitila Mkumbo, wewe ndio ulikuwa wa kurithi uewenyekiti wa Chadema sasa hivi na kuwa mgombea Urais lakini ulishindwa kuwa mvumilivu na hili litaendelea kukugharimu kutoaminika na hata huu ushauri wangu wa wewe kuwa mgombea wa UKAWA historia inaweza kukuhukumu.

Cha msingi jifunzeni kuwapa elimu ya kusiasa wafuasi wenu wajuwe wazi kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu bali kuna maslahi ya kudumu.

Kwa sisi tulio na mawazo huru huu ni wakati wako sahihi kugombea Urais wa Taifa hili, tusidanganyane UKAWA haina mgombea, Tundu Lisu hata akipona hana sifa za kuwa Rais wa nchi labda awe waziri mkuu au waziei wa sheria na katiba, Lisu is too radical, hiyo peke yake siyo presidential material.
 
Hii demokrasia ya kutumia misiba kisiasa inatia kinyaa
 
Huu muungano wa MboKa utadumu milele so long as hamna ACT atakayeleta pua yake jimboni Hai kugombea
 
Tatizo sio CCM ..ila tule tuvyama tudogo tusivyo na wabunge..kama wote wakiungana CCM watapata wakati mgumu sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom