Maktaba ya Mtwa Mkulu: Masimulizi ya James Alkando

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Sep 11, 2013
8,098
9,993
Baada ya kuwa kimya kwenye sekta hii ya uandishi leo naangusha wino wangu kuwapa simulizi. Huku nikiwa na machungu ya kifo cha muandishi wa zamani wa masimulizi ya kurudi kwa James akeke basi hisia zile zimenipa kiu ya kuwaelezeeni yale yaliyompata JAMES ALKANDO Shujaa wa jeshi la polisi. Aghalabu si mwanzo kuifanya kazi hii ya uandishi kwani kupitia kikundi cha make studio tukijiita simple ten miaka ile shule ya msingi mgololo tukiwa na kina David muhina, Aloyce msilu, Godfrey Namende, Israel Muhavile kwakuwataja japo wachache tuliweza kuifanya kazi hii tabaruku kwenu....

JIJI la Dar es salaam ni jiji la shughuli nyingi nchini Tanzania. Ni jiji ambalo wakuu wengi wa serikali na watu maarufu wanaofisi zao na makazi yao.

April, mwaka wa kwanza wa utawala wa rais John John Bashingu kulitokea wimbi kubwa la uvamizi. Kwa kuanza nyumba za matajiri wakubwa zililengwa. Lengo kuu la mvamizi ilikuwa ni fedha ingawa mara kwa mara baadhi ya matajiri wakubwa waliuliwa akiwemo MC Lugar mmarekani na rafiki wa rais John John Bashingu.

Baada ya matukio kadhaa kikao cha matajiri wakubwa kilikaa kujadili namna ya kutumia fedha yao na ushawishi walio nao kumkabili mvamizi huyu ambaye kutokana na kutokuwa na jina jamii ilimuita "mvua" kutokana na uvamizi wa kasi na ghafla. Matajiri hawa walikubaliana kutoa fedha za kitanzania sailing bilioni 100 kwa jeshi la polisi la taifa yaani Taifa police force TPF.

Muheshimiwa rais alionekana kwenye vyombo vya habari akiipokea fedha hii ambayo ni cash na akaikabidhi kwa mkuu wa jeshi la TPF Jenerali Bitingo. Mkuu wa TPF aliahidi kupambana na "mvua" na aliweka wazi mazungumzo yanayoendelea kati ya TPF na NSS (National security service) wanausalama wa Korea kusini ambapo mazungumzo haya yanaendelea kujenga ushirika wa namna gani watakabiliana na mvamizi huyu wa kutisha. Mkuu wa TPF siku hiyo aliwataarifu matajiri kuwa waendelee kuwa na amani kwani mwisho wa maharamia hao umefika. Aidha matajiri hawa waliweka azimio kuwa ili kuokoa maisha yao fedha zao zote zitaifaziwa Bank na itakuwa marufuku mtu kukaa na fedha nyumbani.

Ghafla usiku wa saa sita siku hiyo hiyo mitandao ya kijamii ilianza kumuonesha mtu aliyekuwa akiongea moja kwa moja. Mtu huyo alikuwa ni mvua akiwa na majeraha makubwa na damu zikichuruzika. Watu wengi walipigiana simu na kuamka ili wamtazame. Television ya Taifa jirani la kenya Citizen ilirusha wazi tukio hili na mmoja wa watazamaji alikuwa mtukufu rais John John Bashingu.

"Ndugu wananchi wa Tanzania," alianza msemaji huyo mwenye sura inayo tisha na kuchuruzika damu"......naanza kwa kulipongeza jeshi la polisi kwa kulinda fedha iliyotolewa na matajiri. Nilijaribu kuiba ila nimefanikiwa kiasi kidogo tuu cha shilingi billion kumi tuu ingawa ni moja kati ya mafanikio makubwa kwa kazi yangu. "Alimpongeza sana Jenerali Bitingo kwa mapambano makali kati ya wawili hao wakati Jenerali huyu akiokoa fedha hizo. "Mvua" aliitimisha kwa kusema hana hakika kama mkuu wa polisi atakuwa hai.


Usiku huo filimbi na Ving'ora vilisikika jiji zima huku askari wa majeshi yote wakielekea ofisi ya mkuu wa polisi katika jengo jipya maeneo ya sala sala. Lakini walikuwa wamechelewa walikuta zaidi ya askari 60 wakiwa wameuliwa kwa sumu kali ambayo huenda iliwekwa kwenye chakula. Ofisini kwa mkuu wa jeshi walimkuta ameuliwa katika hali inayoashilia mapambano makali sana na ilionekana alikuwa amejitetea kwa kutumia kisu baada ya kushambuliwa kwa ghafla.

Aidha alimeza funguo ya strongroom tumboni mwake inaonekana baada ya kuhisi kuwa hataweza kukabiliana na mvua. Hata hivyo hakuna siku ambayo mvua alijeruhiwa vibaya kama siku hiyo.. Mkuu huyu na askari wenzake walizikwa kwa heshima makabuli ya kinondoni baada ya mwili wake kupasuliwa na kutolewa funguo ya chumba chenye fedha. Kwenye kabuli lake ulijengwa mnara mkubwa ulioandikwa " Mahali hapa amelala Shujaa jenerali Bitingo"

Mvua alihitimisha Tanzia hii kwa kuandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa "ulikuwa usiku wa kifo, usiku wa mapambano makali. Kwa sasa nitaelekeza uvamizi wangu kwenye mabank na kwakuanza benk kuu ya Taifa yaani TB Taifa Bank ijiandae"

Mapema Asubuhi baada ya mazishi mtukufu rais alihutubia Taifa.Alizungumzia tukio hili kuwa ni tukio la aibu kwa taifa na libido vumilika. Aliwashusha vyeo wakuu wote nane wa vitengo vikuu vya TPF bila kuwaogopa. Aliahidi nafasi zao zitashikiliwa na maafisa wabunifu hapo baadae. Alihitimisha kwakusema huenda mvua ni mpango wa wahalifu wengi na hawezi kuwa tishio kwa siku zote. Baada ya Tangazo hili mataifa mengi yalianza kutoa salamu za Pole kwa serikali ya Tanzania.

Wakati ulinzi mkali ukiimalishwa kwenye ofisi za TB Bank ya Taifa Dar es salaam. Iliripotiwa kuwa Bank ya TB Tawi la arusha inawaka moto. Mabilioni ya fedha yaliibiwa na mtu mwenye kasi ambaye kwenye camera alionekana anamajeraha makubwa. Askari walizingira Bank hiyo yenye utajiri wa fedha za kigeni lakini walikuwa wamechelewa sana. Rais, alitaja hali hiyo kuwa ni ya taaruki alimsihi mvua wakutane ili waweze kumaliza tofauti zao.

Baada ya siku nne zilianza kuenea taarifa kuwa hata ikulu ya Dar es salaam ni muathilika wa uvamizi huo, taarifa hizo zilidai kuwa mvamizi huyo ameingia katika kuta za ikulu ya dar es salaam ambako alikabiliana na ulinzi mkali ambapo aliruka tena na kujitupa Baharini. Vikosi vya ulinzi vilimficha rais katika jengo la makao makuu ya mkoa wa pwani kibaha kwa muda. Mkuu wa majeshi wa Taifa alitoa waraka wa kijeshi kuwa rais ametangaza amri ya hatari.

Naye mvua huko face book aliandika kuwa " ni mguu umeniponza, sasa nitapumzika kupata matibabu ya mguu wangu watanzania niombeeni"

Mvua alikuwa amefanya juhudi zote za kueneza vitisho kila kona na kuzusha taharuki isiyoelezeka. Kila vijiwe, kila ofisi na vyuo walimzungumzia mvua.

Baada ya siku kadhaa mtukufu rais alionekana hadhalani. Alimteua mtu asiyeona na mkulima kutoka milima ya upareni aliyeitwa Brigedia Shirima kushikilia usukani wa jeshi la polisi kama mkuu wa jeshi. Mzee huyu alizungumza kwa njia ya simu na BBC akishukuru kwa uteuzi huo na kuukubali.

Aliahidi kuwa atafanya kazi hiyo kwa mwaka mmoja tuu na baada ya hapo atarudi katika kazi yake ya kulima tangawizi aliyodumu nayo kwa miaka 15 tangu alipo achana na kazi ya Jeshi.Alipo ulizwa kama anaweza kupambana na mvua alisema " kama Mungu yupo upande wa watanzania basi atatoa haki kwa watanzania" alisisitiza kuwa Jeshi la polisi la Taifa TPF liliasisiwa kwa misingi ya weredi na nidhamu ya hali ya juu hivyo kazi yake kubwa itakuwa ni kurejesha nidhamu ya jeshi hilo.

Siku hiyo watanzania walionyesha hasira kali juu ya uteuzi wa mzee huyo tena asiyeona. Walimuomba rais ajiuzuru ili wao wawe salama. Mvua naye katika Facebook alimpongeza shirima kwa uteuzi na kumuomba wakutane splendid bridge mchana ili ampe salamu zake za uteuzi.

Wanazuoni wa chuo cha Dar es salaam (DU) walikoleza moto mjadala huu kwa kusema ni mapema sana kumlaumu rais kwani mpaka sasa hakuna anaye mjua shirima ni nani? Waliwasihi watanzania kudadisi shirima ni nani badala ya kumtathmini kwa hali yake ya kuto kuona.

Usiku, Brigedia shirima alitoa taarifa ya awali kumuhusu mvua ambapo alisema kuwa mvua ni mpango wa mualifu mmoja tuu mwenye wasaidizi wachache. Alimuomba rais aondoe amri ya hatari. Mtukufu rais hakukawia usiku huo huo aliondoa amri ya hatari.

Mvua nae hakuwa mbali alijibu kwa kumpongeza shirima kwa majigambo yake ambapo aliomba kukutana nae baada ya siku tatu saa sita mchana salenda bridge.

Itaendelea Jumatano
 
Back
Top Bottom