Maandamano yanaweza kulindwa na helkopta juu ili asitokee wa kuhujumu raia na mali zao. Waandamanaji wabainishe madai yao na wanamtaka nani ayapokee maandamano yao. Wapi yaanzie na wapi yaishie kisha watu wasambae kurudi walikotoka kwa amani. Wakisema wanataka waishie ikulu au bungeni, au sehemu sensitive kwa nchi itakuwa ni shughuli pevu watakubaliana na vyombo vya ulinzi na usalama kwenda huko wanakotaka kwenda, waridhiane mapema kabla ya siku hiyo ili pasijetokea mauaji ya halaiki nchi ikaaibika kuwa ni ya kishenzi haithamini uhai wa watu wake