Makosa ya Sheria ya makosa ya Mitandao

Shebbydo

JF-Expert Member
Feb 12, 2015
1,174
1,937
Habari wana JF,

Ni masikitiko makubwa kwa hili lililotokea la kukamatwa kwa mwanzilishi na mmiliki wa huu mtandao wa jamii forum, bwana Maxence Melo. Nimejaribu kufuatilia ili kujua ni nini kilichosababisha Max kukamatwa, napata majibu kuwa ni kwa sababu amekataa kutoa taarifa za wanachama wa mtandao huu wa jamii forum.

Swali lililonijia haraka kichwani, ni kwa nini Max amegoma kutoa taarifa za sisi wateja wake. Pia jibu la haraka nililojijibu mimi mwenyewe ni kuwa analinda "Privacy Policy" ambayo ni "Internationally" kwa watumiaji wa mitandao yote duniani. Hivyo nikaona Max yupo sahihi kulinda "Privacy" ya wanachama wake.

Je, hawa polisi kwa nini wanamng’ang'ania Max atoe taarifa za wanachama wa mtandao wake? Hawa nao wamesimamia kwenye sheria ambayo wananchi waliipigia kelele kuwa kuna vipengele ambavyo vinaingilia "Privacy" ya mtu. Sheria inayoitwa ‘Sheria ya makosa ya mitandao’. Sheria ambayo inawapa nguvu polisi kuchukua kifaa cha mawasiliano cha mtu na kwenda kukaa nacho ili kukifanyia uchunguzi.

Watanzania wenzangu hii sheria ndiyo zimwi litakalotula litumalize. Watunga sheria waliipitisha sheria hii kwa kuangalia manufaa ya upande mmoja tu, hawakuangalia upande mwingine wa "privacy" ya mtu. Sikatai kuwa hakuna makosa yanayofanyika jamii forum ambayo yanaweza kuleta taharuki. Yapo, kwa mfano kumekuwa na wimbi la taarifa za uwongo na upotoshaji, matusi na mambo mengine yasiyofaa lakini uongozi wa jamii forum kutokana na sera zake umekuwa ukipambana nayo kwa kuchukua hatua mbalimbali. Kama vile, kufuta "thread" hizo na kumpa adhabu mtu huyo ya kutokuwa na uwezo wa kushiriki jamii forum kwa kipindi fulani.

Tatizo ninaloliona hapa ni kwa huu utawala wa awamu hii, umekuwa ni utawala ambao unaamini katika matumizi ya nguvu nyingi badala ya majadiliano na maridhiano. Haikuwa na maana yoyote ya kutumia nguvu za kukamata na kuweka ndani. Tayari kulishaonekana tatizo katika utumizi wa mitandao ya kijamii, ingefaa zaidi kuwaita na kuwaeleza wamiliki wa jamii forum kuwa katika haya yanayoendelea katika mtandao wenu, yanaweza kuleta athari katika taifa letu. Hivyo simamieni vizuri sheria zenu mlizojiwekea huko, ikiwezekana ziongezeeni makali. Sidhani kama Waanzilishi wa jamii forum waliianzisha kwa madhumuni ya kuleta taharuki katika nchi zaidi ya kutaka kuwaunganisha watu ili waweze kubadilishana mawazo mbalimbali. Ila kulipo na watu wengi hakuwezi kukosa wengine wenye mapungufu fulani fulani. Katika watu takribani 360,000 kweli wakose waongo, wanafiki na hata wachonganishi? Haiwezekani, kwa sababu huu ndiyo ubinadamu. Wewe soma vipi hata uwe profesa kama ni muongo ni muongo tu.

Sasa basi, rai yangu kwa jeshi la polisi na serikali kwa ujumla; tunaomba Maxence aachiliwe huru ili majadiliano yachukue nafasi ya nini kifanyike ili kukabiliana na mijadala na habari zinazoweza kuleta mushkeli kwa taifa letu. Haya matumizi ya nguvu hayatatufikisha popote zaidi ya kuleta misuguano ndani ya jamii yetu ya Kitanzania ambayo matokeo yake ni kuzalisha chuki kwa wananchi dhidi ya serikali. Huwezi kulipuuza kundi la Wananchi zaidi ya 300,000. Pia isijengeke kama si kuimarika imani ambayo tayari baadhi ya Watanzania tumeshaanza kuwa nayo kwamba serikali hii haitaki; kukosolewa, kusemwa na inaanza kuminya uhuru wa kutoa maoni. Uhuru wa kutoa maoni kwa bahati mbaya ama nzuri katika katiba yetu, haijasema kuwa yawe ni maoni mazuri tu.

Ni hayo tu nawakilisha hoja.
 
Kwa mjjibu wa katiba yetu kila mtu anayo haki ya kupata habari sasa wanapomkamata huyo muanzilishi WA jamii forum I'll kutoa siri za members wake lengo lao ni kuua Uhuru WA kupata. Na kutoa habari bsi upo kisheria serikali hii ya pombe haina lengo zuri katika kulinda democracy
 
Tatizo si taarifa za uongo,Bali kukosolewa kwa serikali.angalia post za kupotea kwa Ben.watu wa ccm walivyo comment.lakini siamini kama polisi watawatafuta hao watu.
 
Back
Top Bottom