Makosa ya rushwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Makosa ya rushwa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by KAUMZA, Aug 31, 2010.

 1. K

  KAUMZA JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2010
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 685
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Habari zenu learned sisters and brothers!!!!!
  Nimekuwa nikijiuliza sana swali hili. Je, mwananchi wakawaida anaweza kumkamata mtoa rushwa au mpokea rushwa na kumfikisha TAKUKURU au POLISI? Maana tunaona kaika makosa mengine ya jinai inawezekana.:eek2:
   
 2. P

  Pokola JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2010
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Jinai maana yake ni makosa yanayofanywa dhidi ya umma. Kila mwananchi/raia ni sehemu ya umma, kwa kuzingatia ile dhana ya Mkataba wa Kijamii [Social Contract Theory] ya Montesquieu. Kila raia ana wajibu wa kulinda mkataba huu, lakini viongozi wanasimamia tu utekelezaji wa yote yatakayokubaliwa na raia wote kwa manufaa ya wote. Rushwa ni jinai. Ni wazi kuwa kila raia anapaswa kuzuia makosa ya jinai, ikiwa ni pamoja na kukamata (siyo kuadhibu) watenda jinai, pale inapoonekana kuwa askari polisi hayupo/hatofika kwa muda muafaka katika eneo la tukio.

  Lakini ni vyema zaidi ukitoa taarifa kwa TAKUKURU, wao watakamata na kufungua mashtaka dhidi ya mtoaji/ mpokeaji wa rushwa.
   
Loading...