Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,260
- 33,860
Kuna fikra za baadhi ya watu wanaotamani itokee siku moja "makosa" ya kimtazamo na kiutendaji ya Hayati John Magufuli, aliyekuwa Rais wa Tano wa serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania YAREKEBISHWE.
Kiuhalisia makosa hayo hayawezi kurekebishwa kwa kuwa umbali aliotufikisha Magufuli inakuwa ngumu sana kurudi kwenye njia sahihi kiurahisi. Kitu pekee kinachoweza kufanyika ni kusuluhisha mitazamo yetu na uhalisia wa mambo.
Kwa mfano; chuki kati ya wafuasi wake na wale waliokuwa wanaipinga falsafa yake ya undeshaji nchi inarekebishwaje? Jee watu waliodhurika wakati wa utawala wake wanaponaje ama wale waliopotea wanapatikanaje? Leo hii hawa kina Ben Saanane, Simon Kanguye, Azor Gwanda nani anajua walipo na inawezekana wakarudishwa kwa familia zao. Lissu na wengine waliopata ulemavu zama hizo maisha yao yanaweza kurejerezwa?
Nani mwenye akili timamu anayeweza kusimamisha ujenzi wa bwawa la umeme la Nyerere kwa hatua ililofikia. Au SGR inawezaje kuwachwa wakati tayari mabilioni ya shilingi yameteketea kwenye mradi huo tayari. Nani ataruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa wakati CCM amri ya marufuku hiyo haiwahusu?