Makosa ya Edward Lowassa ni yapi ndani ya CCM?

Makosa ya Edward Lowassa ni yapi ndani ya CCM?

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,506
Kwani huyu Edward Lowassa siyo yule Edward Lowassa wa mwaka 2010 ambaye Mwenyekiti wa CCM-Taifa, Rais Kikwete aliushika mkono wake na kuunyanyua juu kuwaomba wapiga kura wa Jimbo la Monduli ili wamchague kuwa Mbunge wao huku akisema, ‘’hakuna mwakilishi mzuri nchini kushinda Edward Ngoyai Lowassa’’.
monduli11.jpg

Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Jakaya Kikwete, akimnadi mgombea ubunge jimbo la Monduli mkoani Arusha, Edward Lowasa, kwa wapiga kura wa jimbo hilo wakati wa mkutano wa kampeni 2010.
60.jpg

Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa akiwa na Edward Lowassa wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Arusha.

Kwani siyo huyu Edward Lowassa ambaye Mwenyekiti wa CCM-Taifa, Rais Kikwete aliwahi kusema kilichompata Edward Lowassa katika sakata la Richmond Development Company LLC ni ajali ya kisiasa, kwa maana nyingine, alijikwaa kisiasa na anaweza kusimama na kuendelea na safari yake ya kisiasa.

Hivi hawa baadhi ya viongozi wa CCM wanataka kutueleza Edward Lowassa wa leo ni tofauti na yule wa 2012 ambaye jina lake lilikidhi vigezo vyote na kupitiswa na vikao vikuu vya CCM kuwa mgombea Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM-Taifa ili kupambana na Dr. Salash Mokosyo Toure na Nanai Taon Konina ambapo aliwashinda kwa kura nyingi.

Kwani siyo huyu Edward Lowassa ambaye Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, amemmwagia sifa wakati wa ziara yake mkoani Arusha na kusema ni miongoni mwa viongozi waliotekeleza kikamilifu ilani ya chama hicho.

IMG_0751.JPG


Ni Edward Lowassa yupi ambaye baadhi ya viongozi wa CCM wanataka kutuaminisha kwa sasa kama jina lake linaweza kukatwa na Kamati Kuu kutokana na mapungufu kwenye vigezo 13 vya kuwachuja watia NIA wa nafasi ya Urais Tanzania kama ilivyotangazwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula.

Kiongozi yupi wa CCM mwenye uwezo wa kumvika paka kengele?
 
  • Thanks
Reactions: PPM
Hata mm nawashangaa wanaomuona hafai kwa sasa.. Yote hayo yanakuja kwa sababu ya uchu wa madaraka na kutaka kubebana hata kama mtu hana sifa ya kuwa rais..
 
Kosa lake ni kuwa fisadi na kutetea mafisadi wenzie.ebu ona cheni iliyoko nyuma yake,chenge rostam na karamagi hakika tutauzwa tukiwa wazima.say no to lowasa
 
Mtakuja na kila aina ya mapambio, lakini haosheki hata kwa Dodoki la Steel wire
 
Ukiwa mwanaccm ni lazima uwe mwehu kwa kiasi fulani endapo utampinga lowasa..... Nasema hivyo kwa sababu mfumo wa ccm haumuwezeshi mtu kuwa huru endapo anahitaji kugombea nafasi yoyote ya uongozi..... Ukitaka uwe huru ni lazima ukubali shutuma nyingi....
 
unapozungumzia ufisadi wa lowassa unatakiwa uweke bayana ni shilingi ambazo amechukua na ushaidi wake na ukumbuke kamati ya mwakyembe hajawai kuweka ushahidi wowote zaidi ya kutumika kisiasa tu
 
tatizo la watia nia weng wanadhan bila kumtaja lowassa hawauz! ndo maana lowassa amewaacha waseme wanavyoweza Ila yeye ameisha wasemehe saba mara sabin!
 
lowasa hana kosa...ni majungu ya samwel sitta na nape nnauye..mtu safi na anafaa kuingia ikulu
 
lowasa tuambie rafiki zako tutakwambia tabia zako"

misemo ya kimajungu isiyo na mantiki....yesu kristo alisema hakuja kuwatafuta watu wema bali wenye dhambi ili wapate kutubu...unataka kusema Yesu kristo kwa kuwaita wenye dhambi na yeye alikuwa muovu??!!
 
Makongoro for President.. Over

akamalizane na picha zake za gesti....halafu akalipe na bill za kwenye magrocery...halafu bado kesi za malezi ya watoto wake wa nje zitafunguliwa kwa kasi ya umeme punde si punde
 
Back
Top Bottom